Umuhimu wa kusamehe



Katika tafiti ambazo zimewahi kufanywa na wanasaikolojia miaka ya nyuma, waligundua ya kwamba watu wengi hawana maendeleo yao binafsi kwa sababu hawatambui nguvu ya msamahama iliyovyo na nguvu katika safari ya Mafanikio. Tafiti hizo hizo zinaendelea kusema watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wamebeba mizigo mizito ndani nafsi zao.

Mizigo hiyo mizito ambayo inawezekana kuna mtu alisabibisha mtu kuwa katika hali hiyo. Kwa mfano inawekana kuna ndugu,rafiki, mzazi aliwahi kufanya au kukutamkia maneno mazito ambayo yanakufanya Leo, kesho mpaka kesho kutwa usiwe kuyasahau. Maneno au vitendo hivyo vimekusababisha kwa kiasi kikubwa hupunguza hamasa za kiutendaji, magonjwa na mawazo mengi (stress).

Hebu tuangalie japo kwa uchache ni kwa kiasi gani madhara ya kutokusamehe yanavyoweza kukuathiri. Msipo msamehe mtu kunakupekea kwa kiwango kikubwa kuweza kupunguza uwezo wa kufikiri vitu vipya, hata hivyo pamoja na kupunguza uwezo wa kufikiri kunakupelekea kuzama katika dibwi kubwa la mawazo, hata hivyo mawazo hayohayo yanakupekea kujikita katika tabia zisizo za kimaadili kwa mfano ulevi, wizi na mengineyo mengi. Na pindi mtu atendapo  mambo hayo ambayo chanzo chake huwa ni mawazo madhara yake huwa ni makubwa kama nilivyoweza kuanisha hapo juu.

Basi bila kupata kigugumizi cha kusoma makala hii hebu jaribu kusoma kwa umakini na uingie  katika kilindi cha nafsi yako harafu jiulize umebeba vitu gani juu ya watu wengine? Kisha jaribu kutafakari kwa umakini tena mambo hayo yamekuathiri kwa kiwango gani? Baada ya kupata majibu sahihi juu ya jambo hilo, zama tenda katika mishipa ya ubongo wako kisha tafakari bila ya kujionea huruma ya kwamba unachukua hatua gani juu ya swala hilo. Majibu sahihi ambayo utakuwa umeyatafakari ndiyo ambayo yatakufanya uweze kuona mwangaza kwenye giza ni wapi ambapo unatakiwa kuelekea.

Pasipo kupoteza maana ya somo hili nieleze sasa ni kwa nini ni muhimu kusamehe;

1. Huongeza furaha ya moyo(piece of mind)
Kusamehe mtu mwingine humfanya mtu huyo kuwa huru kwa kila jambo ambalo analifanya. Kwani kama nilivyosema hapo awali ya kwamba watu wengi tumebeba mizigo mizito ndani ya nafsi zetu, hata hivyo kutoka na mizigo hiyo mizito tunashindwa kupiga hatua za kimafanikio. Hivyo ili kuweza kupiga hatua za kimafanikio hatuna budi kuweza kujifunza kuweza kuwaaemehe watu wengine waliowahi kutokosea . Hata vitabu vya dini vinatukumbusha ya kwamba Mungu tabia yake kusamehe hivyo nasi hatuna budi kusamehe wengine. Vitabu hivyo hivyo vya dini vinasema ya kwamba  saba Mara sabini. Na endapo utasamehe unafungua milango ya mafanikio yako.

2. Kusamehe ni njia ya mafanikio.
Endapo leo utaamua kusamehe ni ishara ya kwamba utaonfokana katika sakata la kuwa katika wimbi la mawazo , hata hivyo kupelekea wewe kuwa na mawazo chanya, mara kadhaa watu ambao hawana ule moyo wa msamaha kwa namna moja ama nyingine huwa hawapo sawa kwani huwa hawa amani hata kidogo, hata hivyo kama kweli uyataka Maisha yawe sawa ni muda wako sahihi wa kuvutua vile vyote vilivyomo katika nafsi yako kinyume cha hapo utakuwa unapotea hajalishi ulikwazika kwa kiasi gani. Pia ukumbuke wabaya watu, pia watu hao hao ndio wazuri na wana mchango mkubwa katika safari yako ya mafanikio.

3. Kusamehe huimarisha afya.
Afya njema ni njia ya kupata Mafanikio, moja ya kanuni ya kutaka kupata Mafanikio ni kwamba unahitaji kuwa na afya njema ili uweze kuimarika na kupata Mafanikio hayo. Hebu tutafakari kidogo hivi leo ukipata ugonjwa wowote na kukufanya usiweze kuendelea na kazi yako hivi huwa unaathirika kwa kiasi gani katika jambo lako? Kama umepata majibu Nafikiri utakuwa umeona umuhimu wa  kuwa na afya njema.

Watu wengi hawana hamasa za kiutendaji wa mambo mbalimbali kwani dhahiri ya kwamba miili yao tayari imeathiriwa na magonjwa mbalimbali yatokanayo na mawazo ambayo yamesabishwa na watu wanaokuzunguka. Kuna magonjwa ambayo Mara nyingi husababishwa na mawazo kama vile pressure. Hivyo enadapo utamua kuwasamehe watu wengine ambao waliwahi kukosea unaweza kuwa katika misingi ya kuimarika kiafya kiujumla, na kufanya hivyo kutakufanya uweze kuongeza uwezo wako wa kufikiri hata kukupelekea kuweza kupiga hatua za kimafanikio.

Hivyo tambua na elewa inahitajika nguvu ya msamaha ambayo leo itakufanya uweze kupata Mafanikio ya kweli.

No comments