FAHAMU CHANZO NA MATIBABU YA KUISHIWA NYWELE KICHWANI AU KIPARA[ALOPECIA]


kuna vijana wengi ambao hawana hata miaka 40 lakini tayari wana vipara kwenye vichwa vyao na nywele hazioti tena. ni hali ambayo inakosesha raha kidogo na wengi wao huamua kunyoa nywele zote ili kipara ionekane ndio staili yake. wengine huvaa kufia, kuvaa wigi au kuficha na kifaa chochote cha urembo. tatizo hili husababishwa na vyanzo vikuu viinne.
mabadiliko ya homoni ndani ya mwili; binadamu ana homoni nyingi sana ndani ya mwili wake...kuna kiwango maalumu cha homoni ambacho kila binadamu anatakiwa awe nacho.kiwango cha homoni fulani kikizidi au kikipungua huleta shida katika mwili wa binadamu.
magonjwa fulani; kuna baadhi ya magonjwa ya ngozi kama fangasi, mabayo yakishambulia eneo la kichwa huweza kuleta kipara mara moja.
matumizi ya aina fulani ya dawa; dawa hasa zile zinazotumika kutibu kansa, yaani vidonge na mionzi hua na madhara ya kumaliza nywele za mwili mzima.
vipara vya urithi; kuna baadhi ya koo ambazo hupata vipara mapema sana katika ukuaji, hivyo ukiona ndugu zako wengi wana vipara katika umri mdogo basi achana nacho kwani hautafanikiwa kupona ila kama ni wewe peke yako ukoo mzima basi pambana mpaka upone.

vipimo vya kufanya ukienda hospitali;
vipimo vya damu; dokta atakupima damu kuangalia magonjwa ambayo yanaweza kusababisha nywele kuisha hasa upungufu wa homoni na magonjwa ya ngozi.
vipimo vingine; kuna vipimo vingine huweza kupimwa kuangalia kama nywele zenyewe ziko vizuri kiafya kwa kutumia darubini ya hospitali lakini bahati mbaya vingi havifanyiki hapa nchini kwetu.

matibabu;
siku zote matibabu hutegemea chanzo cha ugonjwa husika.. kama ni fangasi mgonjwa atapewa dawa husika, kama ni ugonjwa wa ngozi atapata dawa husika, kama ni sababu ya mionzi au dawa za kansa itabidi avumilie tu kwani hawezi kuacha matibabu ya kansa.

dawa za kutumia; kuna dawa kuu mbili ambazo hutumika kutibu tatizo hili yaani finasteride na minoxidil, bahati mbaya dawa hizi nchini kwetu hazipo kabisa.

upasuaji; kuna aina za upasuaji hufanyika kupandikiza nywele, ni ghrama sana na hazipatikani kwenye nchi maskini kama zetu.mcheza mpira maarufu duniani kwa jina la wayne rooney alifanyiwa upasuaji huu.

tiba mbadala;
kama chanzo hakionekani inaweza kua ni tatizo la homoni na lishe mbovu, mtu huyu hutibiwa kwa kupewa virutubisho vya kunywa na kupaka kwenye nywele ili kushtua homoni za ukuaji na kushtua mizizi ya nywele kitaalamu kama hair follicles.
virutubisho hivyo huweza kuleta maibu ndani ya miezi mitano mpaka mwaka mmoja kama picha inavyonyesha hapo chini.
                                                         



jinsi ya kuzuia hali hii;
kula chakula bora chenye virutubisho vyote.
usisuke nywele kwa kuzibana sana na misuko
chana nywele taratibu na usitumie nguvu sana.

No comments