MWANAMKE HUPASWA KULA VYAKULA HIVI PINDI UKIWA KATIKA SIKU ZAKO (PERIOD).
Katika kipindi cha mzunguko (siku za hedhi) kwa kawaida wanawake hupoteza kiasi cha damu pamoja na baadhi ya madini mwilini. Hivyo Hali hiyo huweza kusababisha upungufu wa damu kama mwanamke atakuwa hapati lishe bora na ya kutosha.
Sasa ili kuzuia upungufu wa damu na madini mwilini, msichana anatakiwa kula vyakula vyenye madini chuma na chokaa kwa wingi ikiwa ni pamoja na hivi vifuatavyo:-
Orodha ya vyakula vinavyopendekezwa
1. Mboga za majani
2. Maharage
3. Soya
4. Samaki
5. Maziwa
6. Korosho
7. Mayai
8. Zabibu (Juisi yake)
9. Matunda damu
10. Dagaa n.k.
Mbali na vyakula hivyo, pia mwanamke huhitaji kunywa maji ya kutosha kipindi hiki na kuzingatia hali ya usafi wa mwili, hasa sehemu za siri .Unatakiwa kutumia vitambaa safi vilivyo nyooshwa kwa pasi au pedi zilizohifadhiwa katika hali ya usafi.
No comments