RIPOTI MAALUM NI KWELI KUNA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME – 4
NI wiki ya nne tukiendelea kuwaletea mada hii ambayo wataalamu
mbalimbali wa afya ya binadamu wanatuelimisha kuhusiana na matatizo ya
nguvu za kiume ambayo sasa ni kama janga kutokana na wengi kuathirika na
maradhi hayo.
Mada hii imekuwa ikijadiliwa na madaktari watatu, Dk. Marise Richard,
Dk, Godfrey Chale na Dk. Leopord Mwinuka ambao wana zahanati za
kuwahudumia binadamu lakini pia Mtaalamu wa Lishe, Abdallah Mandai, leo
atapata nafasi ya kuelimisha kuhusu jinsi ya kuondoa tatizo la nguvu za
kiume kwa kutumia vyakula vya asili, endelea: Mandai anasema vyakula vya
nafaka ambavyo vimesheheni nishati nyingi na zina nyuzinyuzi (fibre) na
sukari, husaidia kutunza uzito wa mwili pia husaidia katika kuzalisha
homoni za testosterone kwenye damu na huwezesha mtu kuwa na nguvu
hatimaye kuongeza nguvu zake za kiume.
“Kula nafaka zisizokobolewa kama vile brown bread (mkate wa kahawia)
uliotengenezwa kwa ngano isiyokobolewa badala ya white bread (mkate
mweupe) pia kula nafaka halisi ni jambo zuri kiafya na kunafanya mwili
kutopata mafuta mengi, ikumbukwe mafuta mengi kwenye damu yanaharibu
mishipa ya damu ikiwamo ya uume. “Tangawizi ni aina ya kiungo mizizi
ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Mzunguko
unapokuwa mzuri huwezesha damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi ikiwamo
uume.
“Tangawizi imekuwa ikitumika sana maeneo ya asia kwa ajili ya wanaume
wenye tatizo la nguvu za kiume,” anasema Mandai. Viungo ambavyo viko
katika pilau huvaa kutumiwa na wenye matatizo ya nguvu za kiume kwani ni
viungo vyakula vinavyoimarisha nguvu za kiume.
Akaongeza: “ Kuna matunda yanayoitwa komamanga, kitaalamu Pemigranate
yenye rangi nyekundu husaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka
mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumwongezea mtu uwezo kwa kufanya
tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.” Mvinyo mwekundu unatajwa kuwa na uwezo
wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu huku ikimwondolea mtu
uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa. Hii ndiyo sababu kubwa kuikuta
ikiwekwa vyumbani katika hoteli nyingi kubwa duniani. Nchi kama Italia
mvinyo ni kinywaji ambacho hakikosekani mezani kutokana na kuaminika
miaka kwa miaka kwamba inasaidia kuongeza nguvu za kiume.
Unywaji wa kiasi unaweza kuwa na faida kubwa kwa kuchochea na kuamsha
hisia na kuweza kwenda mizunguko kadhaa. Mchanganyiko wa mbegu
mbalimbali za matunda ikiwamo tikiti maji, mbegu za maboga husaidia
kuondoa acid mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.
KIUME Vanila husaidia kuamsha hamasa mwilini, vanila ni aina ya
kirurubisho ambacho huwamo ndani ya vyakula ikiwamo ice cream. Asali ina
madini yanayoitwa boron ambayo husaidia mwili kupata homoni
zinazosaidia kuongeza nguvu za kiume. Hata vitabu vya dini hueleza ulaji
wa asali na masega yake kama mlo wenye kuupa mwili nguvu. Karanga
huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu na
kuuimarisha mzunguko huo katika maeneo ya uzazi, hivyo kuongeza nguvu za
kiume kwa mtumiaji mwanaume.
Pia karanga zina madini muhimu kama vile magineziamu, tindikali ya
foliki na madini ya zinki ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa
mbegu za mwanaume na kuongeza hisia. Vyakula vingine vinavyoongeza nguvu
za kiume vikiliwa kwa utaratibu unaofaa ni pamoja na pilipili manga,
mdalasini, makomamanga, kweme, njugu mawe nk. Baada ya kuona makala
zilizoeleza sababu mbalimbali zinazosababisha matatizo ya nguvu za
kiume, sasa tuwe pamoja kwa nguvu zote katika kipengele muhimu
kinachohusu suluhisho la matatizo ya nguvu za kiume. Kikubwa
unachotakiwa kufanya ili kuweza kupata msaada wa tatizo hili ni kuwa
tayari kuweka wazi tatizo lako kwa watoa huduma za afya wa tiba za
binadamu na siyo kwa watoa huduma wasiotambulika.
Ikumbukwe kuwa kuficha tatizo lako na kuendelea kusikiliza maneno ya
vijiweni kwa marafiki ambao hawana uelewa na mambo haya kunazidi
kukuchanganya na kukuchelewesha katika kupata matibabu sahihi, sehemu
sahihi na kwa wakati muafaka. Wagonjwa wengi huwa na aibu kufika katika
huduma za afya kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo hilo wakihofia
kunyanyapaliwa, lakini jambo hilo halipo kwa wataalamu wenye taaluma ya
tiba za binadamu. Kumbuka kuwa si wewe pekee uliye na tatizo hilo, ni
mamilioni ya watu duniani kote wana tatizo hilo hivyo unatakiwa
kujiamini na kujipa moyo kuwa tatizo hili linatatulika.
Wengi hutumia dawa zisizothibitishwa jambo ambalo ni hatari. Unaweza
ukawa unatumia dawa hizo na kupata nafuu na kudhani umepona, lakini
kumbe ukawa unaudhuru mwili wako pasipo kujua. Dawa hizo
zisizothibitishwa wala kupendekezwa kama ni salama na Taasisi ya Chakula
na Dawa (TFDA), zipo kila mahali mitaani na wengi hujikuta wakinunua na
kuzitumia kiholela. Miaka ya nyuma tatizo hili lilikuwa linaonekana
kujitokeza zaidi kwa wanaume wenye umri kati ya miaka 40 na kuendelea.
Lakini katika siku hizi hata vijana wa kati ya umri wa miaka 20 na 30
wanajikuta wanapatwa na tatizo hilo kutokana na wengi kutofanya mazoezi
na kutozingatia vyakula vya kula. Tatizo la nguvu za kiume linaweza
kutibiwa au likapunguzwa makali kwa matibabu mbalimbali baada ya
kufanyiwa uchunguzi yakinifu. Dk. Marishe Richard anasema yapo matatizo
ya nguvu ya kiume ambayo hujikuta hayatatuliki kwa njia yoyote, hivyo
mtu mwenye tatizo hilo huwa ni ulemavu wa kudumu. Je, mitishamba hutibu
ugonjwa huu?
Fuatilia wiki ijayo.
Fuatilia wiki ijayo.
NA @daktari_wamapenzi kwa instagram
Safi sana
ReplyDeleteSafi sana
ReplyDelete