Unahisi Umefungwa Kwenye Mahusiano Mabaya?


Bila uhuru na mipaka ndani ya mahusiano  unaweza kuzimia wakati wowote hasa kama wewe  huwezi kupigana na maadui wadogo wadogo ndani yako wanaokupigia kelele nyingi ambazo hazina maana.

Unahisi Umefungwa Kwenye Mahusiano Mabaya?

Unahisi kama kufungwa  ndani ya mahusiano na huwezi kutatua tatizo?  Bila shaka ,  kuhisi kwako na hali ya akili yako kufungwa na giza kubwa . Hakuna mtu anayependa  kuharibu mahusiano. Watu wengi duniani kote hubaki ndani ya mahusiano kwa sababu mbalimbali, ingawa anaweza kuwa anahisi kuzimia.  Wengi hukosa uchaguzi kwa kuhofia baadhi ya sababu.

Watu hutoa sababu nyingi sana za kubaki kwenye mahusiano  hata kama anaumia kwa kiasi kikubwa hata kusababisha kifo. Hasa katika kujali watoto. Kuna mwanaume mmoja alikufa kwa sababu ya mawazo mengi kutokana na matatizo ya mke wake ,  Pesa nazo ni tatizo la wengi huwafanya watu wawe vipofu, anaamua kubaki kwa sababu ya pesa japo anaumia.  Wengine husikia aibu kwa jamii kwa kushindwa kuvumilia kwenye ndoa. wengine wanaogopa kubaki peke yao. Hata wengine kuhisi hawataweza kuolewa au kuoa tena, Ni kweli kama umeoa   huruhusiwi kuoa au kuolewa kama mwenzi hajafa.  Mitindo ya maisha mara nyingi inasababisha watu washindwe  kuondoka mahali ambapo anaumizwa. Wengi husema kuwa majani hayawezi kuwa ya kijani kila siku. Kuamini wamezeeka  hawataweza kupata mtu wa kuwapenda tena , Hofu imewajaa watu kwa mambo mengi .

Hofu Ya Ufahamu

Pamoja na sababu nyingi,  Zipo za kweli, na zina maana kubwa, kufahamu kuwa umefungwa, pia kuogopa matengano ndio yanafanya watu wengi kujiona kama wamejifunga wenyewe bila kuwa na uhuru. Lakini pia kuepuka upweke. maana upo upweke mbaya unaosababisha vifo kwa watu wengi.

Wanawake ambao wako katika tatizo hili , hutafuta marafiki  ambao kila mara hukaa nao ili kuongea mambo mengi na kufarijiana katika mapito walionayo. wanaume wao huamua kuwa bize kazini, lakini ndani hakuna mahusiano mazuri.  hii yote ni  kazi bure maana kama upweke bado upo pale pale.

Hali kama hii sio nzuri maana huwezi kuwa mfano mzuri kwa watoto. bora kujitahidi kutafuta suluhisho ili kuweza kuishi vizuri kuliko kuteseka. Uteseke hapa Duniani na ukifa huenda utaingia motoni. Tafuta Amani ifuate kwa bidii yako yote.  Tafuta maarifa ya Neno La Mungu Utapona.

Kuna watu ambao hawakuwahi kuishi peke yao, walitoka tu chuo wakaolewa, tangu wakiwa watoto walikuwa na familia  iliyowapenda sana,  na wakakutana na wapenzi walioonyesha kuwapenda sana , lakini kumbe akili ya huyo mwenza ilikuwa bado haijajua chochote kuhusu ndoa. Aliamua tu  kuoa ili apate raha ya mwili na hisia zake binafsi. watu hawa hawakuwahi kujifunza kukaa peke yao, ni ngumu  kuamua  maamuzi.

Matokeo yake anajikuta ghafla amepata kamba ya kukazia nira yake  (yaani mtoto ) wa kwanza na wapili na kuendelea, atawezaje kutoka hapo alipo. Atamwachia nani huo mzigo. kuna kuomba talaka kweli hapo? Fikiria kwa makini.  Pamoja na watoto bado woga wa peke yake utakuwepo, woga wa kupoteza Muda.

Kukataa

Kukataa kwa matatizo, pamoja na uathirika, ni tatizo lingine linalowafanya watu wakwame ndani ya mahusiano. Kupuuzia, kutoa sababu, kujaribu kutaka kumbadilisha mtu utakavyo, kutazamia kuwa ipo siku kutakuwa na wakati mzuri, kamwe bila kushughulikia mapema nyakati nzuri hazitakuja. badala yake utalimbikiza maumivu mengi, bora kukubali kosa na kurekebisha wakati huo huo, hicho kinaweza kusaidia  kuleta mabadiliko.

Kukosekana kwa uhuru.

Ukiwa huru unaweza kumwambia mwezi wako  chocote unachoona kinaleta shida kwenye maisha yako. Unaweza kumueleza hisia zako , unahitaji akufanyie nini. kukosekana kwa uhuru kunasababisha watu kutengana. utakuta upande mwingine  anataka  usalama  lakini upande wa pili anataka kuwa huru. Kitu kizuri ni kujitambua kwanza wewe kama wewe, unataka nini. Bila ya kuharibu upande wa pili. Bila ya hofu ya aina yoyote. Mifano ya uhuru wa kisaikolojia ;

1.Ukiwa peke yako huwezi kujisikia  mtupu au kama mtu aliyepotea.

2.Hausumbuliwi na vitendo au hisia za wengine

3.Unajali , huchukulii vitu kivyako tu

4.Ni mtu unayeweza kufanya maamuzi yako.

5.Thamani yako na maoni yako sio rahisi mtu mwingine kuingilia.

6.Uamuzi unaofanya ni wa mwisho sio wa kubahatisha.

7.Una msimamo, kama No ni No sio may be.

8 Unachagua marafiki kwa Hekima.

Kama huna hivi hutaweza kuishi vizuri kwenye mahusiano yako. utakuwa mtu wa kutaka kumfurahisha mtu huku ukiwa unaumia. Si nzuri.

Njia Ya Kutoka.

Anza upya kujichunguza wewe mwenyewe, Anza kubadilika wewe mwenyewe, utaona na mwenza wako anabadilika. Usitake kumbadilisha mtu kama unavyotaka wewe awe, badala yake kuwa wewe jinsi unavyotaka mwenzi wako awe. Chukua jukumu  la mabadiliko unayotaka. Anza na No kuondoka. Anza zoezi la kuweka mipaka ili kujenga ujasiri, jinsi gani ya kuongea maneno mazuri. Soma neno la Mungu mara nyingi. Kama hujui tafuta msaada ufahamu jinsi gani ya kusimamia neno la Mungu.

Kama unasikia kuhukumiwa, anza kujisamehe, samehe watu. Haiwezi kutokea mara moja , unahitaji juhudi ya kipekee. Hakuna lisilowezekana kama ukifanya maamuzi mazuri.

No comments