JINSI YA KUEPUKA KUWA NA MPENZI MUONGO MAPENZINI.
MPENZI msomaji wangu suala la kumshukuru Mungu kwa uzima hata kunikutanisha pamoja nawe katika makala haya ni la muhimu mno, ni wazi kwa uwezo wake tumevuka changamoto nyingi kwa wiki nzima mpaka tunakutana tena tukiwa wazima na wenye afya njema.
Mbali na yote nikushukuru wewe msomaji wangu kwa kutenga muda wako na fedha kila wiki kununua Gazeti la Championi Jumamosi na kusoma vitu mubashara ambavyo unakuwa umeandaliwa yakiwemo makala haya ya mahaba.
Huu ni upendo mkuu mno kuuzungumzia. Kwa wasomaji wapya karibuni pia.
Mpenzi msomaji tuanze moja kwa moja kujadili mada ya leo ambayo kichwa chake kinaeleza;
‘JINSI YA KUEPUKANA NA MPENZI MUONGO.’
Niweke wazi kuwa wapo wasomaji wangu wengi ambao wamekuwa wakinitafuta mara kwa mara na kuniuliza kwamba wanawezaje kuepukana na kuanzisha uhusiano na watu ambao wanakuwa si wa kweli kwao? Hapa naweza kuongeza kwamba ambao si waaminifu bila kujali wanaume au wanawake kwa pamoja.
Sasa majibu ya jambo hili ni kwamba unapotaka kupata mpenzi mkweli au mwaminifu ni lazima kwanza wewe mwenyewe uwe mkweli kuanzia kwako mwenyewe na kwa huyo mpenzi wako, nitafafanua;
Ninaposema kuwa mkweli kwako mwenyewe ninamaanisha kujiuliza kama wewe ni mwaminifu kabla ya k u z u n g umz a nje kwa mpenzi wako.
Ukijaribu kuchunguza watu wengi wanaolilia kupata wapenzi wa kweli unakuta wao wenyewe si wakweli kwa wapenzi wao.
Mara kwa mara wanakuwa kwenye misuguano na hao wapenzi wao juu ya watu wengine ambao wanawahisi kuwa nao kwenye uhusiano. Sasa kwa minajili hii mwenzako anawezaje kuwa mkweli?
Ni muhimu kujitathimini pale ambapo unataka kupata mpenzi wa maisha ambaye atakuwa mkweli kwako na mwaminifu.
Kujitathimini kwenyewe ndiko huko kuwa mkweli katika uhusiano wako, kuwa na mpenzi mmoja au kuwa huna mpenzi kabisa pale unapoanza safari ya kumtafuta mpenzi kwa ajili ya kutengeneza naye maisha, yaani mwisho wa siku aje kuwa mke.
Napenda kusisitiza kuwa ikiwa wewe mwenyewe huwezi kuwa mkweli ni vigumu kumpata mpenzi mkweli katika maisha yako. Maana hata ikiwa utampata ipo siku anaweza kubadilika na kuwa si mkweli tena.
Ikumbukwe kwamba uwongo siku zote hujitenga na ukweli. Huwezi kuuficha siku zote uongo na kutegemea haipo siku itajulikana kwamba wewe ni
Sasa inapofika hiyo siku, mpenzi wako akagundua kwamba wewe mwenyewe ambaye unamlilia awe mkweli si mkweli kwake naye taratibu anaweza kuanza kubadilika kitabia na akafika hatua ambayo anaweza kuwa si mkweli tena.
Kwa hiyo, mpenzi msomaji wangu, tiba ya kumpata mpenzi sahihi, mkweli na mwaminifu ni hiyo tu, kuwa mkweli kwanza wewe mwenyewe. Hakuna mchawi katika hilo.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine tamu!
No comments