KAMA UNA MOYO MWEPESI USISOME STORY HII, WENGI WAMELIA SANA
Kama nilivyoanza mwanzo....usisome kama una machozi ya karibu...
“Nilipofika nyumbani usiku ule,
mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna
kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya
akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha
anaumizwa.
Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.
Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi.

Nilifahamu kwamba alitaka kujua
ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa
jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi
langu lilihamia kwa Mary. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa
kwa Mary.
Kwa kweli nilimdharau mke wangu!
Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu.
Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu.
Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.
Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Mary aliuteka moyo wangu kisawasawa.

Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.
Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.
Siku iliyofuata nilikuja nyumbani
kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani.
Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja
chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka
baada ya kula raha za kufa mtu na Mary
Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika.
Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika.
Sikujali kabisa nikajifunika
vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka
yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate
angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika
kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi
maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana.
Sababu yake ilikuwa ndogo lakini
muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi
uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya
kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake.
Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi
nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu.
Akaniomba na kunisihi kwamba
katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu
mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa.
Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na
masharti yake ya ajabu.
Nilimsimulia Mary kuhusu masharti
ya kuachana na mke wangu. Mary alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata
akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Mary tena kwa
dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza
dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote
tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah
baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja
kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka
mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na
kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka.
Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya.
Nilimuweka chini nje ya nyumba.
Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.

Siku ya nne nilipombeba hisia za
mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na
tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi
kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Mary kuhusu jambo
hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu
na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku
kuliniimarisha zaidi.
Alikuwa akichagua nini cha kuvaa
asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna,
‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua
sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo
likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila
kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema
‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba
akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha
ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza
uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha
nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka
mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo.
Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu.
Lakini wepesi wake ulinitia mashaka.
Siku ya mwisho nilipombeba
nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni.
Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa
upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga
mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua....
nikapand ngazi. Mary alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Mary,
sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu
akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake
kichwani kwangu. ‘Samahani, Mary, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu.
Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa
maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo
tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za
maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo
kitakapotutenganisha.’
Ikawa kama Mary alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenga
nisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.

Kumbe mke wangu alikuwa
akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa
sababu nilihamishia akili yangu kwa Mary. Alijua kwamba angekufa
karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama
ningelazimisha talaka mapema.
Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema.
Mungu nisaidie Nisifike huku mimi.
Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema.
Mungu nisaidie Nisifike huku mimi.
Kama Stori Hii Imekugusa Na Ungependa Marafiki Nao Waisome Basi Unaweza KuSHARE.
No comments