:Linogeshe penzi lako kwa kuzingatia mambo haya!
WAPENZI
wasomaji wangu, naomba leo niende moja kwa moja kwenye mada yangu ya
wiki hii ambayo kwa kiasi kikubwa inawagusa wanawake. Nazungumzia mambo
ambayo mwanamke anatakiwa kuyazingatia ili aweze kumshika ipasavyo
mumewe na kuinogeshandoa yake.
Ni mengi
anayostahili kufanya mke kwa mumewe lakini kwa leo nitazungumza machache
ambayo naamini yatakuwa na manufaa kwako.Timiza wajibu wako kama
mkeMwanamke anayemjali mume wake ndiye anayetimiza wajibu, lakini wengi
hujikuta wakisalitiwa au kuachwa kabisa na waume zaokutokana na ufahamu
mdogo amadharau ya mambo madogo.Ni busara kutambua kwamba, ndoa haina
mambo madogo. Kila kitu kina umuhimu mkubwa kulingana na nafasi yake
sambamba na utekelezaji wako. Mfano, kumpokea bahasha anaporejea kutoka
kazini ni kitu kidogo tu ambacho wewe unaweza kukidharau lakini thamani
yake kwa mumeo ni kubwa kuliko unavyofikiria.Tambua kuwa, mwanaume
harogwi kwa limbwata la sangoma, mahaba peke yake yanatosha kumshika
vilivyo. ‘Ukimhendo’ kwa kiwango kitakachomridhisha, hatawaza kukuacha.
Unawezaje? Jibu ni rahisi, muoneshe unampenda na uthibitishe mapenzi
yako kwa vitendo na si kwa maneno tu.Daima hili liwe kwenye akilini
yako, mwanamke kupitia mapenzi yake ana uwezo mkubwa mno, lakini lazima
awe anajua kutimiza wajibu wake kwenye maisha ya ndoa.Kama mumeo
anakuacha, ujue kuwa kuna mambo unayomkosea na kuyafanya mapenzi yako
yageuke kuwa kero kwake. Unyenyekevu kwa wanawake wa kisasa kimekuwa ni
kitu adimu sana kiasi ambacho kimekuwa kikihatarisha ndoa zao.Wanaume
wanawapenda wanawake ambao hujionesha waziwazi kuwa wenyewe ni wasaidizi
wao wakuu katika masuala mbalimbali. Hawavutiwi na wale ambao hupuuza
mambo kwa visingizio visivyokuwa na maana.Kuwa mjanja kianaSababu ya
wanaume kuwapenda wanawake wajanja ni kukwepa aibu wanazoweza kuzipata
pindi watakapokuwa kwenye uhusiano na wanawake washamba.Huogopa
kujiingiza katika mapenzi na watu wasio na uelewampana wa mambo ambao
huwafanya kuwa mafundi wa kuiga mambo yasiyofaa.Washamba mara nyingi
huwa ni malimbukeni, hujifunza mambo yasiyokuwa na faida kwa imani
kwamba naye ataonekana mtu kati ya watu. Wanawake wa aina hii ni rahisi
kuwaingiza wenzi wao katika hasara kubwa. Hawakawii kusaliti pamoja na
kudanganyika kwa mambo madogo.Wanawake malimbukeni huharibika vibarazani
na saluni kutokana na sifa kubwa ya umbeya kwenye sehemu hizo. Wanaume
wasiokuwa na subira hujikuta wakiwaacha wake zao mapema, mara tu
wanapoanza kuhisi nyendo zisizoeleweka kwa wenzi wao.Tumekuwa
tukishuhudia wanawake malimbukeni wakiiga tabia za ulevi wa pombe, kuwa
na makuu katika maisha yao kutokana na kuwaona wenzao wakiwa hivyo. Hili
ni tatizo ambalowewe mke wa mtu unatakiwa kuliepuka ili uishi milele na
mumeo.Siku zote mwanamke mjanja hawezi kuiga hovyo hovyo, siku zote
anajua kitu cha kuanzia na kinachofuata. Hadanganyiki kirahisi na hiyo
ni sifa kubwa ambayo inaweza kuinogesha ndoa yako kwa kiasi kikubwa.
No comments