Mke Wangu Ana Mimba; Katokea Kunichukia na Kampenda Mume wa Mtu Jirani na Chumba Tulichopanga
Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana
Husika na kichwa cha habari hapo juu
Mimi kijana mwenzenu nasikitika sana na hii tabia ya mke wangu, kwakweli ana nichanganya sana jaman
Ana mimba ya miez sita lakin katokea kunichukia sana jaman hatak hata kunisogelea wala kula chakula mezan pamoja na mimi
Lakin katokea kumpenda mme wa mtu ambaye ni jiran wa chumba hapa tulipopanga
Mke wangu ni mama wa nyumban na hana kaz lakin mimi huondoka asubuh sana kwenda job lakin hurud usiku wa saa tatu
Nikifika nyumban get had nije nifunguliwe na mtu mwingine mke wangu yeye kalala tu na hata kama nikifika mlangon huwa hafungui upes yaan nitagonga mlango had bas na atakuja kufungua mda atakao taka yeye
Mfano jana nimefika nyumban saa tatu lakin alikuja kunifungulia saa tano usiku
Na kama nikiingia ndan anaanza kutema tema mate et kuna kitu ndan kinanuka shombo ya samak hasa mimi nikiingia
Yaan nakuwa naambiwa mda mwingine yule jamaa huwa anaingia had ndan mwangu kupiga story na mke wangu
Ina niuma sana mimi jaman
Nateseka sana jaman
Naomben usaur wenu
London baby/JF

No comments