MAMBO 15 AMBAYO WANAUME WANAYATAKA KATIKA MAHUSIANO (LAKINI WANAWEZA WASIKUAMBIE)
Tunakupenda, tunakuhitaji, tunakutaka.lakini ni nini hasa tunatafuta kwa mwanamke?
Hatutapiga kelele,au kuandika, au kuweka na kuonyesha katika profile,au kuongelea hilo sisi wenyewe.
Hapana. Wanaume wengi hawana tabia
ya kusema wanachohitaji, lakini naweza kukuambia kutokana na uzoefu
wangu mwenyewe, ingawa sio yote, wanaume wanakutaka na kukuhitaji
uwafanyie vitu kama vifuatavyo.
1.WEMA WAKO.
Ulimwengu unaweza ukawa na ukatili
na uonezi na adhabu ,kazi zetu zinaweza kuwa mbaya, na kukawa na
ushindani mwingi, tunashughulika na kuhukumiana na kutofautiana kwa wale
walio karibu yetu, kuhukumiana kidogo, kusameheana kidogo na uelewa
kutoka kwa wanawake tunaowapenda umeenda mbali.
2.FURAHA YAKO.
Tuambie umefurahi, tuonyeshe
furaha, tunahitaji kuwepo karibu yako unapokuwa na furaha, tutakuwepo
wakati ukiwa na hali mbaya, kwenye tatizo lolote, lakini furaha yako
ndio itakayokuwa inatuvuta kuwepo karibu na wewe, pamoja na kwamba
yanatuhusu sisi hayo.
3.SIFA NA SHUKRANI ZAKO.
Muda mwingine tunafanya vitu
vizuri, tuambie kuwa unashukuru na unathamini hicho na jinsi
ulivyopendezwa na na hicho na kukufanya uwe mwenye furaha, Onyesha
kuwa umeshukuru kuwa na wao katika maisha yako, na unakubali company
yao, mchango wao, na ushirikiano.
4.IDHINI YAKO.
Hatupendi kukubali, lakini mara
nyingi huwa hatufikirii kuwa kibali chako ndicho tunachohitaji, jinsi
tunavyoishi au kutenda.Chukua hio nafasi wakati tunapokuwa sahihi
kuturuhusu kufahamu kwamba umekubali.Tuambie umekubali maamuzi yetu,
uchaguzi wetu,au jinsi tunavyoshughulikia vitu, tuambie unafurahishwa
na sisi na unaona fahari kuwa na sisi.
5.MGUSO WAKO.
Tunahisi mguso wako , kujali
kwako, mabusu yako, urafiki wako kwetu ni muhimu sana-yawezekana ni
kidogo lakini ni muhimu .unapotugusa tunahisi kupendwa, unapokuwa muwazi
kwetu kwa upendo mwingi,unatufanya tujisikie ulimwengu ni wetu wote.
6.SHAUKU YAKO.
Tunakutaka wewe ututake sisi, tuambie kwamba uko ndani, jielezee shauku yako kwetu.
7.NGUVU YAKO NA KUSAIDIA.
Tunakuhitaji sana pale tunapopita
katika changamoto nyingi za maisha yetu. Hata kama hatuwezi kuongelea
hicho, tunahitaji mtu mwenye nguvu ya kimya kimya, tunahitaji mtu wa
kutuweka sawa, kusaidia,na kututia moyo, tuambie tuko nyuma yako
tunapokuwa tunapita katika matatizo mbalimbali.tunaweza tusiongelee
hilo , lakini uwepo wako pale tunapokuhitaji ni muhimu kwetu.
8.UELEWA NA UWEPO WAKO.
Sisi ni watatuzi na tunapenda
kutatua mambo.tunaposhughulikia matatizo, hatuhitaji ufumbuzi zaidi ya
kukuhitaji uelewa wako na uwepo wako.inaweza kuwa hatuongei ni kitu gani
kinatutatiza, lakini ukiwepo, na kuelewa na kuwa msaada hicho ndicho
tunachotaka. Tunachotaka ni kujua kuwa hatupo peke yetu.
9.UNYENYEKEVU WAKO NA UWEZO WA KURUHUSU.
Tunataka mwanamke mwenye
kutuheshimu na anaeleta usawa, tunataka mwanamke anaekubali kufikia
mwafaka na ambaye anakubali kwa upesi bila kinyongo
tunapoharibu.hashikili neno, anaweza kuachia bila kinyongo na kutoa
nafasi tena.
10.UKWELI WAKO.
Kama wewe, tunahitaji tujisikie
kuwa sisi ni pekee katika maisha yako. Tusaidie tujisikie tunahitajika
zaidi kwako kwa kutuonyesha kwamba una wajibu kwetu. Uwepo pale
tunapokuhitaji, tusaidie kuliko mtu mwingine yeyote.
11.UAMINIFU WAKO.
Tunathamini uaminifu wako na
kutuamini sisi, tunakutaka uwepo na sisi pale tunapokuhitaji , na
kutuonyesha kuwa unajali.Kwa inshara hio hio tunataka uamini kwamba
tunategemewa, tunawajibika,na tutakuwa pale unapohitaji tuwepo.
12.UVUMILIVU WAKO.
Sisi sio wakamilifu,inawezekana
sio mwanaume ambae ulimtarajia, tunakubali uvumilivu wako kwa
kutusaidia kukua katika mtazamo tunaoweza kuwa,hatuwezi kubadilika mara
moja . msisitizo wako na uvumilivu wako utatufanya kubadilika jinsi
unavyotaka tuwe.
13.MOYO MSIKIVU NA UCHESHI.
Maisha ni ya muhimu na ya
kuchukulia umakini sana, watu hufanya makosa, hujikwaa,na hata
kumsikitisha mtu, tunapopita katika magumu, mambo yanapotuchanganya
ulimwenguni, tunahitaji kuwa na mtu fulani ambae atakupa furaha katika
mambo madogo, ucheshi wako,furaha yako na kuonyesha kujali hutufanya
tufurahie maisha zaidi.
14.URAFIKI WAKO.
Tunahitaji urafiki wako kila siku
na kila mara.tunataka kufurahia muda na wewe, tunahitaji kushiriki
mvuto wako, kutengeneza urafiki na kuteka mioyo yetu.
15.UMBALI WAKO (WAKATI MWINGINE).
Sio kwamba sisi ni wanaume
wanaopenda kuishi kwenye mapango, wale wanaohitaji muda mwingi kuwa peke
yao kama tunavyotaka kufanya kwako, Lakini tunahitaji kupata muda
kidogo tu ili kucharge hisia wakati mwingine, zawadi kubwa ambayo
tunataka kutoka kwako ni kutoa muda ili tuwepo peke yetu ili kujiona
kuwa tunakuhitaji. Inatupa balance na nafasi ya kukuhitaji zaidi.
Jipange .
mimi nimeanza kuelewa , kuvuliana , kuamini,kuwa mkweli , kuwa mnyenyekevu n.k . je wewe?
washirikishe na wengine makala hii wajifunze pale wanapokosea . Kisha toa maoni yako.
No comments