MUME WA MTU


me swali langu haliiitaji hata kutaja umri…..hivi mtu anaposema ”Nina nyota ya KUPENDWA NA WANAUME ZA WATU” hua ana maana gani?maaana nakua sielewi anakua usoni ana chata flani?ama n vipi?mwingine anasema hivyo kwa furaha na mwingine atasema hivyo kwa huzuni…

MAJIBU YA WADAU

ninacholelewa hapo ni kama kismati cha kupendwa na aina fulani ya watu,mwingine atakua anafurahia kwa sababu anapendezwa na hio hali na mwingine hafurahi maana hapendezwi nayo,mfano unakuta mschana yuko katika kutafuta mtu muafaka wa kupanga nae maisha na kuoana sasa hapati huyo mtu anapata waume za watu tu hapo hawezi kufurahi na mwingine unakuta ni mschana wa mjini tu shida yake pesa sasa hao waume za watu yeye ndio mwakeee hapo waje hata mia yeye ndio anafurahiii yeye ni pesa tu

kweli inakera sana,pale unapomuomba mungu kila siku akupatie wa kwako mwanaume ambae yupo single lakini unaishia kutongozwa na kupendwa tena na kudekezwa juu na mume wa mtu,na hizi haja za mwili na sie wanawake tukidekezwa na kulelewa kama yai na mwanaume tunajikuta automatical unajiachia nae ukizinduka unakasirika unamtimua akija kukubembeleza unamrudia huku ukijisemea ngoja tuu niwe nae kwa mda mpk pale nitakapopata ambae hajaoa maana lasivyo utaishia kugawa papuchu kama pipi kwa vijana ukidhani utatulia nae kumbe mwenzio anataka kukupitia,jamani sio siri kwa upande wangu nashukia sana na nina hiyo nyota kila anayenitongoza na kutaka kusettle na mie ni mume wa mtu,yaan nina chukia na sina jinsi labda ipo siku mungu ataniona na kuniondolea hii nyota.

yaani mimi naamini kuna matukio yanakuwa yanamtokea mtu kutokana na background yake.

1: Family curse/blessings
kuna laana au baraka zinazotembea ktk familia au ukoo ndio pale utasikia wale kwao wote wamezaa na waume za watu, au wale kwa waume za watu hatari.so hiyo mtu inakua sio choice yake bali ni nature inalazimisha.

2: Maneno uliyowahi kujienea huko nyuma hasa wakati unakua.
Yes maneno yanaumba. mfano kuna watu wakiwa wanakua wanaona mfano wa dada zao, ma aunt na majirani wakipewa maisha na waume za watu. binti anaanza kuota na kukiri kwamba akikua atapenda apate mume wa mtu amhudumie. ndivyo inavyotokea. kuna kitu kinaitwa the law of attraction. yaani what you think about you bring about. ukiangalia maisha yako ya sasa utaona ni vitu ulivyokua unaviota zamani

3: laana ya kujitakia
sijajua ukweli wa hili bali inasemekana ukionja tu mume wa mtu basi nyota yako inakuwa ya waume za watu. watakufuata hao tu hutapata kijana mwenzio.pia mwenye mume akigundua uko na mume wake na akakutamkia laana ni rahisi kukupata. so akikunenea kuwa utaishia kuwa kimada ndivyo itakavyokuwa.

4: jini mahaba
hili huwa halipendi msichana aolewe. hivyo litakuwa linakuletea waume za watu ili usiolewe.

5: the way you carry yourself
yes kuna jinsi unajiweka una attract waume za watu tu na sio masingle man. jiweke ki wife material na si kishangingi! mwe nimechoka kuandika ntaendlea baadae

lulu hapo napigana na wewe,sio wasichana wote wanaofatwa na waume za watu wanatamaa ya pesa hapana,binafsi siipendii hii hali na wala sina tamaa maana nina uwezo unaonitosheleza kabisa ila nachokosa ni mapenzi na kujalia na binadamu wa jinsia tofauti na mie kwa bahati mbaya wanaokuwa serious namie na wanaodumu kwa muda mrefu ni wanaume za watu na kwa bahati mbaya sijui nzuri mie sinaga tabia ya umalaya au kuhangaika na mwanaume zaidi ya mmoja,je mtu kama mie utaniweka kundi gani?na hata hao wanaume wananishangaaga kwanini siolewi wakati nina sifa zote za kuwa mke naishia kuwajibu mimi mwenyewe sijui labda muda wa mungu kuamua bado,ila sasa mama ushauri umenifungua kitu kutokana na ushauri wako lazima kuna kati ya hayo mambo uliyosema yananisababishia.kuanzia leo nitakazana na kufunga kwa maombi ili namii niwe huruu na hili janga.

yaaaan dada angu lulu upo sahihi kabisaaaa,jamaniiiii mie najutaaa na machozi juu,nitamuachajee huyu mwanaume nimekuwa nae mwaka na nusu sasa, ananijali utasema hajaoa na kwenye ndoa yake wanaamani tele najua kutokana anavyoongeaga na mkewe kwenye simu na sms zao wanazotumiana,.mwanaume anajua kupanga mambo yake mpk namshangaa ni mhaya ana miaka 37 mie 26,hapa nawaza mambo ya kurudi kuwa single na lonely mpk ntakapompata huyu ambae hajaoa nitaweza kweli na nilivyomzoea huyu jamanii kwa ushauri wake,anavyonijali,anavyonisaidia kwa mambo mengi,nitaweza jamanii kumuacha tuu bila ugomvi,naomba mnishauri unamuachaje mtu bila kuwa na ugomvi,maana kusema ukweli nikimpa sababu ya mie kutafuta mtu single alishasema wewe siku ukipata mtu anataka kukuoa na yupo serious niambie tuu nitaku let go, ila kamwe sitaacha kukupenda maana anasema tangu awe na mimi amekuwa na furaha sana hadi kwenye ndoa yake furaha na amani imerudi na naamini ivyo maana nimeona

No comments