Njia 5 za kitaalam za kudhibiti nyumba ndogo!





Kati ya matatizo makubwa zaidi yanayosumbua uhusiano wa wapenzi wengi ni pamoja na usaliti; Mara zote usaliti huzaa nyumba ndogo! Huu ni ugonjwa hatari unaotafuna uhusiano wa wanandoa wengi duniani. wengi wamelia mpaka machozi yamekauka, sababu ya usaliti.Hata hivyo, wapo wanaolia bila kutafakari namna ya kukabiliana na tatizo hilo, hapa naweza kusema kwamba, unakuwa na tatizo juu ya tatizo lingine. Mwanasaikolojia mmojanchini, aliwahi kusema; “Kufahamu tatizo ni vizuri zaidi kuliko kuwa na tatizo ambalo hulijui. Unapojua tatizo lilipo, inakuwa rahisi kwako kutafuta njia za utatuzi. Kwahiyo matatizo yaje,lakini yajulikane.”Kila watu 10 ninaozungumza nao juu ya ushauri wa ndoa na uhusiano, 8 kati yao huzungumzia juu ya kusalitiwa na wapenzi/wanandoa wao. Ni kesi zisizoisha kwa Wataalamu wa Saikolojia ya Uhusiano, hata mimi nakutana nazo sana. Kila siku napokea simu nyingi sana zenye aina hiyo ya matatizo, kwenye sms ndiyo zaidi, ukiachilia mbali waraka pepe.“Ninafurahi sana kusoma makala zakokaka Shaluwa, zinanipa mwanga kila siku, lakini nina tatizo ambalo nataka unisaidie…mume wangu amebadilika sana, amekuwa na tabia ambazo mwanzoni hakuwa nazo kabisa. Simu yake anaificha sana, lakini mbaya zaidi nimefuma sms anazotumiwa na wanawake wake wa nje.“Nampa kila kitu, nampikia vizuri, namsaidia kimawazo, lakini sijui anatafuta nini huko nje? Ndoa yetu inamiaka 12 sasa, tumejaliwa watoto wawili, mmoja wa kike na mwingine wa kike. Nimechoka na mambo yake kiasi kwamba nataka kuondoka hapa nyumbani kwake.“Kudai talaka nashindwa, maana ndoayetu ni ya kanisani, nimezungumza naye sana, lakini haelewi, nashindwa la kufanya kaka Shaluwa. Naomba msaada wako wa mawazo ili niweze kuutua huu mzigo, maana unanichanganya sana kichwa changu…” hii ni sehemu ya ujumbe uliotumwa kwa njia ya waraka pepe namsomaji mmoja kutoka Mbeya ambaye hapa sitataja jina lake.Unaweza kuona jinsi tatizo hili lilivyo sugu katika ndoa nyingi. Huyu nilimalizana naye kwenye waraka pepe na habari za kufurahisha ni kwamba, ndoa yake inaendelea vizuri na taratibu mumewe ameanza kubadilika baada ya yeye kuanza ‘dozi’ niliyompa. Bila shaka ndoa yakeitapona kabisa!Katika mada zangu zilizopita, niliwahi kuandika kuhusu sababu za wanaumekusaliti ndoa. Katika mada hii, nimeenda mbele zaidi, nachambua njia za kukomesha nyumba ndogo, kwa maana ya pande zote mbili; Wanaume na wanawake!Sasa hebu tuone jinsi ya kukomesha nyumba ndogo.ANZIA KWAKOIli uweze kutibu tatizo hili na kama ni kweli hutaki mumeo/mkeo au mpenzio awe na nyumba ndogo, basi anza kwako kwanza! Jiangalie wewe ukoje? Unatoka nje au hutoki? Maana kama hutaki kusalitiwa na wewe unasaliti ni kichekesho.Kama una kamchezo hako acha mara moja, lakini kama una hisia za kufanyahivyo au yupo mtu anayekusumbua, acha mara moja. Ukiacha utakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuumia na kutafuta njia za kukomesha nyumba ndogo kwa nguvu zaidi.KUMBUSHA YA ZAMANIMathalani una mashaka kwamba mwenzi wako anakusaliti au unaanza kumhisi vibaya kutokana na namna alivyo makini zaidi na simu yake kipindi hiki. Lakini inawezekana kabisa, umeshafuma meseji zisizostahili kwenye simu ya mpenzi wako au umepata fununu kwamba anakusaliti. Kubwa zaidi, inawezekanauna ushahidi kabisa kwamba anakusaliti. Anatoka na mtu mwingine.Usipaniki maana haitakusaidia, lazimausogee hatua moja mbele. Huyo ni wako, tayari mpo kwenye ndoa, kuachana haiwezekani na hata kama inawezekana si suluhisho la mwisho, kwani yawezekana ukakutana na mwingine mwenye kasoro zaidi ya huyo.Kitu cha kwanza kabisa kufanya ili kukomesha usaliti katika ndoa/penzi lenu ni kukumbusha yale ya zamani! Unajua kuna umri fulani wanandoa wakifikisha, wanajisahau. Wanakuwa hawana jipya; Na si kwamba hawana jipya, bali hawataki kuonesha mambo mapya.Nasema wanaweza kufanya mapya kwa sababu mwandoa huyo huyo anayetoka nje kwa kukosa mapya kutoka kwa mpenzi wake, akienda nje,anakuwa mtundu balaa! Yapo, yanaonekana na watu wanawajua. Mume ana nyumba ndogo na mke naye ana nyumba ndogo. Ngoma droo! Haina maana kabisa.Hata kama mwenzi wako hajaanza katabia haka kachafu, lakini ni vizuri basi ukapambana ili kukomesha au kuzuia isitokee. Njia nyepesi na ya pili kukumbusha mambo uliyokuwa ukimfanyia zamani.Wengi hujisahau baada ya kuingia kwenye ndoa, hili ni tatizo. Hakikisha unakuwa mtundu faragha, unamtumiameseji kila wakati, unampokea mumeo anapotoka kazini. Unatoka na mwenzi wako ‘out’ kila wakati, hizi ni njia za kumfanya mpenzi wako akumbuke mambo ya zamani na kamwe asikukinai.1.Outing:Kitu kidogo tu, lakini kinazidisha mapenzi sana. Hebu vuta picha, kipindi cha mwanzo wa mapenzi yenu, wewe umependeza na mwenzi wako naye pia, mnatoka pamoja na kwenda kuangalia bendi mnayoipenda, ufukweni au kwenye hoteli ya kifahari…mapenzi yanasonga jamani! Huwezi kukaa na mkeo kila siku kwenye kochi lile lile, unamtazama kwa mtazamo uleule, halafu ukienda Twanga unakutana na mademu wakali, wenye miguu na matiti ya kuvutia, unadata na kusema mkeo hana mvuto. Nani kasema?! Hebu mchukue, mpige pamba halafu nenda Akudo, kama hamtagombana na wanawake wanaomkodolea macho.2.Surprise:Si lazima iwe ya fedha kubwa, kitu chochote kinaweza kuwa surprise. Acha kujidanganya, hebu nunua hatamaua ya elfu moja, pulizia manukato safi, halafu mpe ukimwambia; “Nakupenda baby.” Unataka surprise gani zaidi ya hiyo? Kila anapokuwa anaona zawadi yako, anajihisi mgumu kumkubalia Pedeshee nanilii anayemsumbua kila anapokwenda buchani. Akili kichwani mwako mtu mzima!3.Badili mazingira:Achana na ulimbukeni wa kila siku kukutana na mkeo sehemu moja, mbona zamani mlikuwa mnatoka na kulala nje ya mji auhotelini? Kuna mkono unapofikia, hata ukimchukua mwenzi wako na kwenda naye Pole Kwa Kazi Guest House ya elfu kumi bado utakuwa umebadilisha mazingira na utaonekana mpya. Kumbuka kinachotafutwa hapa ni upya wa ndoa na mapenzi na kumfanya mwenzi wako asiwe na wazo la kusaka nyumba ndogo. Umeona rafiki zangu? Sasa hebu tuangalie kipengele kingine muhimu zaidi.TAFUTA MSISIMKO ZAIDIIli penzi liendelee kuwa imara lazima utafute msisimko zaidi, yapo mengi ambayo yanaweza kuongeza msisimko katika penzi lako. Haiwezekani rafiki yangu, uwe unarudinyumbani saa tano usiku kila siku, unadhani utamwona mkeo ana tofauti.Hapa ni kujidhibiti mwenyewe, maana usipokuwa makini, unaweza kushangaa unamdharau mkeo na kumuona hana mvuto kabisa. Huo mvuto utaona wapi kama kila ukija unamkuta amevaa kanga moja anataka kulala? Utamuona wa kawaida na mwishoni utaamua kutafuta kitulizo nje, ambapo mapenzindani yatapungua na si ajabu na yeye akaamua kusaka mahali pa kupumzisha moyo wake.Richard Manyota katika kitabu chake cha Saikolojia na Maisha II anasema ili uzidi kumuona mpenzi wako mpya kila siku, lazima umfanye rafiki yako nambari wani. Anasema: “Mke/mume lazima awe rafiki yako wa kwanza, unadhani utamuonaje muhimu kwako,kama hampati muda wa kuwa pamoja mkazungumza kirafiki?“Tunashauri, wanandoa wawe na muda wa mzaha, kutoka pamoja, kujadiliana mambo mbalimbali kirafiki,ili kujenga ustawi bora zaidi wa ndoa yao,” inaeleza sehemu ya kitabu hicho.Akaendelea: “Huwezi kuwa na mkeo, kila siku yupo kwenye muonekano uleule, akakuvutia. Lazima leo, awe na mavazi tofauti, umshike mkono na kwenda naye beach, kesho mmekwenda pamoja Kariakoo kununua mahitaji. Utampenda daima.”Mwanasaikolojia mwingine wa Tanzania, Oscar Ndauka katika kitabu chake cha Uzinzi na Uasherati, anaeleza kwamba mke kukaa ndani kihasara-hasara ni kati ya mambo yanayoua mvuto na ushawishi wa kimapenzi, ambao baadaye huzaa nyumba ndogo.Anasema: “Utakuta mwanamke, akiwachumbani na mumewe anakaa hovyo hovyo, sehemu ya maungo yake yako wazi, sasa nini kitamvutia mumeo kama kila siku anakuona katika hali hiyo? Hapa lazima wanawake nao wawe macho jamani, vinginevyo hizi nyumba ndogo hazitaisha.”FANYA MAMBO MUHIMUWakati ukiwaza jinsi ya kumfanya mumeo/mkeo asitoke nje ya ndoa, lazima pia uwe mtu wa kufanya mambo muhimu. Unapofanya mambomuhimu katika ndoa yako, kunampa sababu mwenzi wako ya kutunza heshima ya ndoa hiyo.Nasema heshima kutokana na ukubwa au ubora wa umuhimu wa jambo utakalokuwa umelifanya kwa ajili ya ndoa yako. Hapa kuna vijisehemu vinne vinavyofafanua zaidi.Tengeneza bajetiKama wewe ni mwanamke, kati ya mambo ambayo yatamfanya mumeo akupe nafasi ya kwanza na kujikuta akishindwa kuisaliti ndoa yake ni wewe kutengeneza bajeti nzuri. Kama mama, wewe ndiyo msaidizi wa familia.Usaidizi hauishii katika kufua, kupika na kufanya usafi wa ndani pekee. Tengeneza bajeti ndogo ya chakula na mambo ya maendeleo kisha mpatie mumeo na umfafanulie zaidi. Zungumzia kuhusu maendeleo na malengo yako kwake kwa ajili ya maisha yenu ya baadaye kama wanandoa.Mpe sababu ya kujisogeza kwakoKutoka nje ya ndoa, kunazalishwa na kutoridhishwa na mahaba ya nyumbani. Inawezekana kabisa, humfanyii mambo uliyokuwa unamfanyia zamani. Mathalani, ulikuwa ukimtumia sms kila mchana ukimkumbusha kula, ulikuwa ukimtakia kazi njema n.k.Wakati wewe ukiacha kufanya hivyo, kazini kwao yupo mwanamke anayemzimia na kazi yake kubwa ni kutunga mashairi ya mahaba na kumtumia mumeo; Atatoka kweli? Kuwa naye karibu, tawala siku yake, mpe sababu ya kuwa na wewe. Mfanye aone umuhimu wa kukuwahi nyumbani mara baada ya kumaliza kazi.Mpongeze anapokosea!Inaweza kukushangaza kidogo, lakini huwezi kuamini kabisa kwamba mwenzi wako anapokosea hutegemeazaidi lawama, matusi na maneno ambayo hayatamfurahisha. Kuwa tofauti, akichelewa kurejea nyumbani, mfungulie mlango, mkumbatie, mbusu na mpe pole kwa kazi.“Hongera mume wangu, wewe ni mchakakazi na unajali familia yako, najua ulikuwa unahangaika, karibu nyumbani baba. Utakula au utaoga kwanza?” Unaona maneno hayo?Mwambie hata kama ananuka pombe!Hapo utakuwa umempa somo tofauti na kumwambia: “Najua umetoka kwa wanawake zako…hili lijanaume sijui nimetoka nalo wapi mimi?” Usilogwe dada yangu, kesho atarudi kule kule, ikiwezekana atalala huko huko kabisa.Linda ndoa yakoSitafafanua sana kijisehemu hiki, lakini kikubwa nilichokusudia ni kwamba, kuwa bora kitandani! Jifunzekila siku kuwa mkali kwenye sayari ya wapendanao. Ukiweza kumkamata vizuri eneo hili, aende nje kufanya nini?Utaalamu faragha si uhuni, kuwa bora,panua mawazo, peruzi mitandaoni, soma majarida lakini pia tafiti mwenyewe. Ukiweza, kila wiki gundua sehemu moja mpya inayompa msisimko zaidi mwenzi wako.ZUNGUMZIA MUSTAKABALI WA FAMILIA YENU Unaweza kumfanya mwenzi wako asikusaliti wala asifikirie kuwa na nyumba ndogo, ikiwa utapata wasaa wa kuzungumza naye mustakabali wandoa yenu. Katika hili, yapo maeneo muhimu zaidi ambayo ukiyakazia, ndoa yako itaendelea kuwa imara. Hebu tuone.Hofu ya MunguJenga mazingira ya mwenzi wako kuogopa Ukuu wa Mungu. Jambo hili linawezekana ikiwa utamsisitiza au kumrejesha katika Mamlaka ya Mungu kiimani. Mweleze kuwa, kwenda kinyume na matakwa yake ni rahisi ndoa kubaki bila uangalizi, mwishowe shetani kuingiza mafarakano.Mhimize kufanya Ibada, tengeni mudawa kusali/kuswali/kuomba dua pamoja kabla ya kulala na kuamka. Mweleze mustakabali wa ndoa yenu uko mikononi mwake, utakuwa umemjenga sana.Magonjwa!Mustakabali wa ndoa yenu, hauwezi kuwa mzuri kama magonjwa hatari yakiingia. Ukimwi ni tishio, tenga muda wa kuzungumza naye ‘seriously’ kuhusu hili; Si kama utakuwa unamtisha, lakini utakuwa unampa ukweli ambao unaonekana.Watoto wenuMatokeo ya familia isiyo na masikilizano ni mwanzo wa mwisho mbaya wa watoto wenu, lakini pia zungumza naye sana juu ya mipango mbalimbali ya wanenu. Onesha unawapenda na wanahitaji sana msaada wenu kama wazazi. Kuzungumzia kwako watoto, kutampanguvu kwamba yupo na mwenzi sahihi anayetumia muda wake kufikiria familia yake.TamaaTamaa ni kati ya mambo yanayosababisha usaliti unaozaa nyumba ndogo baadaye. Msisitize juuya tamaa na umtake awe na uvumilivuna mambo msiyo na uwezo nayo. Huuni ushauri, lakini ukiutoa kwa kumaanisha, unaweza kujenga kitu fulani kichwani mwake.Kusaliti bila kukusudia!Wapo rafiki zangu ambao wanaweza kunishangaa kwa kusema kuna usalitiwa bila kukusudia. Yes, upo. Kama ilivyo kuua bila kukusudua, pia kuna usaliti bila kukusudia. Usaliti huu hufanyika kutokana na muhusika kujenga/kujengewa mazingira ya kufanya hivyo.Epuka kuwa karibu na mtu ambaye mna jinsia tofauti. Usiruhusu mazoea sana hasa ya ku-chart au kuwa naye sehemu tatanishi. Jiheshimu na uwe mtu wa mipaka. Anayetakiwa kukuzoea sana ni mke/mume wako tu. Naweka nukta.

No comments