KAMA UMETEMBEA NA RAFIKI AKE AKAJUA TEGEMEA HAYA
Mwanaume anaweza kukusamehe kitu
chochote kile, anaweza asijali kuwa ulichepuka hasa kama yeye labda
ndiyo alikuwa sababu ya wewe kuchepuka lakini pale utakapochepuka na
marafiki zake itakuwa ni ngumu sana kwake kukusamehe. Ni wanaume
wachache sana ambao unaweza kutembea na rafiki zake na akakusamehe.
Tofauti na wanawake ambao
mwanamke anaweza kumnyanganya rafiki yake mwanaume au akamfumania rafiki
yake na mpenzi wake kisha akamsamehe mpenzi wake na kugombana na
rafiki, kwa wanaume si hivyo. Wanaume wana pride, yaani ile hali ya
kujiona bora na kutaka kuheshimiwa. Wana uanaume ndani yao ambao
unaondoleka pale anapokufumania na rafiki yake.
Unapotembea na rafiki wa mume au
mpenzi wako haiishii pale tu anapokufumania na labda kukusamehe lakini
itaenda mbali kwa mwanaume kujisikia vibaya. Kila akikutana na yule
rafiki yake na wakiongea chochote akili yake itawaza “Huyu jamaa kagonga
mke wangu, anajua kila kitu kwa mke wangu…” Hiyo itamuumiza sana na
kumfanya kukuchukia kila mara.
Anaweza kukusamehe kwakuwa
anakupenda sana lakini mbele ya yule rafiki yake atajiona mnyonge na
itakuwa ngumu sana kusahau. Kwa wanaume wengi hakuna kitu kinachokera
kama kukutana na mwanaume mwingine ambaye anajua kila kitu kuhusu mkewe.
Nikama wanaambiwa “Utaniambia nini wewe mkeo mwenyewe yuko hivi na
vile!”
Lakini haiishii hapo, karibu kila
mwanaume anaamini kuwa ukishatembea na mwanamke mara moja basi hana
thamani tena na hata mkiachana bila kujali sababu za kuachana kwenu
akikomaa sana anaweza kumrudia yule mwanamke au hata kupata mechi. Kwa
maana hiyo basi akijua umempa rafiki yake kila siku atakua na wasiwasi
kuwa anaweza kuchapiwa tena.
Hata akikuona unaongea tu au
unapita maeneo yale, ukimtaja tu au kumzungumzia ataumia. Ningumu sana
kwa mwanaume kusamehe kitu cha namna hiyo. kwa maana hiyo basi kama
unampenda kweli epuka na kaa mbali kabisa na marafiki zake. Hata kama
yeye kakusaliti kwa rafiki yako lakini kama bado unataka kumrudia
usilipe kisasi kwa kumchukua rafiki yake.
Pia usijidanganye kua hatajua,
duniani hakuna siri na ipo siku huyo rafiki yake atamuambia rafiki
mwingine na meingine na hatimaye ikamfikia. Unaweza kutembea na rafiki
wa mume wako leo lakini akaja kujua baada ya miaka kumi na akakuacha
kwani kwake itauma kama ndiyo umefanya siku hiyo hiyo, ndiyo akili za
wanaume zinavyofanya kazi hivyo kuwa makini.
Ataanza kukumbuka namna mlivyokua
mnaongea, namna rafiki yake alivyokua anakusifia, namna alivyokuwa
namkuta nyumbani na mambo mengine ambayo rafiki yake alikua anayafanya
na kipindi hicho hakua na mashaka ila miaka kumi baadaye anakua na
mashaka na hata ukimuambia ilikuwa kabla ya ndoa hatakuelewa.

No comments