"Unatakiwa uwe na subira japo unahamu kubwa, angalia usije ukaharibu na
usimtongoze msichana hapo hapo, kinachotakiwa ni kufuata masharti madogo
na uwezo mkubwa wa kuangalia na kutafakari..".
Facebook
ndio habari ya mjini..., kila mtu yupo na kila msichana mzuri au mbaya,
hata yule wa kwenye ndoto zako anaitumia, na ni sehemu iliyo na
wasichana wengi zaidi waliounganisha na mtandao mmoja kuliko mtaani,
mashuleni na maofisini. Na kizuri zaidi kupita yote hayo, hata kama uwe
na aibu ya kutongoza kiasi gani, face buku huwezi kutetemeka hata
ukucha, unachotakiwa kujua ni mpangilio kwanza ili uweze kuwavutia
wasichana wa kila aina. Facebook
ni msitu wa wasichana, kwa hio inakupasa kuwa na subira japo kuwa
unaham kubwa, angalia usije haribu na usimtongoze msichana papo hapo,
kinachotakiwa ni kufuata masharti kidogo ambayo kiumeni.com inakupa na
uwezo mkubwa wa kuangalia na kutafakari...
Safisha picha zako...
Futa
picha zako zote zile mbaya na ambazo haziitajiki, kwa mfano zile
ulizopiga baa na vimada tofauti tofauti, na sidhani kama ulitakiwa
uziweke intaneti kila mtu hazione!, hakikisha umetoa picha zote za
wanawake wakiwa watupu hata kama ulikua umezishea tu, maana zinaleta
muuonekano mbaya kihisia na zinamwonyesha msichana kwamba wewe sio mtu
mzuriwa
kuanzisha mahusiano naye, zifute na zile ambazo umejipiga mwenyewe, kwa
vyovyote vile hazikuonyeshi ukiwa mtanashati, hakikisha zimebaki za
kwako peke yako na hata kama za marafiki zisiwe na hisia zozote ambazo
zinaweza kumfanya msichana hahisi hujatulia.
Tengeneza marafiki zaidi...
Ukiweza
kupata marafiki wengi zaidi, ndivyo utakavyo kuwa unaongeza wigo mpana
zaidi wa kumpata na kumchambua yule mwenye mvuto zaidi uliokua ukimwota
kwenye ndoto zako, kwa hio kama kiumeni.com tunavyokushauri hakikisha
unajiunga na marafiki wengi zaidi uwezavyo, tafuta hata wale uliosoma
nao zamani na jiunge kwenye magrupu ya facebook ili upate marafiki
zaidi.
Marafiki wa marafiki...
Kama
ukiwa umeweza kujiunga na marafiki wengi, utakua na nafasi kubwa ya
kumchambua yupi unaemtaka, angalia komenti zote zinazopita pamoja na
picha mbali mbali zinazopita, ukimwona yule aliyekushika macho na hisia
kakomenti, hata kama kakomenti kwenye komenti ya rafiki yako, na wewe
komenti hapo hapo na hakikisha umeweka na komenti tata juu yake ili
apate sababu ya kukujibu wewe, na kama hajatoa maoni, tafuta rafiki
unayemjua aweze kukutambulisha kwake, muulize rafiki yako kiungwana kwa
mfano... "Mambo, nimemwona msichana mrembo rafiki yako Angel, unaweza
kunitambulisha kwake?", hili swali lipo moja kwa moja na sidhani kama
anaweza kataa kukutambulisha.
Mtumie mwaliko wa kuwa marafiki...
Kwa
hio kama mmeweza kukomenti hapa na pale pamoja, sasa hivi atakua
ameshakujua, mtumie mwaliko wa kuwa marafiki, kuna asilimia kubwa sana
lazima akubali, na mkisha kuwa marafiki sasa unaweza kuanza kukomenti
kwenye maandiko yake na picha zake, pia mnaweza piga stori za hapa na
pale kwa kuchati, baada ya maendeleo kwenda vizuri na mazoea yamekua ya
kutosha, unaweza mwomba siku moja muweze kutoka wote mtoko!.
Vuta subira na kuwa jasiri...
Iwapo
ikitokea asipokujibu, japo ni mara chache sana iwapo umefuata maelezo
vizuri ya kiumeni.com, usije chukulia haraka na kukurupuka, usimuulize
chochote kuhusu hilo, endelea na stori, mpe muda na subiri tena wakati
mwingine mwafaka wa kumba mtoko tena. Ili kuongeza mafanikio unaweza fanya kwa msichana zaidi ya mmoja, maana samaki ni wengi sana baharini.
Jinsi ya kutongoza msichana kwenye mtandao wa facebook
Reviewed by Unknown
on
May 17, 2018
Rating: 5
No comments