Zijue Faida Tatu za Tendo la Ndoa!
“Watu wanaoshiriki tendo la ndoa mara kwa mara, huwa hawa umwi umwi hovyo”,
anasema Dkt.Yvonne K. Fullbright, mtaalam wa afya ya tendo la
kujamiina. Baada ya nukuu hii kutoka kwa mtaalam, sio ajabu basi
tukisikia kwamba faida kuu ya kwanza ni kuimarisha uwezo wa mwili wako kupambana na maradhi (strengthen
your immune system). Uchunguzi uliofanyika Chuo Cha Wilkes huko jimbo
la Pennsylvania, ulibaini kwamba kati ya wanafunzi waliojihusisha na
vitendo vya kujamiiana mara moja au mbili kwa wiki, walikuwa na
virutubisho zaidi vya kupambana na maradhi mwilini ukilinganisha na wale
ambao walishiriki tendo hilo chini ya hapo. Pamoja na faida hiyo ya
tendo la kujamiiana, wataalam walisisitiza kwamba ni muhimu kwa watu
kuendelea kufanya vitu ambavyo pia ni muhimu kwa uimarishaji wa
virutubisho vya kupambana na maradhi mwilini. Vitu hivyo ni kama
ifuatavyo:
- Kula vizuri
- Kufanya mazoezi
- Kupata usingizi wa kutosha
- Kuhakikisha umepata chanjo zote muhimu kwa ajili ya maradhi ambukizi
- Tumia kinga (condom) kama hamfahamu hali zenu (Katika hili, thehabari tunashauri kama wewe ni mume, basi tafuta mke wa kuoa, na kama wewe ni mke, basi tafuta mume. Baada ya hapo, tulia katika ndoa yako, michepuko sio dili!!!)
Pamoja na kwamba kufanya mazoezi imetajwa kama nyongeza ya tendo la
kujamiina kama vitu ambavyo vinaongeza vurutubisho vya kupambana na
maradhi mwilini, tendo la kujamiina peke yake linahesabika kama mazoezi.
Ndio maana, faida kuu ya pili ni kukufanya ufungue gym kitandani. Kwa
maneno mengine, kujamiiana ni njia moja wapo ya mazoezi. Hapa
ni muhimu kukumbuka kwamba hata mazoezi yanahitaji mapumziko, kwahiyo
usije ukafanya tendo hilo kutwa nzima (kama unao ubavu) na kutegemea
faida, badala yake utachuma hasara, ambazo sio mjadala wetu leo. Kama
tendo hili litafanyika kwa umakini na utaratibu maalum, basi wataalam
wanasema tendo hilo linachoma kalori (calories) tano kwa dakika, kalori
nne zaidi zinachomwa ukilinganisha na mtu anayeangalia TV!
Sababu kuu ya tatu, tendo la kujamiiana linapunguza uwezekano wa kuvamiwa na mshtuko wa moyo (heart attack!). Ukiachilia
mbali kwamba tendo hili ni njia nzuri ya kuongeza mapigo yako ya moyo,
pia ni njia nzuri ya kuhakikisha viwango vyako vya estrogen na
testosterone vipo katika mizani sahihi kitu ambacho ni muhimu linapokuja
suala la kuzuia uwezako wa kupatwa na mshtuko wa moyo, wataalam
wanamalizia.
Hizi ni baadhi tu ya faida, bila shaka unazifaham faida nyingine lukuki,
ambazo hazikutajwa hapa. Kama tulivyoonya hapo juu, kujamiiana ni tendo
la kiungwana na lina faida nyingi kwa afya yako, hivyo basi, tafuta mke
au mume, halafu dili nae! Michepuko sio diliii!
Kizungumkuti
No comments