USITHUBUTU: Mama Amepitia Mahusiano Mabaya Na Wewe …Hapana
Mama yako anaweza kuwa amepitia mahusiano ambayo hayakustahili kupitia. Hakujiona kuwa anastahili kupata furaha na amani kwenye mahusiano yake,
Kwa hio aliachia mtu amtese, amdharau, amtumie isivyo, aliruhusu sumu hio iingie kwenye mahusiano yatawale maisha yake na alikuwa akiyaangalia jinsi hiohio.
Hata kama utamchukia mtu aliyemuumiza, lakini bado utaangalia na upande wa mama yako kuwa alikuwa hana ufahamu wa kutosha , Fahamu kwamba kwa kutokuelewa kwake ndiko kulileta maumivu hayo. hakujua thamani yake, upekee wake, nguvu yake na ubora wake. Kitu ambacho kila mtu angekiona kwake ni ujasiri .
Lakini kama ukitazama mwanamke mwenye nguvu, smart, mzuri halafu amekubali kukaa kwenye mahali ambapo haonyeshi thamani yake, inakufundisha somo. Inakufundisha kuinua kiwango chako, Inakufundisha kuondoa hali ya kukosa usalama, Inakufundisha kufikiri zaidi kwenye maisha yako.
Kuna mtu mwingine kwa sababu ya kuona mateso aliyopata mama yake, Sasa yuko huru. Kuanzia kwenye umri wake mapema, hataki kutafuta mtu wa kumpa furaha, Upendo ,Amani, anataka awe navyo yeye mwenyewe, Hataki kusubiri.
Kwa sababu ya mateso ambayo amepata mama yako unaweza kujaribu na kuona mahusiano ambayo sio sahihi , ambayo utaonyeshwa na bendera nyekundu, mtu mdanganyifu, anayekulisha sumu, utamfahamu aliye mkweli na mtu asiyeaminika.
Unaweza kutafuta tu mtu mwingine ambaye anaishi katika mahusiano mazuri na ukajifunza kwake. lakini kipo kitu ambacho nataka ukijue. Mahusiano mazuri yanaanza na wewe mwenyewe. Ukiwa na mausiano mazuri ya kipekee, na ukiwa na mahusiano mazuri na Mungu. Utapata uongozi wa kiMungu katika maisha yako. Hakuna kitu utakachokosea.
Fikiri na kutazama huko nyuma, Mama alikuwa na mahusiano gani na Mungu, mbali na hio je Alijua kuwa ni lazima kuwa na mahusiano yake mwenyewe? Jibu ni Hakujua. Kwa hio wewe sasa ni mtu ambaye unafahamu. Unauelewa. Una taarifa za kutosha . Kama huna anza kutafuta taarifa nzuri za mahusiano kabla ya kuingia kwenye Jam.
Kila kitu kinahitaji maandalizi ya kutosha. Lakini ukikurupuka , ndio utaishi kama mama alivyoishi kwa kutokufahamu. Usiseme Mahusiano ni mabaya. Mahusiano ni mazuri sana. Ndoa ni nzuri. Hata siku moja usiseme hicho kitu . Kama umewahi kusema anza TOBA mapema kabla hujaamua kuingia huko. Usijifungie mlango kwa maneno ya kinywa chako.
Uzima na mauti upo katika kinywa cha mtu. uwe makini na maneno unayoongea kila siku.
Watu wengi wanayaishi yale walioongea wakiwa wadogo. Maisha ya mtu yanatokana na mawazo yake.
Share kwa wingi ili kusaidia wengine.

No comments