HII NDIO SABABU YA WANAUME WENGI KUPENDA WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA
Wanaume wanapendelea wanawake wenya makalio makubwa
Je wajua kwanini wanaume wanawapenda wanawake waliojaliwa na makalio makubwa ?
Katika majarida mengi umewaona
wanaume wakikodolea macho picha za wanawake wenye makalio makubwa iwe ni
kim Kardashian, Jenipher Lopez Nicki Minaj na Vera Sidika kutoka Kenya .
Sasa basi Utafiti umedhibitisha kuwa ni kweli wanaume wanapenda wanawake waliojaaliwa sehemu ya nyuma.
Kulingana na utafiti wa chuo kikuu Bilkent , chuo kikuu cha Texas, na chuo kikuu cha American University kilichoko mjini Beirut
Wanaume wanakisia kuwa mwanamke
mwenye makalio makubwa anaweza kufanya kazi kwa bidii zaidi ya mwanamke
ambaye hana makalio makubwa.
Hata hivyo kinachowavutia wanaume si makalio haswa bali ni kupinda kwa uti wa mgongo unaosababisha tako kuonekana zaidi.
Kim Kardashian
Utafiti huo unasema kuwa upinde wa 45.5 ndio unaovutia wanaume zaidi.
Wanaume walioneshwa picha za makalio
ya wanawake wengi na asilimia kubwa iliwapendelea wanawake wenye
makalio yaliyopinda kwa kiwango cha 45.5
Aidha zaidi ya asilimia 30% walisema wangalimchukua mwanamke mwenye makalio makubwa zaidi ya yule waliye naye sasa.
Kwa mujibu wa utafiti huo katika
miaka ya awali mwanamke aliyeonekana kuwa na makalio makubwa
alipendelewa kutokana na uwezo wake wa kubeba mizigo mgongoni.
Isitoshe mwanamke kama huyo aliwavutia wanaume wengi na hivyo kuwa na uwezo wa kuzaa watoto wengi.
Aidha mwanamke mwenye makalio
makubwa angeweza kustahili uzito wa mtoto aliyebebwa tumboni na hata
kustahilimi makali ya uzazi kuliko wale wenye makalio wastani.

No comments