Madhara Ya Vidonge Vya Kuzuia Mimba


Vidonge vya kuzuia mimba huwa na hormoni za estrojeni na projesteroni zilizotengenezwa kwa ajili kuzuia hutoaji wa yai kutoka kwenye ovari kwa. Mara nyingi dawa hizi hutumika kuanzia siku ya tano ya mzungungo wa hedhi kwa muda wa siku 21 na huwa na madhara yafuatayo kwa mtumiaji

Msongo wa mawazo na hasira
Kipandauso na maumivu ya kichwa
Kupoteza hamu ya kufanya mapenzi
Kichefuchefu na kutapika
Kuongezeka uzito
Tumbo kuvimba na kujaa gesi
Nyongo kujaa mawe
Homa ya manjano
Kukosa hedhi au kuwa na mzunguko usio kawaida
Kutokwa na usaa au damu sehemu za siri
Uvimbe katika kizazi
Maziwa kuuma
Maumivu ya miguu
Mabaka mabaka usoni
 Pamoja na kuwa na madhara haya vidonge hivi bado ni muhimu kwa ajili ya uzazi wa mpango hivyo ni muhimu kuwasiliana na wataalamu wa afya kabla ya kutumia ili kutambua matumizi sahihi na muda wa kuanza na kuacha matumizi ya vidonge hivi kabla ya kusababisha madhara makubwa zaidi

No comments