Vyakula Vinavyoongeza Hamu na Nguvu ya Kufanya Tendo la Ndoa





Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi

 kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. 

Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 

kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea 

zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 

wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume.

Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia 

upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa 

msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa,

 uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa

 vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu 

zinazochangia kwa kasi tatizo hili

.
Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano 

wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula

ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya

 kufanya tendo la ndoa.  Vyakula hivyo ni hivi

 vifuatavyo:


PILIPILI

Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo huleta mgusu wa hisia za raha wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kuamshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa tendo la ndoa na pia ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa unapata hisia kila sehemu ya mwili.

MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI 

Ulaji wa matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol).  Kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.
Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na pia mwanaume anakuwa na hisia za mapenzi (libido) kidogo.
Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua. Kitalaam inashauriwa kula milo (potions) 3-5 za matunda kwa siku.
NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
Nafaka hasa zisizokobolewa kama mahindi, ngano, uwele, nk zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu. Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.
Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya nejama na mahusiano mazuri ya ndoa yako.

TANGAWIZI

Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama unga na kutumiwa kama chai.

ASALI

Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.
Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.

KARANGA

Karanga huhusika katika kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu (vascular system). Mzunguko wa damu ulio sawasawa katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa murua. Pia karanga zina madini muhimu kama vilemagnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume.

CHAZA (OYSTERS) NA PWEZA

Hawa ni aina ya samaki ambao hupatikana katika maji chumvi. Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni yatestosterone kwa wanaume.
Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume.  Pia madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa kwa wanaume.

SOYA

Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha mafuta (fat) na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zinaphytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya ziada.
Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimuliwa wakati wa tendo la ndoa.
CHOKOLETI
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni (orgasm). Inasaidia sana kula chocolate masaa machache kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa.
PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana. 

No comments