Shinikizo la damu: Chanzo na Tiba yake
Nini maana ya shinikizo la damu?
Ni
msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa
damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa
uchafu.
Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer
Shinikizo la damu husababishwa na nini?
Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:
- Uvutaji sigara
- Unene na uzito kupita kiasi
- Unywaji wa pombe
- Upungufu wa madini ya potassium
- Upungufu wa vitamin D
- Umri mkubwa
- Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
- Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin
Uanishaji wa shinikizo la damu
- Presha ya kawaida <120 <80
- Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
- Presha hatua ya 1 140-159 90-99
- Presha hatua ya 2 160-179 100-109
- Presha hatua ya 3 ≥180 ≥110
Shinikizo
la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni
kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini.
Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata
masharti.
Katika
makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa maji
mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi gani
ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu. Endelea
kusoma.
Takwimu
za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja
duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku
likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi
(Strokes).
Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.
Dalili za shinikizo la damu:
- Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
- Kuchanganyikiwa,
- Kizunguzungu,
- Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
- Kutoweza kuona vizuri au
- Matukio ya kuzirai.
- Uchovu/kujisikia kuchokachoka
- Mapigo ya moyo kwenda haraka
- Kutokuweza kuona vizuri
- Damu kutoka puani
- Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.
‘Mwili
wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita
ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu na madawa –
dr. Batmanghelidj’.
Shinikizo
la damu (hasa la juu) ni kiashiria cha mwili kupungukiwa maji kwa
kiwango kikubwa, ni wakati ambapo mwili unajaribu kujizoesha na upungufu
wa jumla wa maji wakati kunapokuwa hakuna maji ya kutosha kuijaza
mishipa ya damu yenye kazi ya kusambaza maji kwenye seli mhimu.
Mishipa
ya damu imebuniwa maalumu kuendana na mtiririko uliosawa wa ujazo wake
wa damu na mahitaji mbalimbali ya tishu kwa kufunga na kufungua mishipa
mbalimbali ya damu ndani ya mwili.
Figo
hushtuka upesi kulingana na mtiririko wa damu. Hili linaposhindikana,
yaani iwapo mtiririko au ujazo wa damu utapungua, basi Figo huitoa
homoni iitwayo ‘renini’ ambayo yenyewe huzarisha kitu kiitwacho
‘angiotensini’ ambayo huwa na matokeo mawili; kwanza huzibana ateri na
kupandisha shinikizo la damu, pili huisababisha tezi ya ‘adreno’ kutoa
homoni iitwayo ‘aldosteroni’ ambayo huzifanya figo kuishikilia chumvi na
hivyo kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu.
Asilimia
94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu ina bahari
ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora
inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.
Chumvi
inayashikilia na kuyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli
(osmotic retention) na potasiamu inayashikilia maji ndani ya seli.
Wakati
mwili unapokuwa katika upungufu wa maji (yaani haunywi maji ya kutosha
kila siku) mwili utaongeza ujazo wa maji chumvi kwenye bahari ya nje ya
seli.
Kupitia
mfumo maalumu, homoni iitwayo ‘vasopressini’ hutolewa ambayo inaweza
kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli na kuyachoma
maji hayo baridi (baada ya kuwa yamechujwa) ndani katikati ya bahari ya
ndani ya seli kama yanavyohitajika ili kuutunza uwiano sawa wa maji
ndani na nje ya seli.
Lakini
ili mbinu hii ifanikiwe, mbinu gani, mbinu ya kuyachuja maji ya chumvi
toka katika bahari ya nje ya seli, vasopressini husababisha kapilari na
mishipa ya damu kujikaza au kupunguza vipenyo vyake na kukupatia wewe
shinikizo la juu la damu (BP) ambalo ni mhimu ili kuyachuja na kuyachoma
maji baridi ndani ya seli toka katika bahari ya maji chumvi iliyopo nje
ya seli.
Kama
mishipa ya damu haitapunguza vipenyo vyake, baadhi ya gesi itaachana na
damu ili kuziba nafasi zilizowazi kutokana na kupungua kwa umajimaji
mwilini na hatimaye kukusababishia msongamano wa Gesi (Gas locks).
Sifa
hii ya vipenyo vya mishipa ya damu kujirekebisha kwa ajili ya mzunguko
wa damu, ndiyo mtindo unaotumika zaidi katika kanuni za kihaidroliki
wakati ambapo mzunguko wa damu mwilini umejirekebisha kuendana na kiasi
cha umajimaji kinachopatikana.
Wakati
mwili unapokuwa katika upungufu wa maji kwa mfano kutokana na
kutokunywa maji ya kutosha; asilimia 66 ya kuishiwa maji inajionesha kwa
kupungua kwa ujazo wa seli, asilimia 26 inapotea toka ujazo wa
umajimaji uliopo sehemu ya nje ya seli na asilimia 8 tu inapotea toka
katika ujazo wa damu.
Shinikizo
la juu la damu ni kiashirio cha mwili kupungukiwa maji kwa asilimia 8
tu, lakini madhara yanajitokeza sababu ya asilimia 66 ya kupunguwa kwa
ujazo wa seli.
Maji na chumvi vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida.
Hii
ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza unywaji
wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa bora ya
kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.
Kama
watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu wangeongeza kiasi cha
uchukuaji maji, hawatazihitaji dawa za kukojosha, watazarisha mkojo wa
kutosha na hivyo kuiondoa chumvi iliyokuwa imezidi!. Watatakiwa pia
kuacha kula vyakula visivyo na chumvi na hivyo kuepukana na mikakamao ya
mishipa (cramps) kwenye miguu yao.
Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu:
Kwa
mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo la damu kama moja ya
ishara za mwili kupungukiwa maji na kulitibu kwa dawa za kukojosha
ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha;
- Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo
- Shambulio la moyo (heart attack)
- Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
- Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
- Kiharusi
- Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
- Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Daktari
mwingine, Dr.David Brownstein katika kitabu chake kiitwacho; “Salt Your
Way to Live”, anasema kwamba alifundishwa katika vyuo vya kiganga kuwa
chumvi husababisha shinikizo la damu na kuwa kila mmoja lazima ale
vyakula vyenye chumvi kidogo. Na hili watu wengi wamekuwa wakiamini
hivi.
Wakati
akiwatibu wagonjwa wake, anasema; alianza kuona kuwa wale wanaotumia
vyakula vyenye chumvi kidogo wanapata matokeo ya chini au wanapata nafuu
ndogo sana kutoka katika vyakula hivyo vyenye chumvi kidogo au bila
chumvi kabisa na wengi wao walitokewa kuwa na uhaba mkubwa wa madini
katika miili yao.
Katika
utafiti wake ili kuwasaidia wagonjwa wake, ndipo akaja na jibu la
chumvi ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ambayo huwa
na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake, alianza kuona kitu kigeni
kinaanza kutokea. Wagonjwa wake hao wakaanza kuona mashinikizo yao ya
damu yanaanza kushuka katika kiwango ambacho wanaweza kuachana kabisa na
matumizi ya dawa.
Dr.Batmanghelidj
anasema, ikiwa watu watajishughulisha na mazoezi hasa mazoezi ya
kutembea kwa miguu, watakunywa maji halisi zaidi na kuongeza chumvi
(siyo sodiamu) kidogo ya ziada kwenye vyakula vyao, mashinikizo yao ya
damu yatarudi katika hali yake ya kawaida.
Swali
la kujiuliza; Ni zaidi ya miongo minne sasa tangu tulipoambiwa kula
vyakula vyenye chumvi kidogo ili kuepukana na shinikizo la damu, kwanini
sasa Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu inazidi kuongezeka?.
Narudia
tena, mwili unapoanza kuishikilia chumvi, hufanya hivyo ili kuhifadhi
maji, toka katika bahari chumvi hiyo ya nje ya seli, maji huchujwa na
kutumika wakati wa mahitaji ya dharura.
Maji
na chumvi kwa pamoja vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake
ya kawaida. Kuikimbia chumvi kunasababisha shinikizo la damu (BP) kuwa
sehemu ya maisha yetu, tutapata nafuu, lakini baada ya muda mfupi hali
hurudi ileile na pengine kuwa watumwa wa kuchagua kula hiki au kile.
Tofauti
na zamani ambapo shinikizo la juu la damu lilipokuwa ni ugonjwa wa watu
wanene au wenye uzito uliozidi pekee, siku hizi wanene kwa wembamba,
watoto kwa wakubwa wanaugua BP.
Mambo 11 mhimu ya kuzingatia unapokuwa na shinikizo la juu la damu:
- Ongeza kiasi cha unywaji maji na chumvi kila siku
- Kula nyama isiyo na mafuta mengi
- Ongeza kula vyakula visivyokobolewa
- Kula zaidi matunda, mboga za majani, karanga na maharage
- Punguza vyakula vya viwandani vinavyoongezwa sukari nyingi
- Punguza vyakula vyenye lehemu au kolesteroli nyingi
- Acha kuvuta sigara na tumbaku za aina zote
- Acha kunywa pombe
- Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito unaopaswa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
- Punguza mfadhaiko au stress
- Fanya mazoezi ya viungo hasa mazoezi ya kukimbia kila siku na kama kukimbia kimbia huwezi basi kutembea kwa miguu masaa mawili kwa siku inatosha kabisa
No comments