Zifahamu Mbinu Mbalimbali za Kumpata Mpenzi Bora Katika Mapenzi



KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana.

Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza.
Ndio ukweli wenyewe

Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea.

Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi.

Maneno ya kusikia kutoka kwa wanawake
Wakati wa kumtongoza mwanamke tarajia maneno kama;

1. Nina mume au mchumba
Inakuwa kuwa ni kweli au njia ya kukataa

2. Niko bize na kazi`
Hii humaanisha kwamba hana muda wa kuzungumza au hata kuonana, ni dalili pia ya kukataa au kuvuta muda ili aendelea kukutafiti

3. Nimeokoka nampenda Mungu
Hii huwa na maana kwamba yeye ni mtu asiyependa uchafu hasa kama unamtongoza kwa lengo la kufanya ngono tu

4.Mimi nasoma, sitaki hayo hadi nimalize
Sitaki! Ni kwamba anaweza kujisemea kwamba hataki uhusiano uwepo. Anaweza kueleza sababu au kutoeleza.

5. Wewe sio mwanaume wa aina yangu;
Hapo huwa mwanamke anamaanisha labda una sifa tofauti na anazotaka, huenda wewe mwanaume ni mfupi, mweusi au tabia zingine zozote ambazo haziendani nae.

Msingi wa kuomba urafiki 
Kwa mwanamume mwenye umakini, huwa hakosi kupata anachotaka. Jiwe lake lazima litapiga anachokitaka, hasa kama atakuwa mwenye kufanya utafiti wa kina kabla ya kuamua kufanya kitu. Msingi sahihi wa kutongoza ni kufanya utafiti na kuongea kwa mitego, kabla ya kumfikia msichana unayemuhitaji.

Kwa mfano badala ya kusema twende tukale chakula cha mchana, sema utakuwa na muda kweli tukale, au uko bize? Maana yake ni kwamba huenda ni kweli akawa bize au la, lakini kama hataki atakwambia niko bize kama ndivyo unaweza kumuuliza nikuletee nini ninapotoka kula. Kwa namna anavyojibu vibaya au vizuri unaweza kupata mwelekeo wa nini unaweza kujibiwa kama unaongea wazi unachokitaka kwake.

Wanawake wanajua fika nini ambacho mwanaume anakitaka anapoanza kuongea hiki na kile, mara nyingi huwa wanafanya kana kwamba hawajui.

Mambo ya kuzingatia katika hatua ya uchumba
Ukweli ni kuwa uchumba ni wakati mzuri sana wa kuangaliana tabia ili hatimaye kuwa na chaguo jema. Hata hivyo ili kuwa na uhusiano mzuri ni lazima kufahamu kuwa wanadamu wanatofautiana, aidha kitabia au kimuonekano. Ni lazima kujifunza namna gani unaweza kuishi na watu wengine wenye hali tofauti.

Unaweza kuona watu wanatofautiana kitabia, huyo ni mzunguzaji sana, mwingine ni mpole, kiasi kwamba hata ukiwa nae ni kama uko peke yako. Kumlazimisha asiye na uwezo wa kuzungumza sana, awe mzungumzaji, sio sahihi sana, wala kumzuia mzungumzaji asifanye hivyo, pia sio sahihi
Wachumba wanaweza kutofautiana kwa kiwango cha elimu, uchumi, ufahamu juu ya mambo mbalimbali, kikabila, umri na hata kwa rangi pia. Kufahamu hili ni suala la msingi sana ili kuhakikisha.

Ingawa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakilazimisha kwamba wawe wanaoana na wale ambao ni wa kutoka kwenye madhehebu yao tu, wachumba wanaweza wakatoka katika madhehebu/makanisa tofauti na hili ni kwa kuzingatia madhehebu/makanisa mengi yaliyopo.

No comments