KUFELI KWA FIGO (KIDNEY FAILURE)
KUFELI kwa figo, ni hali ambayo hutokea taratibu na ni vigumu kwa mtu wa
kawaida kujua kwamba figo zake zinaelekea kufeli. Yapo mambo mengi
yanayoweza kusababisha figo ikafeli, yakiwemo magonjwa kama kisukari,
shinikizo la juu la damu, kutumia dawa kali kwa kipindi kirefu, kutokwa
na damu nyingi wakati wa kujifungua au kwenye ajali, kutumia dozi kubwa
za madawa ya kulevya nk.
Mgonjwa anapofikia hatua ya figo yake kufeli, ni lazima kilichosababisha
akafikia hatua hiyo kishughulikiwe mapema ambapo akipata matibabu
sahihi kwa muda muafaka, figo zinaweza kurudi
kufanya kazi kama zamani (kwa baadhi ya watu). Matibabu hayo ni pamoja
na kuanzishiwa tiba ya kusafisha damu kwa kutumia mashine inayofanya
kazi sawa na figo (dialysis). Inaposhindikana, hakuna njia nyingine ya
kumsaidia mgonjwa zaidi ya kupandikizwa figo nyingine (kidney
transplant) ingawa zipo pia tiba mbadala ambazo mgonjwa hata kama
hospitalini matibabu yameshindikana, anaweza kutibiwa na akapona bila
kupandikizwa figo nyingine, hatua ambayo huwa ya mwisho kabisa. Zipo
dalili nyingi zinazoweza kukuonesha kwamba figo zako zina matatizo.
Dalili hizo ni pamoja na; kupungua sana kwa kiwango cha mkojo au kukojoa sana hasa
nyakati za usiku, kukojoa mkojo wenye povu jingi, maji kurundikana ndani ya mwili na kusababisha kuvimba kwa viungo kama miguu, uso na wengine huvimba mwili mzima.
nyakati za usiku, kukojoa mkojo wenye povu jingi, maji kurundikana ndani ya mwili na kusababisha kuvimba kwa viungo kama miguu, uso na wengine huvimba mwili mzima.
Dalili nyingine ni mwili kuishiwa nguvu (fatigue), kichefuchefu,
kusinzia mara kwa mara, kukosa pumzi, kupatwa na maradhi ya ngozi,
kusikia kizunguzungu, kupoteza ladha ya chakula mdomoni, kuchanganyikiwa
na kukosa uzingativu na kwa baadhi ya watu, hupatwa na tatizo la
kuzimia mara kwa mara.
Unapoona moja au zaidi ya dalili zilizotajwa hapo juu, ni muhimu kuwahi
hospitali ambako utapimwa na kuanza matibabu kulingana na matatizo yako.
Endapo mgonjwa mwenye matatizo ya figo atawahi kwenda hospitali na
kupatiwa tiba ya uhakika, atafuata masharti ya daktari na kuishi kwa
kuzingatia misingi ya afya bora, mgonjwa wa figo anaweza kuishi maisha
marefu kama mtu asiye na matatizo hayo.
No comments