HAYA NDIO MAGONJWA 4 YA KUAMBUKIZWA,, MUHIMU KUPIMA KABLA YA KUANZISHA MAHUSIANO MAPYA.
mara nyingi wapenzi wapya hua wanatumia kondomu mara kwa mara kwa uaminifu lakini wanapokua kwenye mahusiano kwa muda mrefu hujikuta wanaacha kutumia condom na kuisahau kabisa. kumbuka hapa ndipo watu wengi wanaambukizwa magonjwa ya ajabu hasa kama hawakupima mwanzo wa mahusiano lakini sio hivyo tu maambukizi huendelea kama mmoja wao sio mwaminifu ndio maana utafiti unaonyesha wanandoa wanaongoza kwa ugonjwa wa virusi vya ukimwi kwani baada ya ndoa kondomu hua ni mwiko kwao.sasa leo naenda kuongelea magonjwa hatari sana ambayo ni vizuri kupima baada ya kuanzisha mahusiano mapya ila hata siku ikitokea kinga imesahaulika basi huenda uko salama kama mpenzi wako ni mwaminifu.
ugonjwa wa kaswende; kitaalamu kama syphilis, huu ni ugonjwa hatari sana ambao umeharibu maisha ya watu wengi bila wao kujifahamu.ugonjwa huu amabao huambukizwa kwa njia ya ngono huanza kidogo na kidonda ambacho hakiumi sehemu ambapo wadudu wamepita mfano mdomoni au sehemu za siri. kidonda hicho hupona, ,upele usiowasha hutokea na baadae vyote hivyo hupotea. ugonjwa huu baadae huingia ndani ya mwili na kuuanza kuharibu viungo vya ndani. mwisho kabisa ugonjwa huu huahamia kwenye ubongo na kumfanya mtu kua kichaa.kuna vichaa wengi sana mtaani sababu ya huu ugonjwa.
ugonjwa wa hepatitis b; ugonjwa huu ni hatari na unaua haraka kuliko ukimwi, virusi vya ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya ngono na kugusana kwa dmu au majimaji ya mwili kama ukimwi lakini ni rahisi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu kuliko kupata ukimwi. ugonjwa huu hushambulia maini na kuacha makovu. mgonjwa hupata macho ya njano, homa, maumivu ya kichwa na kadhalika.ugonjwa hii mwishoni hupelekea kansa ya ini ambayo inaua ndani ya miezi sita.
ugonjwa wa ukimwi; huu ni ugonjwa unaofahamika kwani unatangazwa sana hasa kwenye vituo vya radio, tv, magazeti na sehemu mbalimbali. ugonjwa huu uligundulika karne ya 20 na mpaka sasa umeshaua watu wengi sana na zaidi ya 95% ya wagonjwa waliambukizwa kwa kushiriki ngono bila kinga.ni ugonjwa amabao hauna tiba wala kinga na mpaka sasa kulingana na data za shirika la afya duniani watu million 50 duniani kote wanasumbuliwa na ugonjwa huu.lakini bado kuana watu wengi wana uupuza wakati wa kuanzisha mahuasiano wakiamini macho yao kwamba huyu hawezi kua nao.
ugonjwa wa gonorea; huu ni ugonjwa wa zinaa ambao unashambulia jinsia zote yaani wanaume na wanawake, mara nyingi mwanaume hawezi kujificha na ugonjwa huu kwani dalili za ugonjwa huo kama kutoka na usaa kwenye njia ya kukojolea zitamuumbua lakini kwa wananwake ugonjwa huu huweza kukaa kimya na mwana mke hujikuta akisambaza ugonjwa huo bila kujua. mwishoni ugonjwa huu hushambulia kizazi na kusababisha ugumba.
mwisho; sio vipimo vyote vilivyotajwa hapo juu vinapatikana kirahisi sehemu zote lakini hata kama havipatikani vyote basi ni muhumu upime baadhi ya ambavyo vinapatikana kwenye eneo unaloishi ili kuikinga afya yako na kuwakinga uwapendao.
No comments