Kwa wanawake tu; Fanya haya kumchizisha Mpenzi wako kitandani
Mtaalam wa mapenzi, Bi. Layla Quinn, anasema wamaume ni viumbe rahisi
sana kuridhishwa tunapokuja katika suala la unyumba. Mwanzoni, kitu
kinachomhamasisha mwanaume kujamiiana ni muonekano wako (mwanamke) tu
wakimahaba, lakini kadri siku zinavyokwenda ndani ya mahusiano, inakuwa
ngumu kupandisha munkari wake, hata kama wewe ni mwanamke mrembo
barabara!
Bi. Layla anaendelea kusema kuwa, kumridhisha mwanaume wako kitandani
inaweza ikawa rahisi kama tu utakumbuka kuweka mambo katika hali ya
mvuto ( Remember to keep things intereting!). Tafuta namna ya kuleta
hamasa, iliyokuwepo siku za mwanzo mwanzo, na kwa hakika utakamata
usukani. Sasa swali linakuja…..Nini unatakiwa kufanya, ili kumridhisha
mwanaume wako kitandani? Kujibu swali hilo, Bi. Layla amekuja na sheria
10 zifuatazo, ambazo kama zitazingatiwa kwa makini, basi mwanamke
hatokuwa na shida ya kumridhisha mwanaume wake kitandani na nyanja
nyingine muhimu za mahaba.
# 1 Vaa vizuri. Utamu wa kujamiiana unaweza ukawa kwenye tendo lenyewe,
lakini matamanio ya kufanya tendo hilo, yanategemeana na mambo mengine
mengi. Vaa vizuri wakati wa kulala wakati wote, na sio tu wakati wa
usiku, ambao unataka kufanya mapenzi. Vaa nguo nyororo, yenye mtelezo
unaomwagika mwilini. Kwa vazi hili na mtembeo wa kimahaba chumbani,
mwanaume wako hatotaka kutoa mikono yake mwilini mwako.
#2 Usiwe mtu wa aibu aibu linapokuja suala la kujamiiana. Mwaume anaweza
akakupenda kwa mapozi yako na aibu kwanza (lugha iliyotumika hapa ni
“innocence”), lakini hamna mwanaume atakaye endelea kuvumilia mwanamke,
ambaye anastushwa kirahisi na kila kitu (mitindo ya kujamiiana),
isipokuwa mtindo wa kifudi fudi, maarufu kama “Kifo cha Mende”. Wanaume
wanapenda wanawake, ambao ni wataalam kitandani. Wanaume wanapenda
wanawake, ambao wanajiamini na wanabuni manjonjo mbalimbali wakati wa
shughuli. Kama unataka kumridhisha mwanaume wako kitandani, basi soma
mbinu mbalimbali, ambazo zinatumiwa na wapenzi mbalimbali.
#3 Fanya mazoezi na onekana Bomba. Wanaume ni watu wakujali sana
muonekano wa mwanamke. Kwahiyo, sio lazima kuonekana kama walimbwende wa
vichupi, lakini mtazamo wa karibu na hapo, utakuongezea mvuto zaidi
kitandani. Ndio, mwanaume wako “anakupenda kama ulivyo” na tila lila
nyingiiiii…..lakini lazima tuukabili ukweli kwamba watu wenye kufanya
mazoezi wanaonekana na mvuto zaidi, hakuna kupinga hilo. Hata kwetu
Bongo katika nyakati hizi za utandawazi, wakina kaka wengi wanawaona
wanawake kama wakina Naomi Campbell na Jennifer Lopez, ambao wanatamani
kuwa nao. Lakini hauhitaji kuwa kama wakina Naomi na Jennifer
kumridhisha mwanaume wako, bali hakikisha tu upo katika umbo zuri la
kumpelekesha kirahisi kitandani, Basi!
#4 Kuwa Mchokozi. Hapa haimaanishi ule uchokozi wa kuleta ugomvi,
lahasha! Bali, ni ule uchokozi, ambao kwa lugha ya kingereza unafahamika
kama “Tease”, kwa maana hiyo basi tunasema “Tease him”. Cheza nae
michezo mbalimbali na burudika nae ipasavyo, na michezo isiwe ya
kitandani tu, kama karata na kadhalika, bali michezo ya hata nje ya
kitanda kama kukimbia na kucheza kidali po! Kama unataka kuwa mjuzi
kitandani, basi unatakiwa umfanye mwanaume wako akutake wakati wote na
popote pia. Kujamiiana sio kitasa ambazo unawasha na kuzima mnapokuwa
chumbani tu. Mchokoze chokoze wakati mnasakata muziki jukwaani, na
mchokoze chokoze (katika mitindo ya kimahaba, bila kuvuka mipaka) wakati yupo na marafiki zake.
#5 Jiamini na Jipende. Ndio, utaonekana vizuri zaidi ukipunguza maunene,
lakini hiyo haimaanishi kwamba haupo bomba. Hakuna kinacho kera
wanaume, kama mwanamke, ambae anauonea aibu mwili wake mwenyewe wakati
anafanya mapenzi. Jiamini kuhusu mwili wako wakati upo mtupu, na jaribu mambo mbalimbali na mwanaume wako.
No comments