DEAR LADIES
1. Ngono haimfanyi mwanaume asikuache, hata ukukuruke vipi, jikwatue kiasi gani kama hajaona quality za kuwa mke atakuacha tu.
2. Mwanaume anaekupata kwa vile alitumia pesa zake kwako hatakaa na wewe milele. Wanaume halisi hawawezi wakatoka na wanawake feki wanaopenda pesa. Ukibahatika sana atakufanya daraja la pili yaani mchepuko!
3. Uzuri wa mwanamke unaweza ukampelekea akaolewa ila tabia yake ndio itakayoamua ni kwa muda gani atadumu katika ndoa. Uzuri huvutia wanaume, ila tabia hufanya wanaume wadumu na wewe.
4. Pesa kiukweli ina faida sana na ni muhimu kwa mtu yoyote kuwa nayo ila pesa peke yake haiwezi kuleta ukweli wa maana halisi ya furaha na maisha.
6. Kuwa mzuri bila tabia njema hakuwezi kukakupa mume bora, sana sana utapata Boyfriends na wanaume za watu.
6. Tendo la ngono linaleta faraja ila haliwezi kuleta upendo. Sex ni zao la mapenzi, mapenzi sio zao la sex.
7. Sex inaweza kufanya mwanaume alale na wewe usiku kucha, na asubuhi akaondoka zake ila upendo hufanya mwanaume aishi na wewe daima.
8. Kuna mambo mengine pesa haiwezi nunua kama tabia na heshima, kama ulikubali kuolewa nae kisa pesa zake. Usidhani kupitia pesa zake ataweza badilika.
9. Uvaaji wako siku zote ndio utakaoamua ni nini wanaume wazungumze na wewe!
Ni ukweli fulani hivi ambao ni mchungu! ila sio mbaya waweza shushia na juice bariiiiiii
No comments