Namna rahisi na salama ya kupunguza tumbo
Wengi wa wasomaji wamemtumia meseji za kutaka kujua njia ya kupunguza
mafuta tumboni, wanawake kwa wanaume walituma maswali kwa wingi. Njia
iliyosalama ya kupunguza mafuta katika tumbo au kupunguza tumbo kubwa ni
ile ya kupangilia chakula na kufanya mazoezi.
Nilipata nafasi wiki hii ya kuzungumza na daktari mmoja katika hospitali
ya mkoa wa Iringa ambaye sitamtaja kwa jina na alikuwa na mengi ya
kuelezea jinsi hali hiyo inavyoanza na husababishwa ni nani. Alisema
kuwa,kama unataka kupunguza tumbo kwa haraka basi punguza kula vyakula
vyenye wanga na badala yake tumia mbogamboga na matunda kwa wingi.
Vyakula kama viazi mviringo, wali mkate hukaa tumboni kwa zaidi ya siku
tatu, pia ulaji wa nyama nyekundu inasababisha kuongezeka uzito na pia
huongeza ukubwa wa tumbo,vyakulahivyo vinatakiwa kutumiwa kwa kiasi
kidogo sana. "Kuna wakati tumbo linajitokeza na kuwa kubwa kuliko
kawaida hali hiyo inasababishwa na kula vyakula vya wanga kwa wingi,
kutokunywa maji ya kutosha na pia kula bila ya mpangilio maalum"
anasema. Anasema kuwa kama ntu anataka kupunguza mafuta au kuondoa
kitambi anatakuwa kula milo mitatu kwa siku na si kujinyima kula kwa
kudhani kuwa unaweza kupungua uzito. "Vyakula vya wanga na mafuta ufanya
mtu kunenepa, acha au kupunza kula vyakula vyenye wanga ili kupunguza
mafuta yaliyozidi mwilini, mafuta yanaporundikana mwilini athari moja
kubwa ni kuwa na tumbo kubwa." anasema. Anasema kuwa,tumbo kuwa kubwa ni
dhahiri kuwa chakula unachokula hakifanyi kazi inayotakiwa, kumekuwa na
ziada mwilini na hii ziada inafanyika mafuta ambayo hujiwekesha akiba
katika maeneo mbalimbali ya mwili. "Kwa kuwa Chakula hiki cha ziada huwa
hakitakiwi, mwili hukibadilisha na kuweka akiba katika mfumo wa mafuta
kitaalamu kama glycogem.Unaweza kukabiliana na kuzidi kwa protini
zinazoyeyushwa na kuwekwa katika akiba kwa mfumo huo wa mafuta" Daktari
huyo anasema kuwa, mtu mwenye tatizo hilo ni bora akapangilia mlo wake
kwa siku.
"Asubuhi pata kifungua kinywa kilichokamilika, pata mlo wa mchana kama
kawaida na usiku kula matunda tu kunaweza kufanya mwili wako uwe katika
hali inayotakiwa. "Watu wengi wanatumia wanga mwingi wakati wa usiku
muda ambao unaenda kulala na ziada ya chakula haifanyi kazi vizuri zaidi
ya kujikusanya, kujibadilisha na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali
ya mwili hasa tumboni" anasema Daktari. Je Mazoezi husaidia kupunguza
uzito wa mwili na manyama uzembe? Mazoezi ya viungo yamethibitishwa
kusaidia kuchoma mafuta ya ziada katika mwili. Kutokana na hali ya ulaji
unaweza kutengeneza manyama uzembe katika kifua, mapaja na maeneo
fulani ya tumbo ambayo yametengenezwa kupokea maeneo ya ziada
yanayotokana na mafuta yenyewe au sukari iliyobadilishwa kuwa mafuta.
Nishati inayotokana na nafaka ambayop haiwezi kutumika muda huo
hutengenezwa kuwa mafuta na kupelekwa eneo husika. Wanaume huwa na
asilimia 8 hadi 20 ya mafuta katika mwili na ni kawaida wakati kwa
wanawake ni asilinia 13 hadi 25.
Unapofanya mazoezi ya viungo unaongeza hewa ya oksijeni kwa wingi katika
mapafu yako na wakati huohuo mwili nao unaunguza mafuta ili kutoa nguvu
kwa mwili. Mafuta yanayounguzwa kwanza ni yale ya kawaida kabla ya
kuingia katika akiba. Kuna umuhimu wa kutambua kuwa mazoezi ni kitu cha
bure na kama ukifanya kwa mpangilio na vizuri hutakuwa na shida ya
kutengeneza shepu yako. Dk.Martica Heaner,M.A, M.Ed. ambaye hutoa
mawaidha ya keep fit ndani ya MSN anasema ni jambo la heri kama mtu
atakula kidogo kabla ya kuanza mazoezi ili kutoa nishati ya kutosha ya
kufanyisha mazoezi. "Lakini kama unaenda mwendo fulani mdogo tu au
unatembea kwa dakika 30 huenda usiwe na haja kabisa ya kula hata hicho
kidogo na hasa ikiwa uliweka kitu kiogo saa tatu zilizopita" anasema.
No comments