HATARI:Kufanya Mapenzi Kwa Njia Ya Mdomo
Shirika
la Afya Duniani (WHO) limethahadharisha kuwa, kushiriki mapenzi kwa
njia ya mdomo kunasababisha ongezeko la ugonjwa wa kisonono ambao kwa
sasa umekuwa mgumu kutibika kutokana na bakteria wanaosababisha kuwa
sugu.
Aidha,
WHO imeeleza kwamba, kupungua kwa mtumizi ya mipira ya kujamiiana
(condoms) kunachochea kwa kiasi kikubwa kusambaa kwa ugonjwa huo wa
zinaa.
Ugonjwa
wa kisonono kwa sasa umekuwa mgumu kutibika na katika mazingira mengine
hautibiki kabisa kutokana na kuendeleza usugu wa dawa (antibiotics) kwa
kasi sana.
Ugonjwa
wa kisonono husababishwa na bakteria wanaojulikana kitaalamu kwa jina
la Neisseria gonorrhoea. Ugonjwa huu husambazwa kufanya ngono isiyo
salama kwa njia ya uke, mdomo au njia ya haja kubwa.
Dalili
za ugonjwa huu ni pamoja na kutoka maji maji ya njano au kijani katika
sehemu za siri, maumivu makali wakati wa kukojoa, pamoja na kutokwa na
damu.
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na WHO katika nchi 77, bakteria
wanaosababisha kisonono wameonekana kuwa sugu katika dawa zilizokuwa
zikitumika kutibu.
Dr
Teodora Wi, kutoka WHO amesema kulikuwa kuna kesi tatu kutoka Japan,
Ufaransa na Uhispania ambapo ugonjwa huo ulishindikana kabisa kutibika.
Alisema kila mara wakianzisha dawa mpya kutibu ugonjwa huo, bakteria
huyo aliweza kuihimili dawa hiyo mpya.
Jambao
hatarishi zaidi ni kuwa, maambukizi ya ugonjwa huu yapo kwa wingi
katika nchi maskini ambapo usugu huo ni mgumu kugundulika.
Ugonjwa
wa kisonono unaweza kuathiri uke au uume, njia ya haja kubwa pamoja na
koo. Lakini athari za koo ndizo zinazotishia dunia kwa sasa kutokana na
watu wengi kujihusisha na mapenzi kwa njia ya mdomo.
Dr
Wi alieleza kuwa bakteria hao hukaa sehemu ya nyuma ya koo na mgonjwa
anapoanza kupata maumivu na kutibu kwa kutumia dawa za kawaida,
hupelekea bakteria hao kujenga usugu dhidi ya dawa hizo na nyingine
zitakazotumika mbeleni.
No comments