CHOMEZO MALKIA WA JELA SEHEMU YA SITA



SEHEMU YA SITA 
.................................
Usiku mmoja baadh ya maaskar kurejea majumban kwao afande MUGA aliamua kutumia,nafas ile na kuwahonga pesa baadh ya maaskar waliokuwepo zamu usiku huo na kuweza kumchukua msichana LINDA kutoka ndan ya gereza na kuelekea nae katika ofisi yake baada ya kufika tu Afande MUGA alimwomba LINDA aweze kuket kwenye kiti "Leo nina habar njema kwako najua fika zitakwenda kukufuarahisha hata Kama siyo Sana basi hata kiasi tu " aliongea Afande MUGA huku taratibu akionekana waz kumsogelea alipokuwa amekaa LINDA "Mmh Afande ni bora ungeneleza hizo habar mapema hili nijue ntazipokea vipi " aliongea LINDA Afande MUGA alifika na kusimama pemben ya LINDA na kupeleka mkono wake chin kulikuwa na mfuko mweus ambao aliweza kuibuka nao na kuuweka juu ya meza "Afande hiki nin ?" Aliuliza LINDA huku akionekana kuwa na waswas "Ondoa Shaka hii ni kwaajili yako chukua kisha  ufungue "
LINDA kwa woga aliuchukua mfuko ule na kuifungua kisha kutoa kilichomo ndan ilikuwa ni nguo  pamoja na viatu "Mmmmh ! Afande mbona Kama sielew hiv n kwaajil ya nan ? Aliuliza LINDA "Nan mwingine Kama siyo wewe MALKIA "
"Usinitanie Sasa unadhan hiz nguo ntavaa wakat Gan ikiwa tangu niingie humu ndan sale hii nloivaa ndo mavaz yetu ya siku zote au umeanza kuchanganyikiwa Afandee "
"Sikia Kama kuchanganyikiwa tu nimechanganyikiwa haswaa kwaajil yako "
"Mmh! Inaonekana waz acha nikalale zangu " LINDA aliongea vile na kunyanyuka kwenye kiti akitaka kuondoka Afande MUGA alimshika mkono "LINDA Nahitaj tutoke out Leo "
"Eee!!!??? ........ Unasemaa? LINDA hakuamin alichokisikia "Nataka Leo twende tukajirushe mim na wewe "
LINDA alipigwa ganzi kwa muda na kubakia akishangaa tu "Vipi uamin ?" Aliuliza afande "Siamin ....Siamin .. "Huku akijifuta machoz yaliyokwisha anza kumtiririka "Ila tutawezaje kutoka wakat mm n mfungwa tiyar "
"Hilo niachie mm Kama upo tayar twende"
"Navaa au" 
"Hapana utaenda kuvalia ndan ya gari "
Walitoka wakiwa wameongozana huku Afande MUGA akiwa amemfunga pingu msichana LINDA mikono yote miwili ili askar wasiweze kujua kwa urahis ni kipi ambacho kinaendelea wakat huo mkonon mwa Afande MUGA akiwa ameshikilia ule mfuko wenye Nguo walikwenda moja kwa moja mpk kuingia ndan ya gar ya Afande MUGA na kufanikiwa kutoka nje ya eneo la gereza LINDA alikuwa aamin macho yake aligeuka nyuma Mara kwa Mara kuhakikisha Kama kweli yupo nje gereza "LINDA nazid kukusisitiza usihofu ila nataka tu kitu kimoja toka kwako uaminifu usije ukajidanganya kunitoroka hutofika kokote pale " Afande MUGA alianza kumpa LINDA maneno ya vitisho "Siwez kufanya hivo "  Baada ya kufika mbele zaid afande MUGA alimfungua LINDA pingu na kuweza kumpatia zile nguo aweze kuzibadilishia ndan ya gari baada ya hapo Afande MUGA alitoa simu yake na kuonekana kuongea na mtu ,Alikuwa ni mdada ambaye hujishungulisha na kaz ya saloon za kike na Duka la mavazi  Afande alimpitisha akaweza kuoga na kurekebishwa kisha kubadilishiwa mavazi yake Yale aliyovalia ndan ya gar na kuvaa mavaz mengine Alionekana kupendeza kupita kias Afande MUGA alilipia gharama zote na kuweza kuondoka kuelekea club huku Afande MUGA nae akiwa amebadilisha mavaz yake ya kaz na kuvaa kiraia  "Afande Mpk sasa siamin kabisa ninachokiona " aliongea LINDA wakiwa ndan ya club wakinywa juisi "LINDA amin halafu naomba usiniite Afande utaharibu kila kitu Kwa Leo niite Baby "
"Mh! Poa ... Ila nashukuru Sana kwa kitendo hiki cha Leo furaha niliyo nayo sijawah hata siku moja kuipata " 
"Bado huu mwanzo Utafurah zaid ya hapa " wakat wakiendelea kunywa juis zao LINDA aliweza kumwona TABU "Baby Twende tukacheze mziki kidogo " Aliongea Afande MUGA wakat huo LINDA yupo bize akimtazama TABU "LINDA ..LINDA " Aliita Afande Ndipo LINDA akashtuka "Vipi uko sawa ? Afande aliuliza "Hapana Kuna mtu nimemwona aliyepelekea Mimi kuingia Gerezan "
"Utakuwa umemfananisha hebu jaribu kuacha mawazo nimekuleta huku tuinji "
"Baby yeye kabisa sijamfananisha " LINDA alinyanyuka kwenye kiti akitaka kumfuata Afande MUGA alisimama na  kumwahi haraka "LINDA unataka kuniudhi siyo  "
"Afande Siwez kuvumilia "
"Nimekwambia usiniite hilo jina Afande MUGA aliamua kumvuta LINDA na kutoka nae nje ya Club "Unataka kufanya nin LINDA na tumeongea nn kumbe hupend raha umezoea shida Sana "
"Afande naumia we hujui tu ni kias gan "
"Mim naona hatuelewan bora tuondoke utaniharibia tu" afande MUGA aliamua kuondoka na LINDA na kuelekea nae katika eneo la hotel "Huku tumeijia nn sasa ? A link is a LINDA baada ya kuingia katika chumba cha hoteli "We ni mtoto mdogo kwan "
"Naomba nirudishe tu gerezan siwez kufanya unachotaka "
"LINDA sis ni watu wazima siyo lazima ifikie hatua tutumie nguvu kwenye mambo yatakayo tufaidisha wote "
"Mimi sipo tayar "
Afande MUGA alimsukumia LINDA kitandan kisha akatoa pingu na kumfungia LINDA mkono wake kwenye kitanda kisha kutoa nguo zake pamoja na za LINDA na kuweza kumwingilia kimwili bila ridhaa yake Baada ya Siku ile kupita LINDA hakuonekana kuwa na furaha kabisa na kujitenga peke yake huku akiwa amejikunyata na machozi yakimtiririka PENDO alipomwona rafiki yake yupo kwenye hali ile alimfuata na kutaka kujua Ana matatzo yapi "LINDA Una nin ? "
"Sina tatzo "
"Mmhn! Upo kwenye hali hii halafu Una niongope huna tatzo au hupend nijue matatzo yako maana nimekuwa nikikuuliza lakin huwa hutak kuniambia nin kina kusumbua"
"PENDO tatzo nlo nalo hata nikikuambia hutonisaidia "
"Kama Una umwa ni bora useme tu utibiwe kumbuka mficha maradh "
"Mmh! PENDO naomba iwe siri yako usimwambie mtu nakuamin rafiki yangu "
"Usijali " aliongea PENDO huku akipeleka mkono wake na kumfuta LINDA machozi "PENDO Afande MUGA amenibaka "
"Nin !?.... LINDA ilikuaje ?
"PENDO Afande MUGA Ana nihitaj kimapenz Jana alinitoa nje ya gereza na kunipeleka Club "
"Anhaa Sasa napata picha ndo maana ulikawia kurud baada ya afande kukuchukua ule usiku Unataka kuniambia alipokupeleka Club mlikunywa pombe "
"Hapana tuliagiza juis baada ya hapo tukaondoka sikuwa najua ananipeleka wap nilistukia tu tunaingia hotel na kuanza kunilazimisha nifanye nae mapenz nilipojarbu kukataa alitoa pingu na kunifunga kisha kunibaka " aliongea LINDA kwa uchungu huku machoz yakiendelea kumtoka "Mmh! Pole rafiki yangu kumbe afande MUGA Ana tabia mbaya kias hiki "
"Sikutegemea Kama angenifanyie vile "
"Pole Sana Ila usikae hiv changamka "
Baada ya siku kadhaa kupita AMANDA aliamua kwenda tena nyumban kwa TABU alipofika hakutaka kupisha hodi aliingia moja kwa moja seburen na kumkuta TABU akiwa na mchumba wake "He..he..heeeen! We Unawazimu ! TABU aliongea na kunyanyuka alipokuwa amekaa kwenye kochi na mchumba wake "Wazimu wangu ndo nimekuja kukuonesha Leo " aliongea AMANDA huku akifungua mkoba wake na kutoa kisu kisha Mkoba wake kuutupia kwa nyuma huku akisohea taratbu  Mchumba wa TABU alipoona vile alinyanyuka na kumshika mchumba wake ili asiweze kumsogelea Amanda "Dada unajitakia mabaya huon kuwa ni kosa kuingia nyumban mwa watu kufanya fujo " aliongea mchumba wake TABU "Amanda unadhan naogopa hicho kisu chako sikuogopi Kama nilikula pesa yako hapo sawa sikula hata kumi yako " 
"Na utaungana na aliko enda BEN " aliongea Amanda huku akikiweka sawa kisu "LINDA ndo alomwuua mumewe Mimi kosa langu ni nin hapo "
"Kwan Baby kuna kitu Gan kinaendelea Kati yenu " Aliuliza mchumba wake TABU "Baby alinipa kazi nimsaidie hili anilipe pesa lakin  nanilipoona sijafanikiwa sikwenda kumdai hata Mia sasa nashangaa anavyo nifuatili "
"Dada naomba utoke kwa usalama tu kabla hayajakukuta makubwa

No comments