USIJIDANGANYE MWANAUME HAKOMOLEWI!
Haya weee, mimi nipo poa unashangaa nini
kujibu majibu ya kisasa, mbona hujishangai wewe mama mtu mzima
kushindana kwenda utupu na binti yako, sasa likiharibika nani amkanye
mwenzake. Hebu nipishe huko ushaanza kukunja domo kama dege lililokosewa kumwagwa. Umenuna umecheka habari ndiyo hiyo.
Leo, shoga yangu nazungumza na wewe
mwanamke usiye na haya usiyejua wakati gani wa kumkomoa mumeo, jamani
wanawake wengine sijui tumerogwa na mchawi aliyeturoga kaugua
wendawazimu sijui nani wa kutuponya.Kuna kitu kimoja jana kilinikera na
kunifanya niwarudishe kwenye unyago, nikiwa nakwenda zangu mjini
nilipanda kwenye daladala na kukaa siti ya nyuma, mbele yangu kulikuwa
na wanawake wawili waliokuwa wakiongea mambo ya ndani bila aibu.
Kutokana na maongezi yao ndiyo maana
nikajiuliza kama waliochezwa wamesahau mafunzo ya unyagoni itakuwa wewe
unayewekwa masaa mawili mbele ya watu eti Kitchen party! Hivi kwanza
wewe mwanamke, eeh jamani aibu umeiweka wapi kufikia hatua ya kuyasema
maneno ya ndani mwako ndani ya daladala bila hata kugongwa na mshipa wa
aibu.
Nilimsikia akisema eti alikorofishana na
mumewe na kumsubiri kitandani ndipo alipomkomoa kwa kumkaripia
alipomgusa na kumwambia amkome.Weweee mwanamke ndivyo mlivyofundishwa
unyagoni kumfanyia mumeo kitandani pale mnapokosana. Unajua madhara ya
kumnyima mumeo kata ya maji ukweni akiwa na kiu kikali?
Kibaya zaidi upumbavu ulioufanya
unamweleza rafiki yako, pengine hata hajui ndoa ni nini, majibu yake
mepesi. “Shoga tena mkomeshe, wanaume wamezidi.”Hizi ndizo moja ya
sababu za kumfanya mumeo atembee na house girl, pengine kafikisha umri
wa kutumwa sokoni akarudi.
Wewe umekataa pengine wiki ukijua
unamkomoa, mwanaume hakomolewi shoga, tupo day worker kibao tunatafuta
kazi hata ya masaa, telekeza gari day worker alikamate kama tajiri
atakukumbuka.Nataka tuzungumze kitu kimoja kwako wewe mwanamke, ni kosa
kufungua mahakama kitandani, mwenzio anataka wewe ndiyo unaanza
“unajua,” ajue nini mpe haki yake mashtaka baadaye.
Shoga, unamnyima mumeo haja zake
akamalize wapi, akipata nyumba ndogo inayomjali uanze kupiga kelele.
Hebu wanawake tuache akili za punda wa dobi, mumeo akikukosea pataneni
lakini siyo kumpa adhabu ya kumnyima chakula cha usiku.Kwa leo ni hayo
tu.
No comments