Kwanini Kupiga Punyeto sio Jambo Baya....Hizi Ndizo Faida zake Muhimu Sana Kiafya
Ukweli
ni kwamba, jambo la kujichua/kupiga punyeto limekuwepo kwa miaka mingi
sana. Ni sawa kabisa na ni jambo la kawaida kama unaogopa kupiga
punyeto, lakini ni vizuri ukajua kwamba watu wamekuwa wakifanya hicho
unachokiogopa kwa karne nyingi sana zilizopita.
Hii inamaanisha kwamba kupiga punyeto ni jambo la kawaida kabisa ingawa
kuna dhana potofu inayohusishwa na kitendo hiki. Jambo la kuvutia zaidi
ni kwamba takwimu zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya wanawake na
wanaume wote wanaamua kufanya jambo hili wanapojisikia. Hatutakiwi kuwa
wanafiki kwenye hili, ila tunachotakiwa ni kujua faida na hasara za
kujiingiza kwenye kupiga punyeto.
Zifuatazo ni faida za kupiga punyeto kama yawezekana ulikuwa hujui kwamba jambo hilo lina manufaa:
Dawa tosha ya kukulaza
Kujishika sehemu zako za siri au kupiga punyeto inasaidia kupunguza
shinikizo la damu na kusababisha kutengenezwa/kuachiwa kwa endorphins,
aina ya kemikali inayohusika na kupunguza mfadhaiko (stress) na kuufanya
mwili ulegee. Hii ndio sababu kwanini neva za fahamu zinatulia baada ya
kumaliza jambo hili, bila kusahau hisia za usingizi zinazofuata
baadaye.
Inasaidia kuzuia maumivu wakati wa hedhi
Kwa wanawake, kujiridhisha mwenyewe unapokuwa katika siku zako kunafanya
mzunguko wa damu kwenye nyonga kuongezeka, jambo litalofanya maumivu
yapungue. Hali unayoipata wakati unafika kileleni pia inaweza kusaidia
na bila shaka inazidi starehe unayojipa kwa kutumia maji ya moto,
wanawake wanalielewa vizuri hili.
Inakupa fursa nzuri zaidi kujistarehesha kimapenzi
Kama msemo unavyosema, mazoezi hufanya uliweze jambo kwa umaridadi wa
hali ya juu. Washauri wa maswala ya ngono wanashauri kwamba, wanawake
ambao hawajawahi kufikishwa kileleni kwa tendo la ndoa wanatakiwa kuanza
kujipa raha hiyo yeye mwenyewe. Hii itawafanya waweze kuyajua vizuri
zaidi maumbile yao na kuweza kujigusa sehemu ambazo zinawapa raha zaidi.
Utaweza kujijua mwenyewe vizuri zaidi ikiwa ni pamoja na kiwango gani
cha starehe kinaweza kukukidhi.
Inasaidia kuzuia saratani ya tezi dume
Hii yawezekana ikawa ni habari njema sana kwa wanaume wengi. Punyeto
inasemwa kuwa inasaidia kupunguza hatari za kupata kansa ya tezi dume.
Sumu huwa zinajikusanya kwenye mrija wa mkojo lakini kumwaga manii
kunafanya sumu hizo zitolewe nje ya mwili jambo linalompunguzia mwanaume
hatari ya kupata saratani hii.
No comments