Dawa asili na vyakula 20 vinavyotibu tatizo la msongo wa mawazo (stress)
Dawa asili na vyakula 20 vinavyotibu tatizo la msongo wa mawazo (stress)
Hali ya mfadhaiko inasemwa
kutokea wakati ubongo unapokabiliana na tatizo la mvurugiko wa akili na
kujikuta ukishindwa kuendana na hali zingine zinazohitaji umakini kwa
wakati mmoja. Jambo hili linaweza kuuteka ubongo na kudhoofisha uwezo
wake.
Hatimaye hali hii ya ufadhaikaji katika ubongo inaweza kutengeneza
dalili tofauti ambazo zimepachikwa majina mengi kwa mjibu wa sampuli
tabia za nje anazozionesha mtu.
Idadi kubwa zaidi ya watu wanazidi kupatwa au wanategemewa kupatwa na
aina fulani fulani za mifadhaiko. Baadhi ya aina za mifadhaiko ni hali
za asili katika hatua za maendeleo na kukua kwa mtu.
Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu uwezo wao ni mdogo kushughurika na woga, wasiwasi na hamaki zinazohusiana na mifadhaiko. Kwa bahati mbaya tena wanapotafuta msaada wa kitaaluma, wanapewa aina fulani za madawa.
Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Utafiti
uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonyesha kuwa akili hutumia
sehemu kubwa ya nguvu ya mwili. Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko
huchangia sana katika kutokea kwa magonjwa mengi mwilini zaidi ya 50. !
Inaelezwa na wataalamu kwamba karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara wote
duniani wanasumbuliwa na maradhi ya kutoridhika, kufunga choo, vidonda
vya tumbo na maradhi ya moyo. Na wafanyabiashara ambao hawajui namna ya
kupambana na wasiwasi au mashaka hufa wakiwa vijana.
Wasiwasi na hofu ya maisha humfanya yeyote kuwa mgonjwa. Mvurugiko wa
hisia una matokeo hasi katika afya ya mwili, pia wasiwasi na hofu ya
maisha huweza kuleta magonjwa yanayoweza kuuwa kabisa sawa sawa na
inavyotokea pia kwa magonjwa yale yatokanayo na lishe dhaifu.
Baridi yabisi, maradhi ya moyo, tezi, kisukari, vidonda vya tumbo, kansa, yote yanaweza kusababishwa na mvurugiko wa mawazo.
Utafiti wa kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi
tunavyomudu kudhibiti mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa
kiwango gani afya zetu zilivyo madhubuti au zilivyo dhaifu.
Ingawa utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo
wa kinga ya maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili
au mawazo yatokanayo na shida za maisha.
Majaribio yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, watu
wanaosumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, watu waliopewa talaka na wale
wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi
mara kwa mara kutokana na mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa.
Mfano katika kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata
taarifa; neva zenye kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na
adui. Hapo moyo huenda mbio, msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba
kwenye misuli kwa ajili ya maandalizi ya mapigano au makabiliano na
adui.
Oksijeni na virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu
awe tayari zaidi kwa mapigano, na hapo mnyunyizo wa adrenalini, homoni
inayohusika na uzalishwaji wa nguvu mwilini huongezeka.
Kadri mfadhaiko unavyokuwa ni wa muda mfupi, ndivyo pia athari zake
zinavyokuwa ni fupi. Lakini pindi mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu
kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo
mengi kila mara, athari zake nazo hudumu kwa muda mrefu.
Dawa asili na vyakula 20 vinavyotibu tatizo la msongo wa mawazo (stress)
Katika kujidhibiti au kujitibu na mfadhaiko au stress jambo la kwanza ni
kutambua nini chanzo cha huo mfadhaiko wako, ukishapata kujuwa chanzo
ni rahisi kupata suluhisho kwa haraka.
Tambuwa kuwa kila mtu ana matatizo na kila mtu hufeli katika mipango
yake na kila mtu hupata hasara. Tofauti ni kwamba wakati baadhi ya watu
wanaweza kumudu kudhibiti mvurugiko wa mawazo, wengine hawajui kabisa
nini cha kufanya na matokeo yake hupatwa na mfadhaiko ambao huweza
kusababisha maradhi mengi mwilini bila idadi.
Kama utakubali kuyapokea maisha kama yanavyokuja, ukaacha kuyakopa
maisha ya jana na ukaacha kuhofu maisha ya kesho, ni hakika kabisa
utaweza kujidhibiti kupatwa na mfadhaiko.
Kuna watu wakipatwa na matatizo huyaficha kimya na kuendelea kuumia
ndani kwa ndani peke yao, hii ni tabia mbaya sana kiafya, unapopatwa na
tatizo jaribu kutafuta mtu au watu unaowaamini na uwaeleze tatizo lako
hata kama hawatakusaidia moja kwa moja lakini mawazo na ushauri wao tu
vinaweza kuwa ni dawa tosha ya mfadhaiko au stress yako.
Pamoja na hilo dawa asili na vyakula vifuatavyo vitakusaidia kupunguza
kama siyo kutibu kabisa hali hii mbaya inayoendelea kuwasumbuwa mamia ya
watu kila siku.
1. Iliki
Iliki inao uwezo wa kuzirudishia nguvu mpya seli za mwili na kusafisha
mwili jambo ambalo mwishowe linasaidia kuweka sawa akili yako.
Kunywa chai yenye iliki kila siku. Iliki inaweza pia kuongezwa kwenye vyakula na mboga nyingi jikoni. Kazi ni kwako.
2. Kungumanga
Kungumanga hufanya kazi kama dawa ya kuchangamsha ubongo na kuondoa uchovu na mfadhaiko.
Kama matokeo yake matumizi ya tunda hili kutakufanya kuwa na akili yenye
utulivu nah ii ni moja ya dawa rahisi kabisa za kutibu mfadhaiko.
Tumia nusu kijiko kidogo cha chai cha unga wa kungumanga ndani ya kikombe kimoja cha chai ya kijani kutwa mara 1 kila siku.
2. Korosho na maziwa ya moto
Korosho zina vitamini C kwa wingi ambayo inaweza kuuamsha mfumo wako wa neva za fahamu.
Vile vile korosho zina kitu kinaitwa kwa kitaalamu ‘riboflavin’ ambacho
huongeza nguvu za mwili na hivyo ukajisikia ni mwenye furaha na
mchangamfu.
Korosho pia zina magnesiamu, vitamini B6 na tryptophan ambavyo huhusika
na afya ya akili moja kwa moja na hivyo kukusaidia kupigana na
mfadhaiko.
Muunganiko wa korosho na maziwa ya moto unakuwa ndiyo dawa bora zaidi ya asili ya kutibu mfadhaiko wa akili.
Changanya unga wa korosho kijiko kidogo kimoja ndani ya kikombe kimoja cha maziwa ya moto na unywe yote kutwa mara 1 kila siku.
3. Baking Soda
Baking soda inaweza kusaidia kukupunguzia kiasi cha hamaki katika ubongo wako na hivyo kukuondolea msongo wa mawazo.
Sababu kubwa ni kuwa baking soda ina uwezo mkubwa wa kuondoa asidi ndani ya mwili wako.
Tumia nusu kijiko kidogo cha chai kutwa mara 1 ndani ya maji ya uvuguvugu kikombe kimoja kila siku.
4. Mafuta ya Samaki
Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali watu wengi wanaosumbuliwa na mfadhaiko wa
akili huwa wana upungufu wa omega 3 ndani ya miili yao. Na mafuta ya
samaki ni moja ya vyanzo vizuri vya mafuta yenye omega 3 ambayo
huhitajika na ubongo wako kwa ajili ya ufanisi wa kazi zake kila siku.
Kunywa kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya samaki kila siku au kula samaki wa maji baridi kwa wiki kila mara.
5. Figili
Figili (Celery) ina kiasi kingi cha ‘folic acid’ na potasiamu vitu
viwili vinavyoweza kukusaidia usipatwe na mfadhaiko wa akili kirahisi.
Hakikisha kila mara haikosi kwenye mlo wako hii figili.
6. LOZI
Lozi (Almonds) zina vitamini B12 na madini ya zinki kwa wingi ambavyo ni mhimu katika kushusha mfadhaiko wa akili.
Tengeneza juisi yenye lozi 10, kipande cha tangawizi, kikombe kimoja cha
maziwa na kiasi kidogo cha unga wa kungumanga kupata radha. Kunywa
juisi hii kila unapoenda kulala na stress yako itapotea yenyewe.
7. Tufaa
Tunda la tufaa (Apple) lina kingi cha potasiamu, phosphorus, na vitamini
B. Viinilishe hivi ni mhimu kwa ajili ya ubongo wako kujiripea na
kuunda seli mpya jambo ambalo linaweza kusaidia kutuliza akili yako.
Kwenye mlo wako usikose kuwa na tunda hili kila siku.
8. Nyama ya kuku
Upungufu wa vitamini B6 hupelekea msongo wa mawazo kirahisi zaidi.
Mwili wako unahitaji vitamini B6 kwa ajili ya kutengeneza transmita
nyurolojia zinazohusika na kuchangamka kwa akili na mwili wako ambazo ni
‘dopamine’ na ‘serotonin’. Nyama ya kuku inayo kiasi cha kutosha cha
vitamini B6.
Furaha iliyoje kuona kuwa kumbe kula kuku tu kunaweza kukupunguzia au kukuondolea kabisa msongo wa mawazo (stress)?.
Kula nyama ya kuku mara kwa mara. Kwa kawaida asubuhi mi binafsi
napendelea sana kula supu ya kuku. Mhimu zingatia ni kuku wa kienyeji na
siyo hawa wa kizungu ambao wanaweza kukuletea shida zaidi mwilini.
9. Spinach
Kwa mjibu wa utafiti moja ya sababu nyingine ya msongo wa mawazo ni
kupungua ‘folic acid’ mwilini. Ukweli ni kuwa wanasayansi wamegundua
watu wengi wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo wana kiasi kidogo cha
folic acid ukilinganisha na wengine wenye utulivu katika akili zao.
Vile vile homoni mhimu inayojihusisha na udhibiti wa matendo ya akili
ijulikanayo kama ‘serotonin’ kiwango chake hushuka chini sana inapotokea
folic acid imeshuka mwilini jambo ambalo ndilo hupelekea kutokea kwa
msongo wa mawazo au stress moja kwa moja.
Kwa bahati mbaya upungufu huu wa folic acid unawatokea zaidi wanawake kuliko wanaume.
Kikombe kimoja cha spinachi kwa siku kinatosha kukupa folic acid unayohitaji kila siku.
10. Masaji
Masaji ni njia nyingine rahisi ya kuondoa msongo ndani ya mwili wako
isiyo na madhara yoyote. Masaji ambayo inahusisha matumizi ya mafuta ni
njia nzuri sana ya kuweka sawa akili yako na kuondoa sumu mwilini
kirahisi.
Masaji ya mwili itakufanyia ujisikie vizuri kimwili na kiakili pia. Kwa
kazi hii unaweza kutumia mafuta ya nazi ua ya ufuta au ya karafuu kwa
matokeo mazuri zaidi.
Mara moja moja katika wiki pata nafasi ya kupata huduma hii ili kuzuia na kukabiliana na tatizo la msongo wa mawazo (stress).
11. Kahawa
Kahawa inao uwezo pia wa kukufanya ujisikie vizuri na hivyo kuondoa
msongo wa mawazo. Kunywa kikombe kimoja cha kahawa asubuhi ikiwa
unakabiliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili.
Hata hivyo kuwa makini, kunywa kahawa kupita kiasi kunaweza kukupelekea
ukapatwa na mfadhaiko zaidi sababu kahawa ina kaffeina ndani yake ambayo
ni dawa ya kulevya kundi la madawa ya kulevya yanayosisimua akili
(stimulants drugs).
12. Mafuta ya habbat soda
Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda kuwa msaada mkubwa katika
kudhibiti tabia za kuhamaki na wasiwasi na hivyo kukuwezesha kujisikia
vizuri kila mara. Na utaona matokeo haya baada ya matumizi ya habbat
soda kwa siku 30 hivi.
Tafiti kadhaa zimeonyesha watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda
wanakuwa ni watu wenye furaha ya asili na kuwa si wepesi kuwa na huzuni
au kufadhaika.
Kazi hii ya mafuta ya habbat soda ndiyo mhimu kuliko zote sababu
mamilioni ya watu wanakabiliwa na tatizo la kuwa na huzuni au stress na
mifadhaiko ya akili kitendo ambacho kinaweza kuharibu kinga zao za mwili
na maisha kwa ujumla.
Ni vigumu sana kupata mtishamba ambao unaweza kutibu matatizo
yanayohusiana na saikolojia moja kwa moja lakini mafuta ya habbat soda
yanaweza kutumika kwa dhumuni hili la kutuliza, kupunguza na kutibu
tatizo la huzuni au kufadhaika kwa akili.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
13. Chai ya Kijani
Watu wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo mara nyingi wanapungukiwa na
nguvu na ujasiri. Na chai ya kijani inaweza kukurejeshea vyote hivi
viwili yaani nguvu pamoja na ujasiri sababu ina kiinilishe mhimu kwa
ajili kijulikanacho kama ‘L- Theanine’ ambacho hufanya kazi hii ya
kuondoa mfadhaiko wa akili.
Hivyo kupunguza na kuondoa stress hakikisha hukosi kunywa chai hii mara 2 hata 3 kwa siku.
14. Chumvi
Unaweza ukashangaa kuona chumvi nayo imo kwenye orodha hii. Ukweli ni
kuwa watu wengi hawatumii chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyao miaka ya
sasa jambo linalopelekea wengi wao kupatwa na mfadhaiko wa akili na
hata magonjwa kama shinikizo la juu la damu na kisukari.
Huwezi kuwa na afya bora kama hutumii ya kutosha kwenye vyakula vyako
kila siku. Chumvi ni mhimu mwilini kama ilivyo kwa maji ya kunywa.
Chumvi ninayoizungumzia hapa ni ile yam awe ya baharini ambayo haijapita
kiwandani kwakuwa ndiyo huwa madini madogo madogo (trace minerals)
mhimu zaidi kwa afya ya binadamu.
Najuwa umeambiwa chumvi ni mbaya na kuwa unatakiwa ule vyakula vyenye
chumvi kidogo au visivyo na chumvi kabisa, hata hivyo madai haya hayana
ukweli wowote na ndiyo sababu unaona hata kwenye dripu la maji lazima na
chumvi iwekwe ndani yake. Kila lita moja la dripu la maji ndani yake
huwekwa chumvi gramu 9.
Chumvi inaweza kuwa mbaya ikiwa tu wewe si mtu unayependa kunywa maji
mengi kila siku, ila kama unakunywa maji mengi kila siku basi unahitaji
pia chumvi ya kutosha kwenye vyakula unavyokula kila siku.
Kama una msongo wa mawazo na unakula vyakula vyenye chumvi kwa mbali ni
wakati sasa wa kubadili mtindo huo na hutakawia kuona mabadiliko mazuri.
15. LIMAU
Limau ni dawa nyingine ya asili rahisi ya kutibu msongo wa mawazo
unayoweza kuiendea isiyo na madhara yoyote mabaya hapo baadaye kwenye
afya ya mwili wako.
Ndiyo maana kila ukipewa supu asubuhi hawaachi kukuwekea na limau
pembeni, kwakuwa limau huondoa uchovu na kujisikia vibaya kirahisi
zaidi.
Tumia limau mara kwa mara kwenye kachumbali zako au unaweza kuchanganya
vijiko vikubwa viwili vya maji ya limau ndani ya kikombe kimoja cha maji
ya kawaida na unywe kila siku kutwa mara 1.
Usizidishe matumizi ya limau hata hivyo kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea kupungua kwa kiasi cha damu mwilini mwako.
16. KABEJI
Imethibitika pasipo na shaka kuwa kabeji ni chakula bora kabisa ambacho
kinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya aina mbalimbali za kansa,
shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo, maambukizi mbalimbali, na
mhimu kuliko yote ni kuwa kabeji inao uwezo pia wa kuzuia usipatwe na
hamaki na mfadhaiko wa akili.
Kabeji lina vitamini B6, vitamini K na vitamini C. Ukiacha hayo kabeji
pia ni chanzo kizuri cha folate, vitamini B1, potasiamu, copper,
nyuzinyuzi (fiber) na manganizi. Viinilishe hivi ni mhimu sana katika
kuichangamsha afya ya akili na mwili kwa ujumla.
Unaweza kutengeneza supu ya kabeji, juisi ya kabeji, kachumbali yenye
kabeji ndani yake au ule tu mboga ya kabeji kila mara ili kupunguza
stress yako bila gharama wala kutumia dawa yoyote yenye kemikali.
17. MAZOEZI YA VIUNGO
Mazoezi ya viungo ni dawa nyingine inayoweza kukuondoela msongo wa
mawazo kirahisi zaidi bila gharama yoyote wala madhara yoyote katika
afya yako.
Kuna watu mi nawaita kina chauvivu, kina chauvivu utawasikia ‘nakosa
muda wa mazoezi’. Unakosa muda wa mazoezi mbona muda wa kulala hukosi?
Huo ni uvivu tu ndiyo unakusumbuwa.
Hata katika kupungua uzito watu wengi hawapendi kusikia kuhusu mazoezi, wanahitaji dawa hata kupunguza uzito!
Unapopatwa na msongo wa mawazo au mfadhaiko nenda kawe bize na mazoezi
na mazoezi na hutakawia kuona akili yako inarudi kwenye hali ya kawaida
bila kukawia.
Mazoezi huongeza furaha, huongeza kujiamini na hukufanya ujisikie mwenye
utulivu kwa haraka sana. Haijalishi upo bize kiasi gani hakikisha
unatenga muda wa lisaa limoja la mazoezi kila siku ili kujikinga au
kujitibu na msongo wa mawazo.
18. KOROSHO
Unapokuwa unasumbuliwa na mfadhaiko kiasi chako cha madini ya zinki huwa
kinashuka chini kwa kiasi kikubwa sana. Kwahiyo namna nzuri ya
kujitibu tatizo hili ni kutumia vyakula vyenye madini ya kutosa ya
zinki kila siku.
Korosho ni moja ya vyakula vyenye madini ya kutosha ya zinki. Mhimu ni
utambuwe kuwa miili yetu haijaundwa kuwa inahifadhi madini ya zink kila
siku, hivyo unahitaji kuwa unatumia vyakula hivi siku zote kwa matokeo
mazuri zaidi.
Kula kiganja kimoja cha mkono wako cha korosho kila siku na hutakawia kuona akili yako inapata utulivu unaohitajika.
19. MBEGU ZA MABOGA
Msongo wa mawazo au stress kama mlivyozoea wengi ni tatizo linaloendelea
kuwasumbua watu wengi miaka ya sasa. Mbaya zaidi wengi huwa hawaelewi
nini madhara ya msongo wa mawazo kiafya.
Yaani stress au msongo wa mawazo unaweza kukuletea magonjwa mengine
mwilini zaidi ya 50, hivyo utaona ni jinsi gani ilivyo mhimu kwako
kuweka chini stress zako na uendelee na maisha kwani kuendelea kuwa na
stress ni hatari zaidi kwa afya yako.
Moja ya sababu kuu ya watu wengi kuwa na stress ni usawa usio sawa wa homoni zao (hormonal imbalance).
Hivyo kama una tatizo la homoni kwenye mwili hebu weka mazoea ya
kutafuna mbegu za maboga kila siku na hutakawia kuona tofauti. Mbegu za
maboga zina kimeng’enya mhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho
‘tryptophan’ na asidi amino zingine mhimu zinazohusika kutengenezwa kwa
homoni nyingine ijulikanayo kama ‘serotonin’.
Kama ulikuwa hujuwi ni kuwa serotonin ni homoni inayohusika na kazi
mhimu sana ya kurekebisha matendo ya kitabia na kutoa matokeo chanya kwa
mambo yanayohusu usingizi, hali ya mawazo kwa ujumla na mambo
yanayohusu njaa.
Mbegu za maboga ni msaada mkubwa kwa kina mama waliofikia ukomo wa siku
zao na huondoa matatizo ya kiafya yatokanayo na kukoma kwa hedhi. Ni
msaada kwa watu wenye saratani mbalimbali, huimarisha ukuaji na ustawi
wa mifupa na meno, huondoa harufu mbaya ya kinywa na husaidia pia wenye
tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu kila mara.
20. MPANGILIO WA CHAKULA
Chakula unachokula kila siku kinaweza kupelekea mfadhaiko zaidi kama
hutakuwa makini. Hivyo chakula bora kwa ajili ya kukulinda dhidi ya
mfadhaiko lazima kijumuishe vitu vifuatavyo:
- Kula zaidi vyakula vyenye omega 3.
- Vyakula vyenye magnesium kwa wingi.
- Vyakula vyenye vitamini C zaidi.
- Vyakula vyenye vitamini kundi B
- Unywe maji mengi kila siku lita 2 mpaka 3
- Vyakula vyenye tryptophan kwa wingi kama nyama ya kuku, mbegu za maboga, maziwa nk
- Punguza matumizi ya sukari na badala yake hamia kutumia asali
- Acha vilevi vyote
- Usikae mpweke hata mara moja
- Shiriki tendo la ndoa mara kwa mara
No comments