Unahitaji Msaada Kwenye Mahusiano Yako?
Unahitaji Msaada Kwenye Mahusiano Yako?Kuna mambo mengi yanayohusiana na tabia zinazoweza kuleta afya ndani ya mahusiano.
Hasa katika suala la Mtazamo chanya. Kwa haraka unaweza kufikiri ni kuhusu uaminifu, upole, heshima, wema, upendo, furaha, amani ukarimu na aina zote pamoja na hisia, kiroho, na jinsia na vitu.
Yapo pia matatizo kama ya kubakwa, kufanya tendo kwa ajili ya kumridhisha mtu.
Kuna mambo mengine kama uchoyo, kutokujali, kuwa na upinzani, kutokuwa makini, vitisho vya kwenye mahusiano, Mfano ;Mtu kujiona yeye ni zaidi ya mwenzake, kiuchumi, umaridadi. Kutambua kuwa huna furaha na mwenza uliyenaye, Kusahau hisia zako na kutaka kujua hisia za mwenza wako. Kutaka mwenza abadilike tabia zake na kujisahau wewe mwenyewe kuwa ndio chanzo cha mabadiliko.
Mara nyingi iko hivi , Silika za watu wengi hufikiri kuwa wapo mahali sahihi na kujiona kama wenza wanawajali kumbe sio. Kwa sababu unaweza kufikiri unapomkumbatia mtu na kumkiss anapofika tu kutoka mahali , kwamba amefurahia kumbe sio. Kitu anachotaka kujua kutoka kwako ni kuhusu kumjali. Je unamjali?
Nataka nikuonyeshe ndani ya makala hii kwamba mwenza wako anataka kujua kama unamjali . kujali mtu inatoka ndani ya moyo wa mtu. Mfano; Unapotafuta Muda kwa ajili yake, unapotafuta zawadi yoyote kwa ajili yake, inaonyesha jinsi gani yuko ndani ya fikra zako , jinsi gani unamjali unapompigia simu kama yupo mbali.
Ukitaka ufanyiwe vizuri , anza wewe kuwafanyia wengine kama vile unavyotaka ufanyiwe
Utavuna kile ambacho utakipanda, pamoja na sifa zote zile nzuri ambazo nilizitaja hapo mwanzo unahitaji kuwa nazo.
Ni vizuri kutambua mapema kuwa mahusiano yako umkabidhi Mungu. maana yeye ndiye mwanzilishi wa mahusiano. Usitumie akili yako , hutaweza. Mwambie Chanzo.
Kama kuna majira ya masika pia lazima utambue kuwa kuna majira ya kiangazi. Nikiwa na maana kuwa kama Upendo upo , lazima kutakuwepo na chuki pia. kama kuna kuzaliwa , pia kuna kufa. Usitegemee kila siku utakuwa na raha tu ndani ya mahusiano. Jifunze kuishi katika kila majira.
My-Post-3 Unahitaji Msaada Kwenye Mahusiano Yako?Muombe Mungu akupatie Tunda la Roho, Na usitake tu zile sifa za juu ambazo nimetaja awali, hazitaweza kukufaa.
Omba Upendo wa Kristo, Furaha ya Kristo, Amani ya Kristo, Wema wa Kristo, Heshima ya Kristo, Hekima Ya Kristo, Ufahamu wa Kristo, Maarifa ya Kristo, Uaminifu wa Kristo.
Usipende kuiga mahusiano ya watu ambao sio Model wako. tafuta model wa mahusiano yako. Awe ni mtu anayempenda Mungu.
Kufahamu madhaifu ya mwenza wako na kuyavumilia. maana hata wewe una madhaifu yako . hakuna mtu asiyekuwa na madhaifu. utatafuta sana hutaweza kumpata .
Kaa ndani ya familia ya Mungu . Jifunze kwa Yesu, upole, unyenyekevu, wema, utapata raha nafsini mwako maana nira ya Yesu ni laini na Mzigo wake ni mwepesi.
Ukiona unakosa Amani , mwendee mpe Huzuni , chukua Furaha. Ukiona Upendo Unapotea , Kimbia kwake Ongeza Upendo wa Kristo ndani yako.
Mahusiano mazuri ni kutafuta muda wa kuwa pamoja mara kwa mara, uwepo wenu ni msingi, kuambiana vitu vya kweli, kufanya uchunguzi mbalimbali, kupeana mawazo kwa kuandika, mazungumzo mazuri, kuandaa miradi pamoja na kupeana matumaini.
Kama mara nyingi mnafanya hivi , kila siku utaona maisha yako ndani ya macho ya mwenza wako. Utaona unaweza kutimiza kusudi lako, utaweza kutambua uwezo ulionao, Kwa kuwa kutakuwepo hali ya kujenga umuhimu wa kumjali mwenza . wote mtajisikia vema . mapenzi ya Mungu yatatimia kwenu.
No comments