Jinsi Ya Kutongoza Wanawake Wakubwa
Wanawake wakubwa huwa wanakuwa na
ladha tofauti ikija kwa maswala ya mapenzi – ile ambayo wanaonyesha
kupenda wanaume wadogo kiumri. Na kwa sababu wanaume wengi huwa
wanavutiwa na aina hii ya wanawake, bila shaka wanaume hawa hutaka kujua
jinsi ya kuwavutia wanawake wakubwa kiumri. Uzuri ni kuwa uhusiano na
mwanamke aliyekushinda umri siku hizi inaonekana jambo la kawaida.
So, kama unataka kujua jinsi ya kuwatongoza wanawake wakubwa basi hizi mbinu saba zitakusaidia vizuri.
#1 Thamini kile ambacho anakupatia
Kama unataka kujua jinsi ya
kutongoza wanawake wakubwa kiumri, basi unapaswa uthamini kile ambacho
anacho. Kwa lugha nyingine ni kuwa unapaswa kusimamisha fikra zako za
kuangalia miaka yake au mikunjano ya uso wake, na uanze kufikiria mambo
ambayo anaweza kugawa na wewe ikiwemo mapenzi. Wanaume wengi hudhania
kuwa wanawake wadogo ndio huwa na ujuzi ikija na maswala ya mapenzi
lakini huwa si ukweli.
Ijapokuwa ni kweli kuwa kujua
jinsi ya kutongoza wanawake wakubwa kunahitaji mmoja kuzoea, yaani
utahitajika kuthamini na kutambua umri wake, kiujumla; utakuja kujua
baadaemkuwa utakuwa umechukua hatua kubwa katika kudeti wanawake wadogo
na wale wa wasiwasi. Kwa mfano hutapata mwanamke aliyekomaa akikimbia
kwenda msalani ili kuongea na mashoga zake kuhusu deti aliyoko. Hii bila
shaka itakuwa ni mwamko mpya wa kutongoza na pia utaboresha uwezo wako
wa kutumia mistari kiurahisi na haraka.
#2 Mnyeshee heshima
Wakati unapojifundisha jinsi ya
kumtongoza mwanamke mkubwa, weka kwa akili yako kuwa atataka kupewa
heshima zake zaidi ya vile wanawake wadogo utakavyowapatia. Hii ni kwa
sababu ana experience ya juu zaidi ya maisha. Na kwa sababu ambazo
zitategemeana na yeye, mwanamke aina hii anaweza kuwa asiwe huru
kufunguka na kukueleza maisha yake ya zamani ama kukufungukia kuhusu
maisha yake. La muhimu zaidi ni kuwa usimwonyeshe kuwa lengo lako kuu
kwake ni kumuonyesha kuwa unatoka deti na yeye ama una uhusiano wa
kimapenzi na yeye kwa sababu huna jingine la kufanya au umelazimika.
Michezo kama hii haiwezi kufanya kazi kwa mwanamke aina hii – kumbuka
hilo.
#3 Muonyeshe kuwa wewe ni classy, mjanja na usiyesomeka
Kama unataka kujua jinsi ya
kuwatongoza wanawake wakubwa waliokupita umri, basi ni jambo la muhimu
kabisa kuhakikisha kuwa unakuwa mjanja na kuwa na tabia za kukomaa.
Wanawake wakubwa tayari wanaexprerience ya kuwa na deti ambazo zilikuwa
mbaya awali, so kama unataka kumshawishi mwanamke ambaye ni mkubwa wako
kiumri vizuri, basi utahitajika kupandisha gemu yako iwe ya juu.
Kimsingi, wanawake wakubwa
hawatakuwa interested na wanaume wenye nyege ambao wanashindwa
kumaintain gumzo la kawaida mara kwa mara. Badala yake watatafuta
mwanaume ambaye ni gentleman ambaye anaweza kuongea kuhusu mambo ya
kisiasa na yule ambaye anaweza kutofautisha aina aina za duvai ama
angalau yule ambaye anaweza kuchagua sehemu nzuri ya kutoka dinner. So,
kadri unapozidi kuwa mjanja, ndipo inazidi kuwa rahisi kumtongoza
mwanamke aliyekupita kiumri kuweza kuwa na wewe.
#4 Usijionyeshe
Kuonyesha vitu unavyomiliki ama
kuonyesha ujuba wako hakutakusaidia kutongoza wanawake waliokupita umri.
Siku hizi wanawake wanapenda kupata nafasi ya kuonekana kuwa wana
madaraka flani, so mwanamke atapoteza interest na wewe haraka sana kama
utaanza kujidai na kuringa kuhusu idadi ya wanawake ambao umefanya nao
mapenzi ama idadi ya magari unayomiliki. Kama umevalia suti ya
kushonesha ama una Mercedes ya gharama si lazima umwambie kuvihusu kwani
atajionea yeye mwenyewe. Badala yake msifu na kumpongeza kwa mambo
aliyofanikiwa kufanya. Hii ni njia rahisi ya kuweza kuwatongoza wanawake
waliokupita kiumri na wakakukubali kirahisi.
#5 Jiamini
Njia nyingine rahisi ya kutongoza
mwanamke aliyekupita umri ni kwa kuonyesha kuwa unajiamini kwa kila
kitu unafanya au kuzungumza. Wanawake aina hii huwa kwa kawaida
wanapenda wanaume ambao wanauwezo wa kutatua tatizo lolote ambalo
watarushiwa usoni mwao. So, kama wewe ni mwanaume ambaye hujafikia
kiwango cha kujiamini , basi ni wakati wako wa kuchukua hatua ya
kuhakikisha ya kuwa unajenga ujiaminifu wa kuweza kuongea na wanawake.
Unaweza kujifundisha kuhusu biashara, sanaa na mambo ya kisasa, silaha
ambayo unaweza kuitumia iwapo mwanamke aina hii atazua mjadala akiongea
kuhusu swala kama hili. Wanaume ambao wanaelewa kile ambacho wanaongea
huwa wanakuwa na confidence zaidi mbele ya wanawake. Pia wanaonyesha
utawala ikija kwa maswala ya mahusiano. Kama unataka kuwa bingwa katika
kutongoza wanawake waliokupita umri, basi confidence itakuwa ni silaha
kubwa katika mpango mzima.
#6 Yaweke mapenzi yawe ya hali ya juu
Kama unataka kumshawishi mwanamke
aliyekushinda kimiaka vizuri, unafaa kuhakikisha kuwa unaweka mapenzi
yawe juu. Hii inamaanisha kuwa, ijapokuwa hatakuwa na tabia za kama
wanawake walio wadogo, unapaswa humchukulia kama mwanamke mdogo.
Mnunulie chokoleti, maua na zawadi ndogo ndogo mara moja au nyingine.
Msifu wakati amevalia nguo nzuri ama anapopendeza mnapotoka out. Mambo
haya madogo madogo ambayo unamsifia mwanamke yatamfanya mwanamke kuwa na
furaha na atapendezwa na wewe.
#7 Usitaje kuhusu utofauti wa miaka yenu
Na lile jambo muhimu la
kuzingatia wakati wa kujifunza kutongoza wanawake waliokupita umri ni:
kutotaja tofauti ya miaka yenu. Hata kama haujiskii huru na kuwa na yeye
mara ya kwanza, hupaswi kuzungumzia swala hili. Ama unaweza kuharibu
nafasi yako ya kumtongoza. Badala yake makinika na mambo ambayo
yanahusiana nyote wawili, kama vile kuongea kuhusu mambo mnayopenda au
kuongea kuhusu filamu. Pia unaweza kuingiza ucheshi katika mazungumzo
yenu; hii hufanya kazi nzuri kwa mwanamke.
So hizi ndizo mbinu unapaswa kuzijua ikija na maswala ya kutongoza mwanamke ambaye amekushinda kiumri. Upo!
No comments