UNACHOTAKIWA KUFANYA UNAPOKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA.
kujamiiana ni tatizo linalowasumbua wengi nchini. Ni maradhi kwa upande mwingine yanayosababisha ugumba na hata mifarakano na kuvunjika kwa ndoa.
Wakati huo utafiti huo ukiweka bayana hilo kutokana na tatizo la uzazi au kukoma kwa hedhi, tafiti nyingne zinaonyesha kuwa karibu robo tatu ya wanawake hawafikii kilele cha tendo hilo au wanapata maumivu.
Kutibu tatizo la sonona na wasiwasi.
Tiba ya vichocheo (homoni)
Masanja na mke
wake Saumu wameishi kwenye ndoa kwa miaka kumi sasa. Hapo awali, kila
kitu kilikuwa sawa katika uhusiano wao, lakini katika miaka ya karibuni,
Masanja amekuwa hana matamanio tena na Saumu
Wakati huo utafiti huo ukiweka bayana hilo kutokana na tatizo la uzazi au kukoma kwa hedhi, tafiti nyingne zinaonyesha kuwa karibu robo tatu ya wanawake hawafikii kilele cha tendo hilo au wanapata maumivu.
Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kukosa hamu ya tendo la ndoa kunatibika, iwapo hatua muhimu na za msingi zitachukuliwa.
Ni vyema kufika mapema katika huduma za afya ukiwa na mwenza wako kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Nini suluhisho la kukosa hamu ya kujamiiana
Kwanza kabisa,
inashauriwa kitaalamu kubadilisha mfumo wa maisha kwa mfano, kubadili
ratiba za kazi, matembezi au ratiba za wenza.
Kingine ni
kufanya mazoezi mara kwa mara kwa sababu mazoezi huongeza ufanisi,
lakini pia kupunguza uzito na humfanya mtu kuwa na umbile zuri, furaha
na kuongeza ufanisi wakati wa kujamiiana.
Kupunguza
msongo wa mawazo kwa kukubali kwamba tatizo lipo baina ya wanandoa na
hivyo kutafuta suluhu pamoja na kuacha ugomvi. Matatizo ya kimaisha
lazima yatafutiwe ufumbuzi.
Kufanya mazoezi
ya misuli ya kiuno kwa kufanya kama unazuia mkojo wakati unahisi haja
ndogo na kuhesabu kutoka moja hadi tano, baada ya tano pumzika na halafu
rudia. Haya mazoezi (kegel exercise) huongeza uwezo wa kujamiiana kwa
wanawake
Kubadilisha mfumo wa maisha kwa wapenzi
Zungumza na
mwenza wako – Malumbano na matatizo ni vitu vya kawaida katika uhusiano
wowote, ni vizuri kwa wenza kukaa pamoja na kuzungumza matatizo yao,
kuwa wa kweli, waaminifu, kuaminiana, kujaliana na kuzungumza juu ya
tendo la ndoa kwa pamoja.
Ni vizuri kila
mmoja kuainisha vitu anavyopenda na asivyopenda kufanyiwa wakati wa
kujamiiana. Pale inapotokea mmoja hajapendezwa au kufurahishwa na
uwajibikaji au ufanisi wa mwenzie basi
hana budi kutumia lugha nzuri kutafuta kiini cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi.
hana budi kutumia lugha nzuri kutafuta kiini cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi.
Weka mazingira mazuri na muda wa kufanya tendo la ndoa na mwenza wako ili mpate kudumisha uhusiano wenu.
Ongeza msisimko
katika uhusiano wenu kwa kujaribu aina au staili mbalimbali wakati wa
kujamiiana, kubadilisha muda wa kufanya mapenzi (sio usiku tu hata
asubuhi, mchana) au sehemu tofauti na ile mliyoizoea wakati wa kufanya
mapenzi (sio kila siku kitandani).
Kupata ushauri
nasaha kutoka kwa wataalamu wa mambo ya uhusiano, ndoa na hata madaktari
wa magonjwa ya akili kwani hawa ni weledi zaidi katika kazi yao.
Tiba ya dawa
Kutibu ugonjwa ambao ni kiini cha tatizo hili – Kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya zinaa nk.
Daktari kumbadilishia mgonjwa dawa zinazosababisha madhara kama ya msongo wa mawazo na sonona.
Kutibu tatizo la sonona na wasiwasi.
Kutumia dawa au vilainishi vya ukeni wakati wa tendo la ndoa kwa wale wanaopata maumivu au kupunguza uke kuwa mkavu au kuwasha.
Tiba ya vichocheo (homoni)
Dawa za
kitaalamu za kuongeza hamu au nguvu atakuandikia daktari baada ya
kufahamu kiini cha tatizo. Haishauriwi kutumia bila ushauri wa daktari
kwani dawa hizi zina madhara.
Ikumbukwe ya
kwamba vyakula hivi sio tiba mbadala bali husaidia tu kupunguza ukubwa
wa tatizo hili la kupungua au kukosa hamu ya kujamiiana na kuboresha kwa
wale ambao hawana tatizo hili na hivyo kudumisha uhusiano.
Kitunguu swaumu
– Kitunguu swaumu kina kemikali ambayo huongeza mzunguko wa damu kwenda
kwenye uume, huongeza hamu ya kufanya mapenzi na utolewaji wa mbegu za
kiume.
Habat al soda –
Mafuta, mbegu, au unga wa habat soda kama wengi wanavyoiita na ambazo
zimetumika kwa miaka mingi sana kupunguza tatizo hili na waandishi wengi
wa tiba ya nguvu za kiume wameeleza umuhimu wake. Tumia kidogo kwenye
chai au maji ya uvuguvugu mara mbili kila siku. Mbegu hizi hupatikana
kwa wingi katika nchi za asia kama Saudi Arabia, Syria, Iran, Dubai
(UAE), na hata Misri, Tanzania-maeneo ya pwani hupatikana.
Giligilani – Hii huchochea hamu ya tendo la ndoa kutokana na uwepo kwa wingi wa kichocheo aina ya androsterone.
Ndizi – kuwepo
kwa wingi kwa kimeng’enyo aina ya ‘bromelain’ na madini ya potashiam,
huongeza msisimko wa tendo kwa wanaume. Potassium pia hupatikana kwenye
tikiti maji ambalo pia lina kemikali aina ya ‘arginine’ ambayo huongeza
wingi wa damu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kusimika
kwa uume.
Parachichi –
Huwa na kiwango kikubwa cha madini ya folic acid ambayo huvunjavunja
protini. Vitamini B6 kwenye parachichi huchochea kutengeza vichocheo vya
kiume kwa wingi.
Mayai – Mayai
yana kiwango kikubwa sana cha vitamini aina ya B5 na B6, ambazo husaidia
kuleta usawa wa viwango vya vichocheo mwilini na kupunguza msongo wa
mawazo.
Nyanya – Zina
kiwango kikubwa cha virutubisho aina ya bio-active phyto-nutrients,
lycopene, na beta carotene ambazo husaidia kuleta damu kwa wingi kwenye
uume na hivyo kusaidia kusimika kwa uume
‘Chocolate’ – Ina kiwango kikubwa cha kemikali ambazo huongeza hamu ya tendo.
Vitamin A –
Husaidia katika kuweka usawa wa vichocheo vya mapenzi. Vyakula venye
wingi wa vitamin hii ni pamoja na karoti, maini,tikiti maji, spinach,
maziwa nk.
Vitamin B complex – Huongeza kiwango cha kichocheo cha testerone ambacho
husaidia katika kuongeza ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume na
wanawake. Vitamini B complex hupatikana kwa wingi kwenye ndizi, viazi
tamu, lentils mboga za majani, parachichi, mayai, samaki aina ya jodari
(tuna), bata mzinga, maini nk.
Mdalasini na Asali– Mchanganyiko wa vitu hivi viwili husaidia sana katika kuongeza ufanisi kwa wale wenye tatizo hili.
No comments