Mazoezi 12 Ya Kuongeza Nguvu Za Kiume
Nguvu
za kiume huhusisha mambo mengi. Hayani pamoja na, hamu ya mapenzi;
kusimama kwa uume barabara; kuchelewa kufika kileleni kiasi cha
kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi
na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo lenyewe. Kuna viungo vingi
mwilini vinavyohusika na nguvu za kiume.
Viungo
hivi ni kama ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija
iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa na kadhalika. Kukosa nguvu
za kiume ina maana kuwa kiungo kimoja kati ya viungo vyote husika
hakifanyi kazi kwa mfano figo yaweza kukosa kufanya kazi hivi basi
kusababisha kukosa nguvu za kiume.
Kuna
mambo kadhaa yanayosababisha ukosefu wa nguvu za kiume kwa mfano
kupatwa na maradhi, vyakula unavyokula na mtindo wa maisha huweza
kufanya viungo kutofanya kazi. Baadhi ya maradhi hayo ni ugonjwa wa
sukari, presha ya kupanda, presha ya kushuka.
Tabia
zinazosababisha viungo kutofanya kazi ni kama uvutaji wa sigara,
kuchelewa kulala, kutopata usingizi, kujinyanyua, unywaji wa pombe,
utumiaji wa madawa ya kulevya au kufanya kazi kupita kiasi hivi basi
kukosa wakati wa kupumzika. Sababu nyingine ni kama kutumia nguvu nyingi
kusukuma choo kwa sababu ya tatizo la kusukuma choo, kutokunywa maji,
uzito mwingi, kitambi na hasa kutofanya mazoezi.
Kuna
njia nyingi za kuongeza au kurejesha nguvu zako za kiume kwa mfano
unaweza kubadilisha vyakula unavyokula kama kula nafaka zilivyo na nyuzi
nyuzi kwani nafaka husaidia kuongeza homoni za kiume, kula asli, kula
matunda mengi, kula tangawizi, kunywa vanilla na kunywa maji mengi.
Njia
nyingine ni kumtembelea datary na kumwambia shida yako, anaweza kukupa
tembe au akudunge sindano kama njia ya kukusaidia njia ya mwisho na
ambayo tunazungumzia ni kufanya mazoezi ambayo husaidia uongeza nguvu za
kiume. Kati ya njia hizo zote hakuna ambayo utapata matokeo yake kwa
siku moja, utahitaji kufuatilia njia hiyo na kuwa na uvumilivu na imani
kuwa utasaidika mwishowe.
Kuna mazoezi mengi ambayo husaidia kurejesha nguvu za kiume kwa mfano:
1- Kujiinua pande ya juu ya mwili
Zoezi
hili huhitaji uweke mpira wa zoezi chini na uwekelee mguu wako juu yake
huku ukitumia mikono yako hushikilia upande wa juu wa mwili wako.
Hujaribu
kuonyesha kuwa unapoweza kushikilia mwili wako kwa muda mrefu basi
utaweza kuongeza nguvu zako za kiume zaidi. Sehemu ya mwili inayoongezwa
misuli ni mabega, kifua na upande wa mbele wa mkono pande juu.
2- Kujiinua pande ya chini ya mwili
Aina
hii ya zoezi inahitaji ulale wima kwa mgongo kasha uinue miguu yako
hadi kwenye kifua na kisha ushikee miguu yako kutoka nyma kwa sekunde
thelathini.
Rudia jambo hili kwa mara nyingi kama utakavyoweza. Husaidia sehemu ya chini ya mgongo na kutengeneza misuli ya tumbo.
3- Pande ya chini ya mwili
Zoezi
hili unafaa kupiga magoti na kuweka sehemu ya juu ya mwili wima kasha
unafaa kuinamisha sehemu ya juu ya mwili pole pole huku ukiinama zaidi
hadi mahali ambapo utashindwa kurudi nyuma zaidi.
Kaa
hivyo kwa sekunde thelathini kisha upumzike na kurudia zoezi hili kwa
mara kadhaa. Zoezi hili husaidia kuongeza misuli sehemu ya juu ya miguu.
4- Kuongeza nguzu sehemu ya kati ya mwili
Katika
zoezi hili unafaa kusimama huku ukiwa umerudisha mguu moja nyuma na
mwingine mbele na kuinamisha sehemu ya juu ya mwili nyuma.
Miguu
inafaa kuwa na tofauti ya mita moja na kiuno kinafaa kuwa umekisukuma
mbele. Baada ya dakika moja geuza miguu. Zoezi hii husaidia kuongeza
misuli ya kiuno.
5- Uvumilivu
Zoezi hili hufanywa kama umelala kwa mgongo huku umekunja miguu yako na mikono ikiwa wima pande zote za mgongo.
Kisha
uinue kiuno na kukaa hivyo kwa dakika kadhaa, zoezi hili husaidia
kupima uvumulivu wako ukiwa umeinua kiuno na kusaidia kuongeza nguvu
katika kiuno chako.
6- Kuinua uzito
Kuinua
vitu vyenye uzito ni aina ya zoezi inayosaidia kuongeza nguvu za kiume.
Zoezi ya aina hii husaidia mtu kujiamini kwa chiochote anachofanya hata
anapoinua vitu hivyo vyenye uzito.
Kuinua
kwa vitu vizito kama mawe husaidia kuongeza misuli mikononi hasa upande
wa juu, upande wa mbele. Misuli hio husaidia kuongeza nguvu mwilini.
7- Kutembea
Hii
ni aina rahisi ya zoezi ambayo haihitaji matumiizi ya nguvu nyingi
lakini watu wengi hawapendi zoezi hili. Badala yake watu hupenda
kuendesha magari ili wasichoke.
Kutembea
husaidia kupunguza uziti na kitambi. Vile vile kutembea husaidia
kupunguza uchovu baada ya kufanya kazi ambayo haihitaji nguvu nyingi.
8- Kuchuchumaa
Hii
ni aina ya zoezi ambayo unahitaji kuekelea mikono yako kwenye kiuno
chako na kuchuchumaa hadi chini ambapoutakua umekalia miguu yako na
kuinamka bila ya kuondoa mikono kutoka kwa kiuna na bila kuondoa miguu
mahali ilipo.
Zoezi ya aina hii husaidia kuongeza nguvu na misuli pande ya nyuma ya miguu ili kuweza kushikilia mwili.
9- Kuruka
Kuruka
ni zoezi nzuri kwa kuongeza nguvu za kiume. Unaporuka unaongeza miguu
yako nguvu na misuli kwani unapoondoa mwili juu unahitaji kusimama au
kujishikilia vizuri ili usianguke.
Mazoea ya kuruka huhakikisha miguu ina nguvu ambalo ni jambo la muhimu sana katika uongezaji wa nguvu za kiume.
10- Kuogelea
Kuogelea
ni tendo la kuingia katika maji mengi na kutoka mahali pamoja hadi
pengine bila ya kutembea. Kuogelea husaidia mikono na miguu yao.
Unapoogelea
misuli ya miguu na misuli ya mikono yako huongezeka, nguvu vako mwilini
huongezeka kwani unatumia mwili wote katika kuogelea. Miguu husonga na
mikono vile vile hivi basi mishipa ya damu lazima ipeleke damu nyingi
mikononi na miguuni.
11- Kutembea kwa haraka
Hii
ni tofauti na kukimbia na pia ni tofauti sana na kutembea. Kitu cha
muhimu kujua ni kuwa unahitajika kutenganisha miguu yako kwa mbali na
kwa haraka.
Unapotenganisha
miguu na kutembea kwa haraka misuli ya upande wa juu wa mguu
inaongezeka na pia mishipa ya damu inasafirisha damu upande wako wa juu
wa mguu. Hili ni jambo la muhimu sana kwani maana moja ya nguvu za kiume
ni kuweza kusimama kwa uume barabara na ili uume usimame unahitaji damu
kuwepo.
12- Kulala
Hii
si aina ya zoezi lakini ni muhimu kwa mazoezi niliyoyataja hapo awali.
Usingizi husaidia kupumzisha mwili pamoja na viungo vyote vya mwili.
Kupumzisha mwili ni muhimu ili wakati ambapo unahitaji kufanya chocho
uwe na nguvu zinazofaa.
Usipolala,
wakati ambapo unahitaji nguvu zako za kiume, mwili utakuwa umechoka
hivi basi viungo vyako vya mwili havitatoa matokeo.
No comments