Mafuta ya habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo
Inapotokea wafalme wa Misri, Malkia wa Ulaya, Mitume na wanasayansi wa
kisasa wanakuja na kukubaliana katika jambo moja, ni mhimu kudadisi juu
ya jambo hilo.
Ingawa nyakati za sasa tunazungukwa na taarifa na elimu nyingi kuliko
katika wakati mwingine wowote, bado tunahitaji kujifunza vitu kutokana
na historia na maisha ya kale.
Kutoka kwa baba wa sayansi ya matibabu katika nchi za magharibi Hippocrates kwenda mpaka kwa kiongozi wa mfumo wa mwisho wa kifarao Cleopatra hadi kwa mfalme Tut na
jamii iliyofuata, kitu cha pekee ambacho walikuwa wakifanana viongozi
hawa kwa pamoja ilikuwa ni thamani waliyoiona katika mtishamba fulani.
Mtishamba au mmea huo ambao viongozi hao walikutana pamoja si mwingine bali ni habbat soda. Habbat soda ndilo jina linalotumika zaidi mashariki ya kati na huko ulaya hujulikana zaidi kama ‘black seeds’.
Kwahiyo niliamua kuchukua muda kusoma na kupeleleza zaidi kuhusu habbat
soda kwa ajili yangu mwenyewe na ya wasomaji wangu ili hatimaye niweze
kukuletea mwanga kamili juu ya mengi yanayosemwa kuhusu mafuta ya habbat soda.
Unaweza kuwa umesikia majina tofauti tofauti ya habbat soda kutegemea na sehemu gani ya dunia ulipo.
Haya ni moja ya majina yake:
- Kalonji Oil
- Black Cumin Seed Oil
- Nigella Seeds
- Graine De Nigelle
- Black Onion Seeds
- Schwarzkummel
Mafuta ya habbat soda yanatokana na mbegu za habbat soda na mbegu hizi huwa ni nyeusi na ndiyo maana kwa kiingereza wanaita ‘black seed’.
Kuna mashine nyingi za nyumbani unazoweza kutumia kutengeneza mafuta
yako mwenyewe kutoka katika mbegu za habbat soda ingawa bado nakushauri
ununuwe yale ambayo yameandaliwa tayari.
Habbat soda ina sifa hizi:
- Huondoa bakteria mwilini
- Huondoa uvimbe
- Huondoa sumu mwilini
- Inaondoa fangasi
- Inatibu kansa
- Inatibu pumu
- Inadhibiti kazi za histamini
- Inaua virusi
- Inazuia damu kuganda
Vitu viwili mhimu zaidi ambavyo mafuta haya yanavyo ni ‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’.
Vimeng’enya hivi viwili ndivyo vinaweza kusemwa kuwa ndiyo sababu ya mafuta haya kuwa ni dawa kwa kila ugonjwa. Vinaimarisha moja kwa moja kinga yako ya mwili na kuifanya ipatikane wakati wowote itakapohitajika na mwili.
Vimeng’enya hivi viwili ndivyo inaaminika ndiyo sababu mfalme Tut alipatikana na chupa ya mafuta ya habbat soda kwenye kaburi lake akitumaini kuyachukua na kuyatumia atakapofufuka!
Mtume Muhammad (S.A.W) amewahi kunukuliwa akisema ‘Mafuta ya habbat soda ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo’
Mbegu za habbat soda zinatoka katika majani ya mmea ujulikanao kama ‘Nigella
Sativa’ na unalimwa karibu katika kila pembe ya dunia kwa sasa. Asili
yake ni Afrika kaskazini, mediterania/ulaya na Asia na kutoka hapo
umesambaa kila sehemu ya dunia.
Habbat soda inachukuliwa kama moja ya dawa za asili bora zaidi kuwahi kutokea.
Nini yanachoweza kufanya mwilini haya mafuta ya habbat soda? kuna matumizi mengi ya habbat soda katika kutibu na kukinga magonjwa mbalimbali.
Nini yanachoweza kufanya mwilini haya mafuta ya habbat soda? kuna matumizi mengi ya habbat soda katika kutibu na kukinga magonjwa mbalimbali.
Hapa nimejaribu kukusanya baadhi ya magonjwa 89 ambayo unaweza kujitibu kwa kutumia habbat soda.
Kama kawaida unapewa angalizo kutotumia dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa daktari
Magonjwa 89 yanayoweza kutibika na habbat soda ni pamoja na:
1. Yanaimarisha afya ya moyo
Afya mbovu ya moyo inaweza kuwa ni matokeo ya sababu nyingi lakini
sababu zote chanzo chake kikuu ni matokeo ya kutokuupa moyo virutubishi
unavyovihitaji.
Mafuta ya habbat soda yana asidi mafuta safi na yenye Omega 6 na 9, pia
yana kirutubishi kingine mhimu zaidi kijulikanacho kama “phytosterols”
ambacho husaidia kulazimisha kusinyaa na kutanuka kwa mishipa ya damu
na hivyo kusaidia kuzuia damu kuganda na kujikaza katika ateri.
Viinilishe hivi pia husaidia kushusha lehemu kwenye damu na kiasi cha damu sukari.
Kwa karne nyingi mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu matatizo mengi yanayohusiana na moyo.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja mpaka miwili
2. Hupigana na maambukizi ya fangasi
Maambukizi ya fangasi yanatokea wakati bakteria wanapozidi juu ya ngozi
yako na kupelekea kutokea kwa magonjwa mengi ikiwemo miwasho, upele na
ukurutu.
Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni mazuri kwa tiba karibu kwa
kila aina ya fangasi kitu kinachopelekea wanasayansi wengi kuamini kuwa
habbat soda ni dawa ya asili na mbadala mhimu zaidi kwa kila mtu kuwa
nayo nyumbani.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha
mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja. Mengine pakaa kama
mafuta yako ya kupakaa sehemu yenye muwasho kutwa mara 2 hadi 3.
3. Hudhibiti Aleji (mzio)
Wengi wetu tunapatwa na aleji na kutokewa na chafya au mafua yasiyoisha
na kupelekea kushuka kwa kinga yetu ya mwili. Kutumia mafuta asili ya
habbat soda kwa ajili ya kutibu aleji kunaweza kuleta matokeo mazuri
bila gharama kubwa.
Na siyo kwamba mafuta haya yatakupa nafuu kwa haraka sana dhidi ya aleji
tu, bali pia yatakufanya kujisikia nafuu haraka zaidi kuliko dawa
nyingine nyingi za kutibu aleji za viwandani zilizopo sokoni leo.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja mpaka miwili.
4. Ni mafuta mazuri kwa ajili ya ngozi yako
Iwe ni muonekano au afya ya ngozi kwa ujumla, ipo sababu kwanini watu wanapenda kuwa na ngozi ya kupendeza na yenye afya.
Mafuta ya habbat soda yana asidi mafuta mhimu zaidi, yana vitamini
nyingi, yana viondoa sumu vya kutosha na asidi amino mhimu ambazo miili
yetu huzihitaji.
Mafuta ya habbat soda ni mafuta safi ya ngozi kwa nyakati zote za siku
na kwa siku zote. Mafuta haya pia yanasaidia ngozi kutokuungua moja kwa
moja na miale ya jua huku yakizuia usizeeke haraka kwa kuondoa mikunjo
yoyote kwenye ngozi yako.
Matumizi: Yawe ndiyo mafuta yako ya kupakaa mwilini kila siku
5. Hutibu kansa ya ngozi (Melanoma)
Kansa ni matokeo ya kinasaba cha damu (DNA) kujizidisha au kujizalisha
mara nyingi na kwa haraka zaidi dhidi ya uwezo wa kinga ya mwili. Mara
nyingi kansa hutokeza vivimbe sehemu mbalimbali mwilini.
Mafuta ya habbat soda yana virutubishi vingine viwili ambavyo ni
‘thymoquinone’ na ‘thymohydroquinone’ ambavyo utafiti unaonyesha huwa
vina uwezo wa kudhibiti kansa kwenye ngozi na kansa nyingine mbalimbali
mwilini.
Hii ni kutokana na sifa yake ya haya mafuta katika kuzuia uvimbe na bakteria, sifa kuu mbili za habbat soda.
Habbat soda hufanya hivyo kwa kuzilenga seli zako nyeupe za damu kwa kuziongezea kinga ya mwili na hivyo kuua seli za kansa.
Matumizi: Yawe ndiyo mafuta yako ya kupakaa mwilini kila siku.
6. Hutibu chunusi
Chunusi ni matokeo ya moja kwa moja ya vivimbe kwenye ngozi hasa ya paji la uso na usoni kwa ujumla.
Mafuta haya yanaondoa uvimbe wa aina yoyote kwenye ngozi na kuitengeneza
upya ngozi huku yakiiacha nyororo na muonekano wake wa asili.
Mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kwa ajili hii ya kutunza na
kutibu maradhi mbalimbali ya ngozi na wafalme na malkia wengi katika
historia yote ya dunia.
Matumizi: Yawe ndiyo mafuta yako ya kupakaa mwilini kila siku. Unaweza pia kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku kusafisha mwili ndani
7. Hutibu maambukizi
Maambukizi ya aina yote hupigwa na kinga ya mwili hasa na seli nyeupe za damu ndizo zinazohusika na kazi hiyo.
Kwa kuiongezea nguvu kinga ya mwili moja kwa moja, mafuta ya habbat soda
yanausaidia mwili wako kupigana na maambukizi kutoka kwenye nywele
kichani mpaka kwenye kucha.
Hii ni sifa ya pekee ya habbat soda ambayo imekuwa ikijulikana kuwa nayo
katika historia yote ya dunia tangu enzi hata leo bado ni moja ya dawa
za asili zenye nguvu ya kupigana na maambukizi ya aina nyingi ya mwili.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja mpaka miwili
8. Hutibu tatizo la ugumba
Ugumba unaweza kutokea kutokana na sababu nyingine nyingi, ingawa
imethibitishwa pasipo na shaka kwamba mafuta ya habbat soda yamewasaidia
wengi kuimarisha afya zao za uzazi.
Kwa wale wote wenye tatizo la uzazi au ugumba tambueni kuwa mafuta ya
habbat soda yamekuwa yakitumika kutibu matatizo ya ugumba kwa zaidi ya
miaka 2000 sasa.
Mpaka leo bado mafuta ya habbat soda yanaendelea kuripotiwa kama ndiyo
dawa bora zaidi ya asili kwa ajili ya kurekebisha tatizo la ugumba kwa
watu wa jinsia zote mbili.
Wakati huo huo mafuta ya asili ya habbat soda yamethibitika kuwa dawa
bora zaidi ya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake na hutibu
tatizo la nguvu za kiume hata kama mwanaume utakuwa na umri wa miaka
120. Unachohitaji ni kuyatumia kwa kipindi kirefu hata miezi miwili au
hata zaidi mfululizo kama tatizo limekuwa sugu sana.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku kwa mwezi mmoja mpaka mitatu.
9. Huotesha nywele
Moja ya matumizi makubwa ya mafuta haya ni kuotesha nywele. Bidhaa
nyingi sokoni zinazotumika kwa ajili ya kuotesha nywele zinaacha madhara
makubwa zaidi kwa mtumiaji kuliko faida zake.
Kwahiyo kwa wale wenye tatizo la upala, nywele zisizokuwa na kwa wale
ambao nywele zao hazina afya mnashauriwa kuchagua mafuta haya kwa
matatizo haya yote.
Ingawa haieleweki ni kwa namna gani mafuta haya yanakuza nywele lakini
wanasayansi wanaamini haya yanaweza kuwa ni matokeo ya uwezo wake mkubwa
wa kuondoa sumu na protini nyingi ndani yake.
Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya nywele yenyewe ni meusi kabisa kabisa
na huwa mazito kidogo tofauti na yale ya kunywa na kupakaa mwilini.
Matumizi: Sugulia kipande cha limao fresh eneo ambalo
nywele zimenyonyoka na kisha pakaa kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya
habbat soda ya nywele na uache kama dakika 15 hadi 20, unaweza kuacha
hivyo hivyo au ujisafishe na maji safi, unaweza kufanya kutwa mara 1 au 2
kwa mwezi mmoja hadi miwili
10. Hutibu mafua na homa
Mafua na homa ni matokeo ya kushuka kwa kinga ya mwili na kadri
unavyoendelea kuyavumilia magonjwa kama haya ndivyo unavyozidi
kuidhoofisha zaidi kinga yako ya mwili.
Kama tulivyoona kabla kuwa mafuta ya habbat soda huongeza kwa haraka
sana kinga ya mwili, huondoa haraka sumu mwilini na bakteria mbalimbali
na hivyo kufanya kuwa ndiyo dawa nzuri ya asili dhidi ya mafua na homa
za mara kwa mara.
Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta haya na vijiko vitatu vikubwa
vya asali changanya katika glasi moja (ml 250) ya maji ya uvuguvugu na
unywe kutwa mara moja kila siku.
Kitendo hiki hakitakuondolea mafua na homa pekee bali pia kitaimarisha afya yako kwa ujumla. Fanya kwa siku 7 hadi 14
11. Hutibu majipu
Liwe ni jipu moja au majipu mengi kwa pamoja, mafuta ya habbat soda
ndiyo dawa nzuri kukupatia nafuu ya haraka. Hii ni kwa sababu kwa sehemu
kubwa majipu ni matokeo ya maambukizi ya bakteria na mchafuko wa damu.
Na mafuta ya habbat soda ni wakala mzuri wa kuondoa bakteria na kusafisha damu na hivyo kuwezesha majipu kuwa chini ya ulinzi.
Unaweza kupakaa mafuta haya juu ya jipu moja kwa moja na wakati huo huo
mengine unywe kama ilivyoelezwa kwenye namba 9 hapo juu. Hata hivyo
ikiwa jipu ni kubwa sana na huoni nafuu hata baada ya kujaribu mafuta
haya muone daktari kwa msaada zaidi.
12. Hutibu kikohozi na Pumu
Ile sifa yake kuu ya kuondoa vivimbe kwenye tyubu za koo, kitendo chake
cha kuongeza kinga ya mwili, kuua bakteria na virusi ndiyo sababu za
mafuta haya kutumika kutibu kikohozi na pumu.
Imeandikwa katika historia kuwa mababu wa zamani wa Misri walikuwa
wakitumia mafuta ya habbat soda hasa kwa ajili ya kuimarisha afya ya
mfumo mzima wa upumuwaji.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa wiki 3 hadi 4 hivi
13. Hutibu kuharisha
Mara nyingi kuharisha ni matokeo ya maambukizi ya virusi na bakteria na
kama tulivyoona mafuta ya habbat soda hudhibiti bakteria na virusi
mbalimbali mwilini na hivyo kufanya ndiyo dawa nzuri mbadala kwa ajili
ya kutibu au kuzuia kuharisha.
Huweka sawa mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na tumbo kwa ujumla na hivyo kuzuia mwili wako kupatwa na tatizo la kufunga choo.
Inashauriwa kuchanganya kijiko kidogo kimoja cha chai au viwili vya
mafuta ya habbat soda na kikombe kimoja cha mtindi na utumie asubuhi na
usiku kwa siku mbili hivi na kuharisha kutasimama.
14. Hutibu shinikizo la juu la damu
Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya shinikizo la juu la damu ni moja kati ya matumizi makubwa ya mafuta haya kwa sasa.
Ingawa haijathibitishwa rasmi kama dawa ya kutibu shinikizo la juu la
damu lakini wagonjwa wengi wa shinikizo la juu la damu wameripoti
kushuka kwa kiwango kikubwa cha mashinikizo yao ya damu wakati
wanapotumia mafuta haya ya habbat soda.
Tafiti kama hizi zimepelekea wengi kuanza kutumia mafuta ya habbat soda kama dawa ya asili kwa ajili kutibu shinikizo la juu la damu.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa wiki 3 hadi mwezi mmoja.
Pia hakikisha unakuwa na uzito sawa kulingana na urefu wako. BP ya juu
inaweza kuchelewa kupona ikiwa uzito wako upo juu ya inavyotakiwa uwe
nao.
15. Huondoa tatizo la kukosa usingizi
Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni dawa nzuri ya asili dhidi ya
tatizo la kukosa usingizi na matatizo mengine kama hayo ya kuvuruga
utulivu wa usingizi kwa ujumla. Watu wengi wameripoti kupata usingizi
mororo na utulivu kwa ujumla kwa kutumia habbat soda.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.
16. Huzuia mishtuko na kukakamaa kwa mishipa
Mafuta ya habbat soda ni dawa nzuri ya kuzuia kukakamaa na mishtuko
mbalimbali kwenye mishipa. Unaweza kuyanywa mdomoni au unaweza kupakaa
na kuchua moja kwa moja sehemu ya mishipa yenye matatizo kwa ajili ya
matokeo mazuri ya haraka.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa
mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa. Pakaa na ujichuwe pia sehemu ya
mishipa yenye matatizo
17. Huondoa kichefuchefu na mvurugiko wa tumbo
Mafuta ya habbat soda kwa ajili ya kuondoa kichefuchefu na kuvurugika wa tumbo ni moja ya sifa nyingine kubwa ya mafuta haya.
Uwezo wa mafuta haya kutibu haya matatizo mawili unatokana na nguvu yake
kuhamasisha vimeng’enya vyakula vya mwili wako na kuondoa gesi tumboni.
Matumizi: Kwa ajili ya kuondoa kichefuchefu changanya
kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya habbat soda na glasi moja ya juisi ya
tangawizi na unywe glasi moja asubuhi na nyingine jioni kila siku kwa
siku mbili tatu.
18. Dawa bora kwa matatizo ya meno
Dawa nyingine nzuri kwa matatizo ya meno kama jino kuuma, kuoza, kutoboka, kulegea nk ni mafuta ya asili ya habbat soda.
Kuondoa maumivu ya jino unachohitaji kufanya ni kunyunyiza matone kadhaa
ya mafuta haya juu ya hilo jino na utulie tuli kama dakika mbili hivi
kutwa mara mbili.
19. Huua seli za kansa ya damu
Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda yanacho kitu mhimu sana
kiitwacho kwa kitaalamu kama “thymoquinone” ambacho huziua seli za kansa
ya damu (leukemia HL-60 cells).
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
20. Hutibu saratani ya matiti
Mafuta ya habbat soda yana uwezo wa kuzuia seli za saratani ya titi
kuendelea kujizalisha na inashauriwa kwa ajili ya kutibu saratani ya
titi yatumike kwa kipindi kirefu miezi hata miwili au zaidi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
21. Hutibu saratani ya utumbo mpana
Kimeng’enya kiitwacho ‘thymoquinone’ kilichomo kwenye
mafuta ya habbat soda na sifa yake kubwa ya kuondoa sumu ndivyo vitu
viwili vinavyoyawezesha mafuta ya habbat soda kuzishambulia na kuziua
seli za saratani ya utumbo mpana (colon cancer).
Yanabaki kuwa ndiyo dawa mbadala bora zaidi kwa saratani ya utumbo mpana inayosumbua watu wengi miaka ya karibuni.
Habbat soda si dawa ya magonjwa mengine mengi tu bali pia ni moja ya
vitu mhimu sana katika kuzuia kukua, kujizidisha au kujizalisha upya kwa
seli mbalimbali za kansa.
Uwezo wa mafuta ya habbat soda kudhibiti uongezekaji wa seli za kansa
unashawishi sana kiasi kwamba madaktari wengi wamekiri kuwa ni dawa moja
bora sana mbadala dhidi ya saratani ya kwenye utumbo mpana.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku mpaka upone
22. Hutibu fangasi ya ngozi na mapunye
Fangasi, mapunye, ukurutu na magonjwa mengi ya ngozi yanaweza kutibika
kwa kutumia mafuta ya habbat soda. Fangasi na mapunye ni tatizo
linalowapata watu wengi karibu kila sehemu katika nchi tajiri hata
katika nchi maskini pia.
Unaweza kuyanywa mdomoni na wakati huo huo ukapaka moja kwa moja juu ya
ngozi sehemu yenye tatizo kwa majuma kadhaa. Kama ni kunywa basi kunywa
kijiko kidogo kimoja cha chai kila siku mpaka upone
23. Husaidia kupunguza uzito
Uwezo wa mafuta ya habbat soda kushusha uzito unatokana na sifa yake ya
kuweza kupunguza sukari katika damu. Zaidi ya kuwa ni wakala muondoa
sumu mwilini wa asili, mafuta ya habbat soda husaidia pia kuongeza nguvu
katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kupunguza kiasi chako cha
njaa.
Hii ya kudhibiti kiasi cha njaa ni mhimu sana hasa wakati unataka kudhibiti mfumo wa vyakula unavyokula.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa
mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa, usisahau pia kufanya mazoezi ya
kukimbia (jogging kila siku)
24. Hutibu Kisukari
Kitu gani kimeyafanya mafuta ya habbat soda kuwa ndiyo dawa nzuri ya
asili dhidi ya Kisukari? Ni ule uwezo wake mkubwa wa kushusha shinikizo
la damu na kusaidia wagonjwa wa Kisukari wote ambao ni tegemezi au si
wategemezi wa insulin.
Ni dawa nzuri kwa watu wote wenye kisukari aina ya kwanza na kisukari
aina ya pili kwa wakati mmoja. Pia huboresha kwa ujumla AFYA ya damu
yako.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 2 kila siku kwa mwezi mmoja hadi miwili
25. Hutibu kifafa na mishtuko ya moyo
Dawa nyingi za kisasa zinazotumika kutibu kifafa na mishtuko ya moyo
huwa zina orodha ndefu ya madhara mabaya (negative side effects) pia.
Bahati nzuri kwa upande wako wewe unayesoma makala hii ni kuwa mafuta ya
asili ya habbat soda (black seed oil) ni dawa nzuri ya kutuliza kifafa
na matokeo yaletwayo na kifafa.
Baadhi ya tafiti zimeonyesha watu wenye kifafa na mishtuko ya moyo
waliacha kuonyesha tabia au dalili za kifafa au mishtuko ya moyo
walipotumia mafuta ya habbat soda kwa wiki 4 hadi 6 huku wakitumia
sambamba na dawa walizopewa hospitalini.
Watafiti wengi wanasema hii ni kutokana na kiinilishe mhimu kilichomo kwenye mafuta haya kijulikanacho kama ‘thymoquinione’.
Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku mpaka upone.
26. Hutibu vidonda vya kooni
Mafuta ya habbat soda yamethibitishwa kutibu vidonda vya kooni (tonsils)
na kuondoa kila aina ya maumivu kooni na kuondoa uhitaji wa dawa za
kuondoa maumivu (pain killers).
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
27. Hutibu kidonda ndugu (MRSA)
Kidonda ndugu au kama kinavyojulikana kwa kitaalamu kama ‘Methicillin
resistant Staphylococcus aureus (MSRA)’ ni ugonjwa unaoendelea
kuwasumbua wataalamu wengi katika mahospitali maeneo mengi duniani.
Mara nyingi hutokea kama matokeo ya kudhoofika kwa kinga ya mwili. Uwezo
wa kuondoa uvimbe na sumu wa mafuta haya unayafanya kuwa dawa mbadala
yenye ufanisi zaidi katika kutibu kidonda ndugu.
Mafuta ya habbat soda yatakusaidia kutibu kidonda cha aina hii bila
shida yoyote, yatazuia pia kuendelea kuongezeka au kusambaa zaidi kwa
kidonda hiki.
Kama kuna matumizi mhimu sana ya dawa hii basi ni hili la kutibu vidonda
mbalimbali ikiwemo kidonda ndugu kidonda ambacho huletwa na bakteria na
kuwa sugu kutibika kwa dawa nyingi za kawaida.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku na upakae sehemu yenye kidonda mara 2 kila siku kwa majuma kadhaa.
28. Huondoa utegemezi wa madawa ya kulevya
Kutumia mafuta ya habbat soda kuondoa utegemezi (uteja) kwa madawa ya
kulevya na vilevi vingine ni moja ya kazi nyingine zilizothibitika
kufanywa na mafuta haya.
Katika majaribio, mafuta ya habbat soda yameonyesha kuwa msaada mkubwa
kutuliza hali ya kujisikia vibaya na mauzauza mengine yatokanayo na
kuacha kutumia dawa za kulevya na wakati huo huo yameonyesha kudhibiti
hamu ya kutaka kurudia tena matumizi ya madawa ya kulevya baada ya mtu
kuamua kuacha.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa mwezi mmoja na nusu mpaka miwili
29. Huondoa makovu
Iwe ni makovu ya upasuaji uliopita au ni makovu mengine yoyote, mafuta
ya habbat soda ndiyo dawa nzuri kwa ajili ya kuondoa makovu. Ni moja
kati ya dawa mbadala chache ambazo zimethibitishwa kuondoa na kutibu
makovu moja kwa moja.
Matumizi: Pakaa mafuta haya sehemu yenye makovu mara 2 mpaka 3 kila siku kwa majuma kadhaa.
30. Hutibu kansa ya mlango wa kizazi
Kansa nyingine ambayo mafuta ya habbat soda yamethibitika kuitibu ni kansa ya mlango wa kizazi (cervical cancer).
Hii tena inawezekana kutokana na kimeng’enya ‘thymoquinione’
kipatikanacho kwenye haya mafuta, tafiti zinaonyesha kuwa husaidia pia
kwa kuziongezea nguvu na idadi seli nyeupe za damu na kuzidhibiti seli
za kansa kuendelea kujizalisha.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.
31. Huzuia madhara ya miale ya jua
Tafiti zinaonyesha kuwa watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda
na kukaa kwenye jua masaa mengi walipatwa na madhara machache ya miale
ya jua kulingalisha na wale ambao walikaa juani muda mrefu bila kutumia
habbat soda.
Kiasi kikubwa cha kinga ya mwili kilionekana kwa watu waliokuwa
wakitumia mafuta ya habbat soda. Kuna tafiti pia zinazothibitisha habbat
soda kuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wa kansa walio kwenye matibabu ya
mionzi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha
mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku, pia pakaa kama mafuta yako
ya kupakaa kwenye ngozi kila siku
32. Huzuia na kutibu athari za sumu ya risasi
Sumu ya risasi (lead) ndiyo moja ya sumu zinazowapata watu wengi dunia
nzima sababu ya maendeleo ya viwanda na matumizi ya madawa ya
mashambani. Risasi inaweza kuleta shida na mambo mengi kuhusiana na kazi
za mwili wako kwa ujumla na kuleta matatizo katika moyo, tumbo, figo,
mfumo wa fahamu, mifupa na hata katika mfumo wako wa uzai.
Tafiti zimeonyesha kwamba mafuta ya habbat soda kuwa na uwezo mkubwa
kuzuia na kurekebisha madhara katika ubongo yaliyotokana na sumu ya
risasi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha
mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku, pia pakaa kichwani kila
siku yale ya nywele nayo yamethibitika kuwa yanatibu maumivu ya kichwa
na matatizo mengine mengi kuhusiana na kichwa
33. Huimarisha ukuwaji wa ndevu
Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda yanaweza kuhamasisha ubora na ukuwaji wa ndevu kidevuni.
Ingawa hii siyo kazi yake hasa ya msingi, unaweza kupakaa moja kwa moja
mafuta ya habbat soda ya nywele juu ya kidevu chako na utaona ndevu
zinakuwa na afya nzuri, zinakuwa haraka na kuziacha zenye unyevunyevu
pia.
34. Hutibu maumivu ya kuumwa na nyuki na nyigu
Unga wa habbat soda ukichanganywa na maji kidogo ni dawa nzuri kabisa ya
asili kwa maumivu au uvimbe kutokana na kuumwa na wadudu kama nyigu na
nyuki. Chua sehemu iliyoathiriwa na mchanganyiko huu kutwa mara mbili
kwa siku 2 au 4 hivi.
35. Huondoa msongamano kifuani
Mwagia na uchue kwa dakika kadhaa juu ya kifua chako na mafuta ya habbat
soda kuondoa msongamano (makohozi, gesi nk) kifuani. Utapata matokeo
mazuri zaidi kama utachanganya mafuta haya na asali kwa ajili ya hili
zoezi.
Unaweza pia kuamua kunywa mdomoni kijiko kidogo kimoja cha chai kila siku badala ya kupaka juu ya kifua.
36. Hutibu maumivu ya sikio
Mafuta ya habbat soda yakichanganywa na mafuta ya zeituni yanaweza
kutibu maumivu ya sikio na miwasho mingine masikioni. Changanya nusu
kijiko kidogo cha mafuta ya habbat soda na nusu kijiko kidogo kingine
cha mafuta ya zeituni, pasha moto kidogo mchanganyiko huu na kuweka
matone mawili matatu sikioni sehemu iliyoathirika.
Unaweza kuweka skafu au kofia juu ya sikio dakika 2 baada ya kunyunyiza
matone ya mchanganyiko huu na utulie sehemu moja kwa dakika kadhaa.
37. Dawa nzuri ya magonjwa ya macho na kuona
Mafuta ya habbat soda yanaweza kutumika pia kutibu maambukizi ya kwenye
macho na wakati huo huo kuongeza uwezo wa macho kuona (eyesight and
vision).
Yametumika pia na watu wengi kutibu maambukizi ya kwenye macho yao ambayo hupelekea macho kuwa mekundu.
Ili kutibu hayo unaweza pakaa mafuta haya sehemu zinazozunguka jicho
lako kabla ya kwenda kulala na unaweza kufanya zoezi hili kila siku kwa
matokeo ya haraka zaidi.
38. Hutibu kiharusi
Unapougua kiharusi hasa usoni, mafuta ya habbat soda yanaweza kuleta
nafuu haraka. Weka kiasi cha mafuta ya habbat soda kwenye bakuli au
sahani na usogeze pua yako karibu na mafuta na unuse nuse mafuta hayo.
Chukua sekunde 10 mpaka 20 kuvuta pumzi ndani kwa nguvu na urudie zoezi. Fanya zoezi hili kila siku mpaka upone.
39. Huondoa msongamano puani
Habbat soda pia hutumika kuzibua na kuondoa msongamano puani. Hii ni
moja ya kazi ambayo mafuta haya yanazifanya vizuri zaidi. Unaweza
kuyanywa na wakati huo huo kuyanusa puani kama nilivyoeleza kwenye namba
38 hapo juu.
40. Huondoa mawe kwenye kibofu cha mkojo
Kutumia mafuta ya habbat soda kwa ajili ya kuondoa mawe kwenye kibofu
cha mkojo ni njia nzuri ya kuondoa maumivu na mawe katika kibofu cha
mkojo kwa pamoja.
Uwezo mkubwa ulionayo mafuta haya katika kuondoa vivimbe na sifa yake ya
kuondoa sumu ndivyo vitu vinavyoyafanya mafuta haya kuwa dawa bora ya
asili ya kuondoa mawe katika kibofu cha mkojo.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku mpaka upone.
41. Huondoa mawe katika Ini
Kama ilivyo kwa mawe katika kibofu cha mkojo, mawe katika ini pia
yanaweza kusababisha maumivu na madhara mengine makubwa wakati ukijitibu
kwa kutumia dawa za viwandani.
Sifa za mafuta ya habbat soda huondoa mawe katika ini kwa hali ya mwendelezo mpaka yatakapoondoka yote.
Kunywa mafuta haya yakichanganywa na asali kwa matokeo mazuri zaidi.
Kijiko kidogo kimoja unaongeza na asali kijiko kidogo kimoja. Tumia kwa
mwezi mmoja hivi
42. Huondoa gesi tumboni
Mafuta ya habbat soda huusaidia mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula na
hivyo kukusaidia kuondoa gesi. Pia yamethibitika kuondoa mvurugiko wa
tumbo na takataka nyingine tumboni kwa haraka zaidi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku mpaka upone kabisa
43. Hutibu bawasiri
Dawa nyingi zinazotumika kutibu bawasiri zina madhara mengine mabaya na
nyingi ya hizo hazitibu kabisa bawasiri na kulazimisha wengine kufanya
upasuaji. Mafuta ya habbat soda kwa upande wake yanatoa suluhu ya haraka
katika kutibu bawasiri zote ya nje nay a ndani na tafiti zinaonyesha
yanao uwezo wa kuzuia kusambaa au kuongezeka kwa ugonjwa huu.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha
mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku, pia pakaa sehemu yenye
tatizo nje na ndani kutwa mara 2 kwa majuma kadhaa
44. Huondoa maumivu ya kichwa
Faida nyingine mhimu ya mafuta ya habbat soda ni uwezo wake katika
kutibu maumivu ya kichwa na kipanda uso. Kwa karne nyingi Waarabu na
Wazungu wamekuwa wakitumia mafuta haya kwa kupaka maeneo ya karibu na
pua, macho na sehemu ya mbele ya kichwa ili kuondoa maumivu ya kichwa.
Hata ukiyanywa kijiko kidogo kimoja kila siku maumivu ya kichwa yatapotea.
Pia yale meusi kwa ajili ya nywele nayo yanaondoa maumivu ya kichwa na
hili nimelishuhudia mimi mwenyewe nilikuwa na tatizo la kuumwa kichwa
mara kwa mara sababu ya kukaa kwenye computer masaa mengi lakini tangu
nianze kutumia mafuta haya sijawahi kuumwa kichwa tena.
45. Huongeza kinga ya mwili
Unaweza kutumia mafuta ya habbat soda kuimarisha kinga yako ya mwili kwa
ujumla na hivyo kuongeza ulinzi wa mwili wako dhidi ya magonjwa
mbalimbali ikiwemo dhidi ya bakteria na virusi. Mafuta ya habbat soda
ndiyo bidhaa pekee ya asili iwezayo kuimarisha kinga yako ya mwili kwa
muda mfupi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku mpaka kinga yako imeimarika.
Unaweza kutumia pia mafuta haya hata kama huumwi chochote.
46. Husaidia mama anayenyonyesha
Mafuta ya habbat soda yakitumika na mama anayenyonyesha husaidia
kuongezeka kwa uzalishwaji wa maziwa. Kunywa kijiko kidogo kimoja cha
chai kutwa mara 1 kila siku.
47. Huongeza kumbukumbu
Utafiti unaonyesha kuwa mafuta ya habbat soda yana uwezo wa kuongeza
uwezo wako wa kumbukumbu, ufahamu na umakini. Karibuni imethibitika
habbat soda yanaweza kuongeza uwezo wa kukumbuka vitu kwa haraka
vikiwemo vya muda mfupi na hata vile vya muda mrefu.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha
mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku mpaka hali yako ya
kukumbuka vitu imekaa sawa.
48. Huondoa madoa meusi kwenye ngozi
Moja ya kazi za mafuta ya habbat soda ambazo wengi hawazijuwi ni hii ya
kuondoa madoadoa au mabaka meusi juu ya ngozi. Unachohitaji ni kuyatumia
kama mafuta yako ya kupakaa kila siku na hutachelewa kuona matokeo.
49. Huondoa maumivu ya kung’atwa na wadudu
Wadudu kama mbu na wengine wanapokuuma huacha pia maumivu fulani na hata
uvimbe. Kupaka mafuta haya juu ya eneo lililoathirika kutasaidia
kuondoa maumivu na uvimbe au muwasho wowote sababu ya wadudu hao.
50. Hutibu kukauka kwa midomo (Lips)
Tatizo hili la midomo ya nje (lips) kukauka limepelekea kutengenezwa kwa
bidhaa nyingi za viwandani kwa ajili hiyo na wanawake ndiyo wanaonekana
kuzitumia zaidi huku baadhi ya bidhaa hizo zikiripotiwa kusababisha
baadhi ya saratani.
Mafuta mhimu (essential oils) yapatikanayo katika mafuta ya habbat soda
yanaweza kuzuia kukauka kwa mdomo na kuzalisha upya ngozi kwenye sehemu
za nje ya mdomo (lips) na kukuachia rangi safi ya asili ya lips zako
bila madhara yoyote mabaya hapo baadaye.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha
mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kila siku, pia pakaa sehemu ya lips
zako kila siku.
51. Yanatibu kufunga choo
Kama vile yanavyokusaidia katika mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula
ndivyo yanavyokusaidia pia kwa tatizo la kufunga choo au kupata choo
kigumu sana. Kuna watu wengine asipopata choo hata siku mbili haoni kama
ni tatizo kwake na mwingine amezoea kupata choo kigumu kila siku na
anaona ni kawaida tu.
Kufunga choo au kupata choo kigumu sana kila mara ni ishara mbaya kuhusu
afya yako. Ni dalili ya moja kwa moja kuwa huna maji ya kutosha mwilini
au maji unayokunywa hayabaki mwilini na yanapitiliza kwenda nje bila
kutumika na mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula.
Mafuta ya habbat soda yanatibu tatizo la kufunga choo (constipation)
bila shida yoyote. Kunywa kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya kila
baada ya chakula cha mchana na baada ya chakula cha usiku kwa matokeo ya
haraka.
52. Hutibu maumivu ya mgongo na mishipa
Unaweza kupunguza mahitaji ya dawa za kuondoa maumivu ya mgongo na
mishipa kwa kupaka au kujichua na mafuta ya habbat soda sehemu yenye
maumivu moja kwa moja.
Hutakawia kuona nafuu kwa haraka.
53. Husaidia kuondoa maumivu ya tumbo
Kwa matatizo mengi ya tumbo, mafuta ya habbat soda yanaweza kuwa msaada mkubwa wa kukupa nafuu kwa haraka.
Kuondoa maumivu ya tumbo ni moja ya kazi kubwa inayotambulika na wengi
ya mafuta ya habbat soda. Kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku baada ya
kula chakula cha usiku kwa matokeo ya haraka.
54. Huondoa maambukizi kwenye fizi
Maumivu na maambukizi kwenye fizi za meno vinaweza kuondolewa kwa
kutumia mafuta ya habbat soda. Uwezo wake wa kuondoa sumu na uvimbe
ndiyo sababu ya madaktari wengi kupendekeza itumike kutibu maambukizi
kwenye fizi.
Unaweza kutumia kama dawa yako ya mswaki pia uyanywe kijiko kidogo kimoja kila siku.
55. Hutibu U.T.I
Maambukizi na matatizo mengi kwenye kibofu cha mkojo na njia ya mkojo
kwa ujumla yanatibika na mafuta ya habbat soda ikiwemo ugonjwa wa U.T.I
(yutiai) unaowasumbua watu wengi miaka ya karibuni.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.
56. Huzuia mdomo kukauka
Kutibu tatizo la mdomo kukauka chukua kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya na weka mdomoni kwa sekunde 30 hivi.
Jigeuzegeuze kichwa na mdomo kuhakikisha mafuta yanagusa kila sehemu za
mdomo wako kabla ya kutema au unaweza hata kuyameza. Kisha safisha mdomo
na kinywaji kingine kitamu kama juisi hivi au asali kuondoa radha yake
ya ukakasi.
57. Huzuia pua kuvuja damu
Haya ni moja ya matumizi ya asili ya mafuta ya habbat soda nyakati za
joto katika majira ya kiangazi katika jamii nyingi mashariki ya kati.
Kama unapata tatizo la pua kuvuja damu unachotakiwa kufanya ni kuweka
matone mawili au matatu ya mafuta haya ndani ya pua zako na ukae utulie
uone kazi ya mafuta ya habbat soda kuzuia damu kuvuja puani.
58. Huondoa majeraha ya kuungua moto
Kupaka mafuta ya habbat soda juu ya majeraha ya kuungua kwa moto au maji
ya moto kumethibitika kuponya majeraha hayo na kuzalisha upya ngozi.
Kuondoa majeraha hayo chua eneo lenye athari ukitumia mafuta ya asili ya
habbat soda kwa kuondoa maumivu haraka na kuizalisha upya ngozi yako.
59. Hutibu mba kichwani
Mafuta haya si mazuri kwa ajili ya kukuza au kuotesha nywele zako tu,
bali pia huhamasisha ukuwaji wa vinyweleo vya ngozi na hata kuzuia na
kutibu mba.
Unachohitaji kufanya ni kupaka mafuta ya kutosha ya habbat soda ya
nywele kichwani kwako na uache kama dakika 30 hadi 60 hivi na unaweza
kujisafisha au kuacha hivi mpaka utakapoenda kuoga tena.
Na mafuta haya unapoweka kichwani yanadondoka kidogo kidogo hadi kwenye
ubongo na utaona vitu kama maumivu ya kichwa vinaanza kuisha taratibu.
60. Huondoa maumivu kwenye maungio
Moja ya matumizi yanayojulikana na wengi zaidi ya mafuta ya habbat soda
ni kutibu maumivu ya kwenye maungio (joints) mbalimbali mwilini. Utapata
nafuu ya haraka ukitumia mafuta haya kuondoa maumivu katika maungio.
Unaweza kujichua ukitumia mafuta haya moja kwa moja sehemu yenye maumivu
kwa matokeo ya haraka zaidi. Pia kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku
kwa matokeo mazuri zaidi.
61. Huzuia kudhurika kwa figo kama matokeo ya Kisukari
Ukiacha ukweli kwamba mafuta ya habbat soda ni dawa mbadala nzuri kabisa
ya kutibu Shinikizo la juu la damu na Kisukari pia ni dawa ya kuzuia
kudhurika kwa figo kama matokeo ya kuugua ugonjwa wa kisukari.
Sababu ya hili ni kutokana na viinilishe mhimu sana vilivyomo kwenye habbat soda ambayo hujulikana pia kama ‘nigella sativa’ au ‘black seeds’.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
62. Huweka sawa mzunguko wa hedhi
Mafuta haya yana kazi mhimu sana linalopokuja suala la kulinda na kutibu
matatizo mbalimbali ya uzazi. Matatizo karibu yote ya uzazi kama
maumivu ya tumbo chini ya kitovu, siku za mwezi zisizoeleweka au
kutokuwa na mzunguko maalumu, kukosa hedhi, matatizo katika mfuko wa
uzazi na hata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Ni dawa nzuri kutumika hata kwa wamama wakubwa wanaopatwa na matatizo
kutokana na kusimama kuona siku zao. Unaweza kuyanywa kijiko kidogo
kimoja kila siku na hata kupaka ndani ya uke mara kwa mara kwani
hutumika pia kutibu .U.T.I na fangasi za ukeni.
63. Mazuri wakati wa ujauzito
Inasisitizwa kuwasiliana na daktari wako wakati wa ujauzito kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote.
Hata hivyo mafuta ya habbat soda yameonyesha matokeo chanya hata
yakitumika wakati wa ujauzito ingawa bado hakuna hitimisho la jumla
ikiwa yatumike kwa mama mjamzito au yasitumike sababu katika baadhi ya
kesi yanaonyesha kupunguza kukazika kirahisi kwa misuli ya mfuko wa
nyumba ya uzazi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
64. Hutibu baridi yabisi (Arthritis)
Mafuta ya habbat soda yamethibitika kuwa dawa bora dhidi ya ugonjwa wa
baridi yabisi, maumivu kwenye mishipa na hali ya mwili kuwaka moto kwa
ujumla.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku mpaka upone.
65. Hutibu vidonda vya tumbo
Ni moja ya dawa za asili chache zinazoweza kutibu vidonda vya tumbo moja
kwa moja. Tafiti nyingi zinathibitisha mafuta ya habbat soda yanatibu
aina zote za vidonda vya tumbo!
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa
mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa hadi siku 60. Vidonda vya tumbo pia
upate unga wa asili wa majani ya mlonge na unga wa mbegu za maboga kwa
matokeo mazuri na ya uhakika.
Kumbuka pia kunywa maji mengi ya kutosha kila siku, epuka pia vinywaji na vyakula vyenye asidi nyingi.
66. Yanaondoa maumivu mbalimbali
Mafuta ya habbat soda yanaondoa mahitaji yako kwa dawa nyingi za kuondoa
maumivu (painkillers) mbalimbali mwilini. Katika kesi nyingi mafuta ya
habbat soda yanaweza kuondoa kabisa mahitaji ya dawa za kuondoa maumivu.
Uwezo wake wa kuondoa vivimbe unayafanya kuwa chaguo zuri zaidi katika
kutibu maumivu yote ya mwili wako kutoka kwenye nywele mpaka kwenye
kucha.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.
67. Hutibu kansa ya Ubongo
Mafuta ya habbat soda ni msaada mkubwa katika kudhibiti na
kusambaratisha vivimbe kwenye ubongo na seli za kansa kwenye ubongo
wako.
Makundi kadhaa ya watafiti wamehitimisha kuwa mafuta ya habbat soda ni
dawa halali ya asili kwa ajili ya kutibu kansa ya ubongo na uvimbe
katika ubongo.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa
mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa. Pia pakaa kichwani moja kwa moja ama
mafuta ya habbat soda ya kawaida au hata yale ya nywele kila siku.
68. Yanapunguza wasiwasi (Anxiety)
Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda kuwa msaada mkubwa katika
kudhibiti tabia za kuhamaki na wasiwasi na hivyo kukuwezesha kujisikia
vizuri kila mara. Na utaona matokeo haya baada ya matumizi ya habbat
soda kwa siku 30 hivi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
69. Huondoa huzuni na mfadhaiko (stress)
Tafiti kadhaa zimeonyesha watu waliokuwa wakitumia mafuta ya habbat soda
wanakuwa ni watu wenye furaha ya asili na kuwa si wepesi kuwa na huzuni
au kufadhaika.
Kazi hii ya mafuta ya habbat soda ndiyo mhimu kuliko zote sababu
mamilioni ya watu wanakabiliwa na tatizo la kuwa na huzuni au stress na
mifadhaiko ya akili kitendo ambacho kinaweza kuharibu kinga zao za mwili
na maisha kwa ujumla.
Ni vigumu sana kupata mtishamba ambao unaweza kutibu matatizo
yanayohusiana na saikolojia moja kwa moja lakini mafuta ya habbat soda
yanaweza kutumika kwa dhumuni hili la kutuliza, kupunguza na kutibu
tatizo la huzuni au kufadhaika kwa akili.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa
mara 1 kila siku na kwa matokeo mazuri pata pia unga wa mbegu za maboga
zilizokaangwa kidogo na chumvi ya mawe ya baharini, tumia muda mrefu
hata miezi miwili hata zaidi ikibidi.
70. Hutibu kizunguzungu
Historia nyingine katika matumizi ya mafuta ya habbat soda ni katika kutibu kizunguzungu.
Mafuta ya habbat soda yanatambulika kwa kutibu kizunguzungu na kile
unachotakiwa kufanya ni kujichua shingoni na mashavuni kwa kutumia
mafuta ya habbat soda na dalili za kizunguzungu zinatakiwa zianze
kupotea mara moja.
Fanya zoezi hili kwa wiki 2 hivi
71. Hutibu Kiungulia
Faida nyigine kubwa ya mafuta ya habbat soda ni kuwa ni dawa ya asili
dhidi ya kiungulia. Ingawa kuna tafiti chache zinazoweza kuthibitisha
hili, bado historia inaonyesha mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika
kutibu kiungulia kwa karne nyingi.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
72. Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu
Kumekuwa na tafiti nyingi hivi karibuni ambazo zimeonyesha mafuta ya
habbat soda kuwa msaada mkubwa kwa kuzuia na kupunguza kuongezeka kwa
dalili za ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Matokeo yalionyesha kwamba yakitumika kila siku kijiko kidogo kimoja hadi viwili vya chai huleta matokeo mazuri zaidi.
73. Hutibu homa ya uti wa mgongo
Nguvu za mtishamba huu zimethibitika kuwa msaada mkubwa katika kutibu
homa ya uti wa mgongo (meningitis). Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa
mafuta ya habbat soda ni moja ya tiba asili nzuri zaidi kwa ajili ya
homa ya uti wa mgongo inayoaminiwa hadi sasa.
Kunywa kijiko kidogo kimoja hadi viwili vya mafuta haya kila siku kwa majuma kadhaa.
74. Huongeza afya ya figo
Kuanzia kwenye ugonjwa wa figo hadi kwenye mawe ya kwenye figo, mafuta
ya habbat soda yamethibitika kuwa msaada mbadala kwa matatizo ya figo.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
75. Huimarisha afya ya mbegu za kiume
Ukiacha uwezo wake katika kuongeza stamina na nguvu kwa wanaume na
kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake, mafuta haya pia hutumika
kutibu tatizo la afya dhaifu la mbegu za kiume na kuongeza wingi wake
kwa ujumla (semen count).
Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, mbegu za kiume zinaonekana kuimarika na
kuwa nyingi za kutosha baada ya kutumia dawa hii kwa miezi miwili kila
siku.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
76. Huimarisha mifupa
Tafiti zimeonyesha kuwa mafuta ya habbat soda yanaongeza ukuwaji wa seli
za uboho wa kwenye mifupa kwa asilimia 150 yanapotumika. Hii ni kwa
mjibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa kwa watu wengi mbalimbali.
Kile kinashangaza zaidi ni kuwa mafuta haya yameonekana kuwa na uwezo wa
kuzuia uongezekaji wa vivimbe mbalimbali walau kwa zaidi ya asilimia
50.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa mwezi mmoja hata miwili.
77. Tiba asili ya chango kwa watoto
Ukiwa na mtoto anayesumbuliwa na chango au msokoto wa tumbo linaweza
kuwa ni jambo linalokupa msongo wa mawazo maishani. Ingawa visababishi
vya chango kwa watoto bado havijulikani bayana, kile ambacho
kimethibitishwa ni kuwa mafuta ya habbat soda ni tiba asili kwa chango
au msokoto wa tumbo kwa watoto.
Ni mhimu kuanza na kiasi kidogo sana kama matone matatu hadi matano na uendelee kuongeza kiasi cha dawa kidogo kidogo kila siku.
78. Hurekebisha matatizo katika tezi dume
Afya ya tezi dume ni ishu kwa wanaume wengi duniani kote na kupata dawa
ya asili nzuri kwa ajili hiyo inaweza kuwa mtihani kwa wengi.
Kwa bahati nzuri mafuta ya habbat soda yamekuwa yakitumika kwa ajili ya
kuimarisha afya ya tezi dume kwa karne nyingi sasa. Tafiti zinaonyesha
kuwa ni dawa nzuri hata kwa saratani ya tezi dume.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa wiki 4 hadi 6.
79. Huondoa udhaifu wa mwili kwa ujumla (lethargy)
Wengi wetu tunapatwa na kupungukiwa na nguvu za mwili na wakati fulani
nguvu zote za mwili kwa ujumla na nguvu za ubongo na za kiroho pia.
Kwa ajili ya matatizo ya udhaifu wa mwili iwe kimwili, kiakili na hata
kiroho hakuna dawa nyingine ya asili iwezayo kurekebisha hali hizo kama
yawezavyo kufanya hivyo mafuta asili ya habbat soda.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku
80. Huondoa uchovu sugu
Kutoka kwenye maelezo yaliyotangulia hapo juu, mafuta haya pia
yamethibitika kuondoa uchovu sugu wa aina zote na kuupa nguvu mpya
mwili.
Matumizi yake ni kama kwenye namba 79 hapo juu.
81. Huhamasisha uzalishwaji wa mkojo
Faida nyingine kubwa ya mafuta ya habbat soda ni uwezo wake wa kuhamasisha uzalishwaji wa mkojo.
Matatizo mengi ya kibofu cha mkojo na tezi dume yamekuwa yakitibiwa kwa
kutumia mafuta ya habbat soda kwa zaidi ya miaka 2000 sasa na tafiti
zimethibitisha hivi karibuni faida hizi za mafuta ya habbat soda katika
majaribio ya kimaabara yakionyesha kuimarisha sana kwa afya ya tezi dume
na kazi zake kwa ujumla.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.
82. Huzuia madhara yatokanayo na shambulio la moyo
Kama tulivyoona pale mwanzo kabisa kuwa mafuta ya habbat soda yamekuwa
yakitumika miaka mingi kutibu matatizo mbalimbali ya moyo, vivyo hivyo
yameonekana kuzuia madhara ya pili yatokanayo na shambulio la moyo
(heart attack) na magonjwa mengine kwenye mfumo wa upumuwaji kwa ujumla.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.
83. Husaidia kuongeza damu mwilini
Wengi wetu tunakumbwa na tatizo la kupungukiwa damu (anemia) na hili
linaweza kuiweka miili yetu katika hali ya hatari zaidi. Kwa mara
nyingine tena mafuta ya habbat soda yanaonekana kuokoa tatizo hili baya
la kiafya.
Yamethibitika kutibu tatizo la upungufu wa damu moja kwa moja.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
84. Huondoa vimelea vya magonjwa
Mafuta ya habbat soda ni kinga dhidi ya vimelea (parasites) vingi vya
magonjwa na huvitafuta na kuviua vimelea hivi popote vitakapokuwa ndani
ya mwili. Hufanya kazi hii kwa kuvilevya hivyo vimelea na kuupa urahisi
mwili kuviangamiza.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
85. Husaidia kupunguza uzito
Kwa sababu uzito na unene kupita kiasi huhusiana pia na matatizo mengine
ya kutofanya kazi kwa kinga ya mwili, ukaidi wa insulin, kansa na
matatizo mengi katika mfumo wa upumuwaji, ndipo mafuta ya habbat soda
yanapokuja kuwa mhimu kwa ajili ya kupunguza uzito na unene kupita
kiasi.
Mafuta ya habbat soda yamethibitika na watafiti wengi kote duniani kuwa msaada mkubwa kwa wale wanaotaka kupunguza uzito.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa wiki 4 hadi 6.
Usisahau pia kufanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku dakika 60,
epuka kukaa kwenye kiti masaa mengi na ubadili chakula unachokula kila
mara hasa uepuke vyakula vya wanga na vile vyenye mafuta mengi na unywe
maji ya kutosha kila siku.
86. Huziua seli za kansa za aina nyingi
Hutibu na kuziua seli za karibu kansa za aina zote, kansa ya mdomoni, kansa ya ini, kansa ya kongosho nk.
Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda kuwa dawa nzuri dhidi ya kansa
mbalimbali mwilini kwa kuzuia uongezekaji wa seli za kansa na
kusambaratisha kansa zenyewe katika baadhi ya kesi.
Hufanya kazi hii kwanza kwa kuiimarisha kinga yako ya mwili na kuziua seli zenyewe za kansa moja kwa moja.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa mwezi mmoja hadi miwili.
87. Huongeza afya ya ini
Mafuta ya habbat soda yanaimairisha afya ya ini kwa ujumla na kuimarisha
kinga ya mwili. Ni dawa nzuri kutibu matatizo mengi ya ini hata kama
familia yenu wote mna historia ya kuugua ugonjwa wa ini.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa
88. Huondoa sumu mwilini
Tatizo la mwili kuwa na sumu ni tatizo kubwa kwa watu wengi miaka ya
karibuni na kupata mtishamba au dawa ya asili kwa ajili ya kuondoa sumu
bado ni mtihani kwa watu wengi. Kwa bahati nzuri kwa upande wako umepata
mafuta ya habbat soda.
Mafuta ya habbat soda yamethibitika kuondoa sumu kila sehemu ya mwili yanapotumika.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa wiki 4 hadi 6
89. Huondoa hali ya kuchanganyikiwa (Schizophrenia)
Kutokana na sifa yake ya kuondoa vivimbe na sumu mwilini mafuta ya
habbat soda yanaweza kutumika pia kutibu ishara na dalili za
kuchanganyikiwa.
Tafiti zimeonyesha mafuta ya habbat soda yakitumiwa na watu wenye
kuchanganyikiwa wanapata nafuu haraka ya tatizo hilo ukilinganisha na
wale wasiotumia mafuta haya.
Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku kwa majuma kadhaa.
Hitimisho:
Ni rahisi kuelewa kuwa faida nyingi ambazo mafuta ya habbat soda inazo
zinawashangaza bado watu wengi. Unaweza kudhani hayo hayawezekani kwa
mtishamba wa asili kutoa tiba kwa magonjwa mengi namna hiyo! Kile
ninachojuwa ni kuwa ukweli hujieleza wenyewe.
Kiasi cha faida kinachopatikana katika mafuta haya ukilinganisha na bei
yake ndicho kinachowafanya watu wengi wabaki na mshangao usioisha!
Watu wengi wanashangaa ni kwanini makampuni mengi ya madawa yatumie
mabilioni ya pesa kutengeneza dawa mbalimbali kwa magonjwa mengi ambayo
yangeweza kutibika kwa kutumia mafuta ya habbat soda tu kama tulivyoona
hapo juu.
Ukiacha hayo, kupata hospitali na ukapata matibabu sahihi na kwa gharama
nafuu bado ni changamoto katika nchi nyingi maskini na nyingi ya dawa
zinakulazimu kuendelea kuzitumia kwa kipindi kirefu na pengine bila hata
uhakika wa wewe kuja kupona.
Bahati nzuri kwa wewe ambaye umebahatika kupata habari hizi za habbat
soda na umeweza kuona ni magonjwa mangapi unaweza kutumia kujikinga na
kujitibu nayo.
Na jambo zuri kuliko yote ni kuwa huhitaji kutoka hata jikoni kwako ili
kupata nafuu ya ugonjwa wowote ukiwa na mafuta ya habbat soda karibu
yako.
Mtishamba huu wa ajabu utaendelea kubaki kwenye vitabu vizazi na vizazi
vingi vijavyo kama moja ya tiba asili mhimu zaidi iliyowahi kujulikana
na binadamu.
Unahitaji mafuta ya asili ya habbat soda au unga wa habbat soda? Niachie ujumbe WhatsApp +255625640247
No comments