USHOGA na USAGAJI UNAVYOWAATHIRI WASICHANA TANZANIA -3
KATIKA matoleo yaliyopita Ijumaa limeweza kuzungumza na watu mbalimbali
ambao kwa namna moja au nyingine wanashiriki au pamoja na wale
wanaozungukwa na watu wanaojihusisha na michezo hii ya kusagana.
Mbali ya kuzungumza na wazazi, lilizungumza na wahusika wenyewe ambao
walieleza ni kwa namna gani walianza kujihusisha na michezo hii.
Viongozi wa dini pia wamezungumza. Shehe wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad
Salim ameweza kutoa maoni yake juu ya suala hili na namna vitabu vya
dini vinavyokataza juu ya watu kujihusisha na vitendo vichafu kama hivi
na kwamba havimpendezi Mungu.
KWA NINI HAWAWEZI KUACHA?
Hata hivyo, kabla ya kusonga mbele kwa kupata maoni kutoka kwa viongozi
wengine wa dini na wanasaikolojia, turudi kwa kina dada wanaojihusisha
na vitendo hivi.
Wanayo ya kueleza kuhusu ni kwa nini hawawezi kuachana na vitendi hivi, tuwasikilize;
“Binafsi siwezi kuacha kwa sababu hata nikikutana na mwanaume sisikii
raha kabisa kama ninavyokutana na wanawake wenzangu. Tukikutana
ninafurahia tendo sana na kiukweli kuacha nimekwisha jaribu lakini
nimeshindwa kabisa,” alisema Fatuma, mwanadada ambaye ameweka wazi
kwamba anashiriki vitendo hivyo vya usagaji kwa zaidi ya miaka mitatu
sasa.
Kwa upande wa Willen wa Ilala, ambaye alikuwa tayari pia kutoa ushuhuda
wake juu ya kushiriki kwenye vitendo vya usagaji alisema kuwa watu
mbalimbali wamejitokeza na kumshawishi aache na amejaribu na kushindwa.
“Wazazi wangu walinipeleka mpaka hospitali kwa ajili ya kupata matibabu
ya kisaikolojia, lakini nilipojaribu kuachana na huu mchezo na kutafuta
mpenzi nilijikuta nikiishi bila furaha.
“Ile raha niliyokuwa naipata wakati wa kufanya tendo ninapokuwa na
mwanamke mwenzangu sikuweza kuipata tu jambo ambalo lilisababisha niwe
sikutani mara kwa mara na mpenzi wangu, baadaye akaniacha.
“Aliponiacha tu nilirudi kwenye mchezo wangu niliokuwa ninafanya awali
ambao kwa sasa ndiyo mtu hanielezi kitu kabisa kwenye vitendo hivi,”
alisema Willen.
Willen aliendelea kueleza kwamba imefika hatua analazimika kutafuta wanawake tofautiotofauti kwa ajili ya kukidhi haja zake.
Mbali na kuwatafuta wanawake hao pia analazimika kuanzisha uhusiano na
watu wenye umri mkubwa na fedha ili tu waweze kumpatia fedha ambazo
atakwenda kuwahonga kina dada ambao anawataka washirikiane naye kwenye
mchezo huo wa usagaji!
“Kuna wakati mimi mwenyewe huwa ninajiona kwamba nipo kwenye basi ambalo
si sawa. Lakini ndiyo hivyo tena, siwezi kuacha. Huwezi amini kuna
wakati mpaka nawagombanisha wanawake wenzangu.
“Ninawasichana watatu ambao nipo nao kwenye uhusiano wa kimapenzi na
wanasoma kwenye chuo fulani hapa Dar. Wasichana hao wamekuwa kwenye
ugomvi mkubwa wakinipigania baada ya kufahamiana kwamba wote ninatoka
nao kimapenzi,” alisema Willen.
WANAUME NI CHANZO
Kwa upande mwingine uchunguzi wa Ijumaa uliweza kuangazia pia zaidi ya
akina dada hawa kushawishiwa na wenzao kujiingiza kwenye vitendo hivi,
zipi sababu zaidi zinazowafanya kinadada wengi kwa sasa kujitumbukiza
kwenye lindi hili la usagaji.
Baadhi yao ambao wamezungumza na gazeti hili wameeleza kwamba wanaume ni
chanzo cha kuwafanya wao kujiingiza kwenye michezo hiyo.
Msikie Rose; “Kiukweli mimi nilijikuta kwenye ushawishi wa kuingia
kwenye tabia hii baada ya wapenzi wote niliokuwa ninaanzisha nao
uhusiano kuwa pasua kichwa. Kila mpenzi hakuwa mwaminifu kwangu,
nilipokuwa nikiwalilia wasichana wenzangu waliniambia niachane na
wanaume na kwenda kwao ili tuliwazane.
“Ndiyo hivyo tena nikajikuta nimeanza huo mchezo na sasa imekuwa ngumu
kuacha kufanya hivyo ingawa nimejaribu mara kadhaa kuwa kwenye
uhusiano.”
Kwa upande wa Janet ambaye katika mitaa ya Tandale anajulikana kwa jina
la J wa Ukweli, alisema kwamba kilichomfanya ajitumbukize kwenye masuala
haya ya kusagana ni kutokana na kutoridhishwa kimapenzi na mpenzi wake.
“Mpenzi wangu alikuwa haniridhishi kimapenzi, niliogopa kumweleza kwa
kuhofia kwamba atajisikia vibaya. Nikawaeleza rafiki zangu, lakini nao
waliniambia kwamba nisiumizwe kichwa na hilo maana wao walikuwa na kundi
linaitwa ‘hatutaki stress’, yaani wanawake ambao hawataki adha za
wanaume.
“Ni kundi linaloundwa na kina dada wanne, ambao walikuwa wanaburudishana
wao kwa wao kutokana na kutoridhishwa kimapenzi na wapenzi wao, pamoja
na dhana ambayo imejengeka kwa sasa kwamba wanaume wa Dar es Salaam
wengi wana matatizo ya nguvu za kiume,” alisema J wa Kiukweli.
J aliendelea kusema kwamba mbali na rafiki zake hao, kuna makundi mengi
kwa sasa kwenye mtandao wa Whatsaap ya kinadada ambao wanajiita
‘hatutaki sterss’ ambao wapo kwa ajili ya kuridhishana wenyewe kimapenzi
na kwamba huhamasishana kwa kuwakusanya kinadada wengine na kuwafanya
kuwa wanachama wao ili waweze kuwa na washirika wengi na kwamba hiyo ni
njia waliyogundua ya kuwakomoa wanaume!
Mpenzi msomaji, kwa leo tuishie hapa, wiki ijayo tutakuletea uchambuzi wa wanasaikolojia na madaktari
No comments