JINSI YA KUJIKINGA DHIDI YA FANGASI WA UKENI



Fangasi wa ukeni ni miongoni mwa magonjwa ambayo hutesa wanawake kwa namna mbalimbali. Husababisha muwasho, harufu mbaya, maumivu, majimaji, homa nk kiasi cha kuingilia ratiba na ufanyaji kazi wa kila siku wa mtu. Huweza kuwakumba wanawake wa aina zote, ila wanawake wenye ujauzito huwa kwenye hatari zaidi. Ukikosa matibabu mazuri unaweza ukahangaika nao kwa muda mrefu sana, lakini ukipata matibabu mazuri basi ndani ya muda mfupi tu unapona kabisa na kuweza kuwa vizuri.
Kinga ni bora kuliko tiba, ukijua jinsi ya kujikinga usipate ugonjwa huu au usipate tena basi ni vyema zaidi. Leo tuangalie namna mbalimbali ambazo unaweza kutumia ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huu.
Unaweza kujikinga dhidi ya fangasi hawa kwa :
1. Epuka kufanya mapenzi bila kutumia kinga
2. Hakikisha usafi na ukavu mara zote wa sehemu zote za
siri
3. Epuka matumizi ya sabuni kali kujisafishia ukeni
4. Hakikisha unavaa nguo kavu na kuwahi kubadilisha nguo
za ndani mara tu itakapotokea zimelowa
5. Zingatia sana usafi wa nguo za ndani na pedi
MATIBABU YAKE
Matibabu ya fangasi huweza kufanywa kwa dawa mbalimbali kama vile Fluconazole, Clotrimazole, Miconazole nk (NB: Pata ushauri wa daktari na uandikiwe kisha ndipo ununue na kutumia dawa hizi). Kwa kuhakikisha unapata matibabu mazuri zaidi ni vyema kupata ushauri wa daktari (Sio gharama siku hizi, hata Tsh 5,000/= haifiki) ili aielewe kesi yako vizuri zaidi kisha ajue matibabu na dawa nzuri zaidi kwa ajili yako. Ukizingatia hayo matibabu ya fangasi hawa ni rahisi sana na utapona kabisa.
Usiteseke tena, pata ushauri na matibabu sahihi na jikinge vyema dhidi ya fangasi hawa sasa.

No comments