HIVI UNAIJUA MAANA YA MAPENZI VIZURI AMA.......???
Mara nyingi watu wengi
hukosea kwa kuchambua mapenzi katika mahaba pekee. Watu wengi hudhania
mapenzi huwa yanahusisha moyo wa binadamu, lakini hakika ni kwamba
huhusisha ubongo wa mwanadamu.
Kuna aina nyingi za
mapenzi ambazo binadamu huonyesha katika maisha yao wanapoendelea na
shughuli zao za kila siku. Kama binadamu sisi husahau aina nyingine za
mapenzi kwani wengi wetu hawajui neno mapenzi lina maana nyingi.
Kwa kufafanua mapenzi yapo na aina zifuatazo
Mapenzi ya kimwili (Eros)
Aina hii ya mapenzi ni
ya kimahaba. Kwa mfano mwanamume kumtamani mwanamke ama vile vile
mwanamke kumtamani mwanamume kwa hamu ya ngono. Hapa mapenzi huwa
yanayoendelezwa na hisia za kumtaka yule mwingine kimapenzi.
Hii ndio aina ambayo
watu wengi duniani hudhani ndio maelezo kamili ya mapenzi ill hali hii
ni moja yapo ya zingine nyingi. Aina hii ya mapenzi ni muhimu kwa watu
wanaoanza kutongozana ama watu wanaofikiri kuwa katika uhusiano.
Mapenzi ya Urafiki (Philia)
Aina hii ni ambayo
inavutiwa na mtu kukufanyia kitendo kizuri ama kukusaidia ama ni mtu
mzuri kwa ujumla. Mapenzi hapa yaweza kuwa kwa ndugu ama rafiki yako
mzuri.
Mapenzi haya huwa sana
ambapo mtu wanashiriki maadili sawa na mwenzake na kwamba hisia zao
sinaambatana ama mmoja anapokea matendo sawia na yale anamwelekezea yule
mwenzake.
Mapenzi ya aina hii
yanaenziwa sana duniani. Wataaluma huamini kwamba mapenzi ya urafiki
husaidia kutoa tamaa ya mwili na kuzingatia kufahamiana zaidi kwa
marafiki na dunia kwa jumla.
Mapenzi ya Familia(Storge)
Aina hii ya mapenzi ni
inayoonekana na wazazi kwa watoto wao na pia kutoka kwa watoto kwa
wazazi. Aina hii hutofautiana na ya urafiki kwani haizingatii kile mtu
anachokutendea bali uhusiano wa kidamu na vile wazazi na watoto wao
wanavyotegemeana.
Sifa za binafsi
hazizingatiwi hapa ili wazazi waonyeshe wanao hisia hizi. Uhusiano wao
huchangia kwa mapenzi haya. Mapenzi haya huhusishwa na mtu kujiskia yuko
huru na salama.
Mapenzi ya Kujitolea(Agape)
Aina hii ya mapenzi
inazingatia asili, mapenzi kwa Mungu au miungu na mapenzi kwa usiowajua.
Hii ni mapenzi ya kujitolea kwa ubinafsi ama mapenzi ya ubinadamu.
Aina hii inahusishwa na
kuto tarajia malipo au kitu chochote kwa matendo unayoyafanya. Yaani ni
mapenzi yakujitolea mhanga. Aina hii ya mapenzi hutusaidia kuwapenda
watu tusiowajua na kusaidiana kibinadamu kwa hali yoyote ile.
Dunia yastahili kuwa na
aina hii kwa wingi ili tukaweza kukaa kwa amani na furaha. Mapenzi kwa
Mungu ama niungu pia huwa katika aina hii. Kumwabudu Mungu aliye binguni
ni mfano mmoja wa kueleza aina hii.
Mapenzi Changamfu (Ludus)
Aina hii ya mapenzi ni
mapenzi yasio na dhamira yoyote na ma mzaha tu. Mapenzi haya hayana
masharti hata kidogo. Mfano wa aina hii ya mapenzi ni kama mtu
anovyomtongoza mwingine, kupinga densi na kucheza.
Aina hii ya mapenzi
haina mambo mengi kwani huwa ni kawaida tu. Aina hii huwa sawa kwa watu
wanaojitosheleza kimaisha. Aina hii ya mapenzi huwa gumu wakati mtu
mmoja hufasiri kwamba mwingine ana hamu ya kimwili. Inafaa watu waweze
kuelewa kama wanahamu zaidi na raha na kufurahi tu.
Mapenzi Madhubuti(Pragma)
Aina hii ni mapenzi
ambayo yako na msingi wa wajibu wako kwa mwingine na wa kuzingatia
maslahi ya mwingine ya siku za usoni. Mfano mwema ni kwa wapenzi ambao
wako katika ndoa.
Aina hii inahusishwa na
uvumulivu na maelewano kati ya walio katika ndoa. Aina hii ya mapenzi
hukuzwa kwa muda wa miaka kadha na ndio maana yaitwa madhubuti ya ka
kudumu.
Mvuto wa kimwili sana hauzingatiwi katika aina hii ya mapenzi bali kujengana kimawazo na kufanya maisha yao kuwa bora zaidi.
Kinyume na aina zingine
za mapenzi mapenzi madhubuti huzingatia pande zote mbili za wapenzi
wawili. Lazima wewe wanapendana ama kuwa na mafikira na dhamira sawia.
Mapenzi ya Kibinafsi (Philautia)
Mapenzi haya ni ya mtu
binafsi. Aina hii ya mapenzi huwa ina matokeo mawili, yaweza kuwa nzuri
ama ya kudhuru. Upande mbaya wa aina hii huwa kwa ile hali ya ubinafi,
kutafuta umaarufu na kutafuta utajiri na hufanya mtu kujiona ana dhamana
kuliko mtu mwingine yeyote.
Upande huu hufanya mtu
akajiona yuko mkubwa kuliko mungu. Pia kuna upande mzuri wa aina hii ya
mapenzi ambao inahusiana na mtu kujijua, kwa kufahamu uwezo wako na
kujidhamini kwa uzuri wako na unachoweza kufanya.
Kwa uhusiano wowote,
huwezi kumpenda mwingine kama wewe mwenyewe hauna mapezi ya kibinafsi.
Kwa kujipenda kwanza ndio tunaweza kupenda wengine na kuwatunza vizuri
maishani. Aina hii ni muhimu sana kwa maisha ya kila mwanadamu.
Mapenzi ya kibinafi
humsaidia mtu kujua mazuri na mabaya na kupanga maisha yake kwa nji
inayostahili. Mapenzi ya kibinafsi humwongezea mtu hali ya kujiamini na
kujidhamini.
Watu waliyo na mapenzi
ya kibinafsi huweza kuelewana sana na watu wengi kwa vile kwa
kujidhamini watu pia hukudhamini. Hii husaidia kwa vile mnaelewana na
watu kazini, nyumbani na mahali pengine ambapo mnapatana.
Watu waliyo na mapenzi
ya kibinafsi hawahitaji kujigamba ili watu wawajue ama kujionyesha kwa
watu. Uzuriwao hujionyesha kwa wanayofanya na wanavyoongea. Watu
wanaojipenda kibinafsi huwa wako huru kwa mambo mapya na uwazi.
Uchambuzi na ufahamu wa
mapenzi ni nini husaidia kila mwanadamu kutambua aina gani anafaa
kuwapa watu kwa kila wakati na aina gani ya mapenzi kutupilia mbali.
Mwanadamu anaweza penda
ila kwa hiari yake. Haina maana lazima mtu akupende ndio umpende nawe.
Kila mwanadamu anauwezo wa kumpenda mwingine ama kitu anachotaka hata
kama yeye mwenyewe hajapatiwa mapenzi hayo.
Lazima kama mwanadamu
kufanya mapenzi kama kitu cha kawaida kwa kila tunachofanya maishani.
Iweke iwe sehemu ya maisha yako na utu wako. Pia ni muhimu kuwa na aina
hizi zote za mapenzi kwa uhusiano kwa kila siku na watu wengine
ilituweze kuishi maisha marefu.
Kama binadamu, mapenzi
ya muhimu sana ni yale ya kujitolea na yale ya kibinafsi. Unapokuwa na
mapenzi yasiyo tarajia kitu chochote na mapenzi yako mwenyewe ndio
utaweza kuwapa watu mapenzi hayo mengine.
Tukiweza kushikilia
aina zote zingine za mapenzi kwa mahusiano yetu basi tutakuwa na maisha
marefu na yenye kufana. Mapenzi ni kitu muhimu maishani na ni sharti
yaenziwe na kila mwanadamu.

No comments