HAKIKISHA UMEISOMA HII YA LEO, VITU VIZURI 60 VYA KUMWAMBIA MSICHANA UMPENDAE




Ninamaanisha kuwa maneno matamu.Wakati kijana uko kwenye process ya kutafuta na kujaribu kuuteka moyo wa msichana, unatakiwa kujifunza  kutumia maneno matamu.Na lazima ujue kuwa sio kila neno  unalotumia litagusa moyo wa mwanamke unayemtaka,Lakini maneno matamu yanafanya kazi ya kushangaza .

 Wakati vijana wengine wanalalamika kuwa ni vigumu kuuteka moyo wa msichana, jibu ni rahisi kwa sababu hawatumii maneno sahihi. watu wengi pia  huwa hawana maneno ya kusema na wengine hawajui kabisaaa hata jinsi ya kuanza. sasa hebu tujifunze haya maneno ya kumwambia msichana unaempenda na unahitaji awe wako  milele.

1.Macho yako ni mazuri , yananifanya nipotelee kwako kila nikiyatizama.


2,Unanifanya niwe mwanaume bora , kwa hio nastahili  mapenzi yako.


3.Tumbo langu hutetemeka unapoleta mikono yako usoni pangu.


4.Wewe ni mzuri na ni mrembo  naogopa hata kukugusa naona kama nitakuchafua.

5.Unapotabasamu huzuni  kwangu hupotea , ghafla nakuwa mtu wa furaha.

6.Ungeweza kupata mwanaume yeyote duniani , lakini  umenichagua mimi.

7.Hapana.wewe sio mnene uko poa na ndivyo nipendavyo.

8.Ninapokushika nashisi kulegea kwenye magoti.


9.Wewe ni rafiki yangu, najifunza vitu vingi kwako,ndiye mtu ambae nimekuchagua, ndio mpenzi wa maisha yangu. ni wangu pekee, wewe ndio kila kitu kwangu.

10.Siamini , maana jinsi ulivyo amazing, lakini upo na mimi.


11.kila nikiangalia muda naona kama hautoshi kukupenda , natamani niwe na wewe milele. yaani wasife.

12.Umenifanya niamini kuwa zipo nafsi zinazoungana, zinazokutana pamoja.

13.Usiku nikiwa naangalia nyota na kuzilinganisha kila moja ili kuelewa ni kwa nini nakupenda,nilifanya vizuri hatimae nikazikimbia.

14.Kukutana nawe  ni kitu ambacho hakijawahi kutokea.

15.Unapoonyesha kunipenda, huwa nazidiwa na hisia , hapo hupotea kabisaaa.


16.Kabla ya kulala ni lazima kwanza nikupigie simu ndio nitapata usingizi.


17.Naweza kuwa nawe maisha yote, lakini bado nahisi kama  haitatosha  kukupenda.


18.Napata furaha nikiwa na wewe. 19. Napenda kutumia muda na wewe.

20.Napenda ngozi yako laini, ninapoigusa.


21.Natamani maishsa yangu yote nikuone ukiwa na furaha.                                       

22.Usibadilike nakupenda jinsi ulivyo.


23.Nikiwa na wewe nafurahi kama mtoto.


24.Napenda nywele zako.


25.Napenda nikukumbatie ninapokuaga.

26.Natamani kukubusu kila sehemu ya mwili wako.

27.Naanza siku na wewe ndani ya mawazo yangu, na ninamaliza  siku na wewe kwenye ndoto zangu.

28. ukiwa na mimi huwa natamani kusimamisha muda, maana muda unakwenda haraka.

29.Nikisikia sauti yako asubuhi , siku nzima ni mtu wa furaha.

30.Tabasamu lako zuri linanifanya niyeyuke.

31.Unaponiaga napata shida kukuruhusu uende.

32. Umenielewa vizuri, ni kama unasoma mawazo yangu.

33.Mungu alikupendelea kukuumba, akili na kila ulichonacho.


34.Najivunia kuwa na wewe na ninafurahia.

35.Napenda unavyosema unanipenda.

36.Mapenzi yetu ni kama mawimbi ya bahari,  wakati mwingi hutulia, na wakati mwingine huvuma,lakini yanarudi palepale.


37.mapenzi yetu yawe kama ua rose ambalo halina miiba.


38.Najua kwa nini watu wanatutazama , ni kwa sababu wewe ni mzuri kuliko mwezi.


39.Muda utakuwa hauna thamani endapo  sitatumia na wewe.


40.kama siku yangu ingeanza na busu lako, nisingehitaji kahawa.

41.Kama ningeambiwa nielezee rangi, basi ningeenda kwenye rangi za rainbow, kwa sababu wewe ni mzuri.ni wa muujiza.


42.Mimi bila wewe  ni  mbaya, lakini ni mzuri nikiwa na wewe.


43.Tukishikana mikono na mioyo yetu inashikana,na nafsi zetu zinapatana .


44.Siku ya kwanza tulipokutana, nilijua ipo siku tutakutana tena, na nafurahi imetokea.


45.Nafurahi tumekua pamoja, sina cha kukosa hata kidogo.


46.Moyo wangu unapumua kama ndege, kila unapotabasamu.

47.Kila ninapokuwa nimeshuka moyo, nikikusikia wewe moyo wangu unapata nguvu.


48.Shika mikono yangu nami nitashika moyo wako, tunza kwa maisha yote.


49.Maisha yote , milele yote,isio na mwisho, toka nimekutana na wewe maneno yote yana maana.

50.Siku naona kama mwaka, na  siku inapita kama sekunde.


51.Natamani ningekuwa  kama pweza mwenye mikono mingi ili nikukumbatie na mikono myote.


52.Siamini katika nafsi mpya, lakini baada ya kukutana na wewe nimeamini, natamani  kama ningeweza kurudi nyuma na kutengeneza kitu.


53.Sitaweza kukutoa kwenye mawazo yangu , kwa maana nakuhitaji uwepo.


54.Kuna wakati nahisi upweke, kwa wakati huo, basi huamua kukupigia simu  na kusikia sauti yako.


55.Ninapokutizama namuona mungu jinsi alivyokuumba na kukubariki.


56.Unanifanya niwe wa muhimu .


57.Ni siri ambayo inanifanya nikutazame  zaidi kwa kila siku.


58.Kuongea na wewe  kila siku unanifanya nikufahamu zaidi na zaidi.

59.Moyo wangu nakupa,nipe moyo wako ili tuifungie kwa pamoja, na tutupe ufunguo mbali.

60.Nakuhitaji muda wote, siku , mwaka na hata milele.

ASANTE SANA KWA KUSOMA MPAKA MWISHO NICHEKI INSTAGRAM KAMA @DAKTARI_ WAMAPENZITZ ILITUWE MARAFIKI NA USHAURI ZAIDI

No comments