Sababu 5 Zinazokufanya Uoe Au Kuolewa Na Mtu Ambae Si Chaguo Sahihi Katika Maisha Yako
KUNA baadhi ya sababu zinazosababisha watu kuoana pasipo kufanya maamuzi sahihi. Wanandoa wengi huingia katika ndoa wakitegemea mambo mengi kubadilika, kitu ambacho ni makosa yanayosababisha ndoa nyingi kuvunjika.
Kabla ya kuoa/kuolewa unapaswa Ujitambue Kwanza na ujiulize maswali kadhaa, kwanza jiulize; (1) Je huu ni wakati sahihi? (2) Kwa nini mtu huyu? na (3) Unamuoa au kuolewa na mtu atakaye kuwa sambamba na malengo yako katika maisha yako yote?
Wakati kuna sababu kadhaa za kumuoa/kuolewa na mtu sahihi, pia upande mwingine kuna sababu kibao zinazopelekea watu kuoa watu wasio sahihi kwao. Kabla ya kusema "Ndiyo" zingatia sababu tano hapa chini zinazokufanya uoe au kuolewa na mtu ambaye si sahihi ambae baadae hupelekea kutengana na kupeana taraka.
(1) Tumekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu. Kuwa katika mahusiano kwa kipindi kirefu sio sababu pekee ya kufanikiwa kumpata mwenye mafanikio katika maisha yako, unaweza ukawa umemvumilia kwa muda mrefu na sasa ukaamua tu kwasababu umekwisha zoea tabia yake na kufuata usemi wa "maji ukisha yavulia nguo sharti uyaoge".
(2) Msukumo wa Marafiki - Rafiki zangu wote wamekwisha OA/KUOLEWA....... itabidi na mimi nioe/niolewe. Kufuata mkumbo wa makundi katika jamii sii kitu kizuri, kwani ndoa siyokitu cha kubeep na kuacha. Jipange kwanza na muda ukifika basi itaingia katika ndoa yenye mpangilio mzuri wa maisha.
(3) Sidhani kama nitaweza. Usipo jiamini na kujipenda mwenyewe sidhani kama itakuwa rahisi kumpenda mtu mwingine unayetegemea kuwa nae maishani.
(4) Mategemeo ya kuboresha tabia ya mwenza wako. Tukisha oana nitambadilisha tabia. Cheti cha ndoa siyo leseni ya kumrazimisha mwenzi wako kubadilika kwa lazima. Jaribu kuwa na subira na kumtafuta mwenzi mnae endana nae kitabia.
(5) PESA - Anakazi nzuri naamini ataleta pesa au anatoka katika familia ya kitajiri. Kunaukweli mkubwa katika misemo ya wahenga yani "kama ukiowa kwaajili ya pesa, basi utazilipa" japokuwa kuwa na pesa sio vibaya, lakini hii haitazuia pia haizuii kuwa na muunganiko mbaya wa ndoa.
Wanandoa wengi huingia katika dimbwi hili ambapo wengine hushinikizwa kuoa kulingana na taratibu za kimila au kidini. Lakini pia wazazi wakati mwingine huchangia ndoa nyingi kuvunjika, ikiwa ni kwa kuwachagulia wananandoa mke au mume.
Vijana ambao bado hamjaoa au kuolewa "Jitambueni Kwanza", fikirini kwa kina kabla ya kufanya maamuzi yasiyo sahihi ambayo yatawagharimu muda wenu na kupata mateso ya muda mrefu.
No comments