MAGONJWA YA ZINAA KWA MAMA MJAMZITO:DALILI ZAKE,MADHARA NA TIBA YAKE MAGONJWA YA ZINAA KWA MAMA MJAMZITO:DALILI ZAKE,MADHARA NA TIBA YAKE



Magonjwa ya zinaa ni magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiyana (sexually transmitted diseases),inayosababishwa na bakteria,virus au fungus wanaopenda ishi sehemu ya maji maji au unyevu unyevu katika mwili ,kama mdomoni,kooni,sehemu za siri au sehemu ya hajakubwa.

Iwapo mtu atakutana kimwili na mtu mwenye maambukizi hapo ni rahisi kuambukizwa. Magonjwa ya zinaa yanampata mwanamke na mwanaume pia kwa njia ya mdomo,uuke au uume.

Magonjwa ya zinaa yapo ya aina tofauti kuna

  • Kaswende

  • Kisonono

  • Gonorea

  • Ukimwi

  • Klamidia

  • Malenge lenge sehemu za siri

  • Dutu za sehemu ya siri


Magonjwa ya zinaa ni hatari kwa afya ,mama mjamzito akipata ugonjwa wa zinaa atapata dalili tofauti tofauti kama zifuatazo

  • Kuvimba sehemu za siri

  • Maumivu makali pindi ufanyapo mapenzi au wakati wa kukojoa

  • Kupata homa

  • Kutokwa vijipele ukeni vinaweza kuuma au visiume

  • Kupungua uzito

  • Maumivu ya mgongo

  • Kutokwa majasho kwa wingi nyakati za usiku

  • Kutokwa maji maji ukeni yenye harufu au isio na harufu

  • Kutokwa damu au usaha ukeni

  • Kuwashwa sana

  • Uke kubadili rangi



Madhara ya magonjwa ya zinaa kwa mama na mtoto


  • Mtoto anaweza kupata upofu

  • Uziwi-kushindwa mtoto kusikia

  • Mwanamke au mwanamme anaweza kuja kushindwa kuzaa sababu ugonjwa utaenda kuadhiri sehemu za uzazi

  • Kuziba mirija ya uzazi

  • Kifo

  • Ulemavu kwa mtoto

  • Mtu kupoteza kinga ya mwili kuwa dhoofu,kuumwa mara kwa mara.


Tiba


Magonjwa ya zinaa yanatibika iwapo  yatatibiwa mapema isipo kuwa ukimwi peke yake hauna tiba,mambukizi mengine mama mjamzito atatibiwa kwa kupewa antibiotic, mtoto  iwapo ataadhirika kipindi mama yake anamimba  baada ya kuzaliwa atawekwa dawa machoni ya kusafisha na kutibu.



Iwapo mama amegundulika anamaambukizi na muda wa kijifungua umekaribia itabidi azalishwe kwa c-section ( operation)ili kumwepusha mtoto kupata maambukizi.


U.T.I / fungus ni magongwa ya infection nayo yanaweza mpata mama ila yenyewe hupati kwa njia ya kujamiiana haya yanatokana na virus na bakteria pia ambao unaweza watoa vyoo vya public au nyumbani iwapo mkiwa hamsafishi vyoo vizuri na kutumia maji safi ya kujitawazia.



Hivyo ni vizuri mama mjamzito ukahisi muwasho kwa siku 2-3,maji maji kutoka ukeni usiyo yaelewa ,kutokwa kijipele wahi hospital wakutibu kwani nayo ni hatari kwa afya yako na mtoto inaweza sababisha miscarriage ,tiba utapewa dawa kama ya kupaka ,sindano au kunywa kati ya hizo.


Baada ya kutumia dawa ya infections,mtu anaweza tumia njia kwa kutoa sumu ya ugonjwa zaidi kwa kutumia vitu asilia  kwa kula

  1. Kitunguu thomu punje 2 mara 3 kwa siku

  1. Kula parachichi

  2. Kunywa yoghurt glass 2 kwa siku


Ushauri


Mama unatakiwa kuwa mkweli na muwazi kwa mpenzio  ili msilete ugonjwa wa zinaa na maambukizi yatakayo kuja waadhiri nyie na mtoto,iwapo mmoja wenu sio mwaminifu mtumie condom.

No comments