JINSI YA KUMPAGAWISHA MWANAUME KITANDANI
Mwanamke yeyote anayeweza kumfanya mwanaume kuwa mtu wa furaha anastahili pongezi kubwa sana kwa kazi nzuri unayofanya hasa kujitoa ili kuhakikisha ndoa yake inakuwa na afya kila siku.
Wapo wanaume (siyo wote) hata kama mwanamke anajitahidi kwa nguvu zote na ujuzi wake wote kumfurahisha, bado mwanaume haelewi somo anaendelea na maisha yake kama anavyojua yeye, hana muda wa kusikiliza kitu chochote kutoka kwa kiumbe anaitwa mwanamke.
Binafsi namshukuru Mungu na pia nakiri kabisa kwamba ni moja ya wanaume walio barikiwa duniani kupata au kuoa mke ambaye anajitahidi siku zote kuhakikisha ninakuwa mwanaume mwenye furaha; kwani naziona juhudi zake kwa maneno na matendo.
Ili kuchambani kuwe na furaha ni muhimu furaha kuanzia nje ya nyumba kabisa then sebuleni na kumalizia chumbani.
Jambo la msingi katika mahusiano ya ndoa; kila mwana ndoa anatakiwa kufanya lile ambalo na yeye anapenda kufanyiwa.
Jitahidi sana kutenga muda kwa ajili ya mume wako kwani maisha ni mafupi sana kuishi kwa kubishana, hasira, gubu, donge, kusemana na kulaumiana hakuna maana zaidi ya kupoteza muda kwani katika vita ya mume na mke anayepata hasara wa kwanza ni ninyi wenyewe then watoto.
Muhimu ni kuishi kwa kupeana mambo mazuri sasa hivi kwani huwezi kujua kesho kitatokea nini, life is too short so live at fullest.
Anza kwanza wewe mwenyewe mwanamke kuwa mtu wa furaha thenmwambukize na yeye, hapo mtakuwa mmefungua mlango wa furaha ya nje na ndani ya sita kwa sita.
Furaha ya kwanza kwa mwanaume ni wewe mwanamke unavyoonekana.
Idara ya mwonekano, urembo, uzuri ambao unakufanya uwe mwanamke.
Mwanaume siku zote anapenda sana mwanamke ambaye anapendeza (likable) jitahidi kujiweka safi muda wote,
kwa nini uwe rough,
mchafu, unanuka, hujipendi,
mzembe, hujipambi,
unakuwa kama huishi dunia ya leo.
Kujipamba na kupendeza ni asili ya mwanamke na wanaume huvutiwa na jinsi mwanamke unavyoonekana.
Ni vizuri kumuonesha mume wako jinsi unavyompenda, jinsi unavyomjali na jinsi unavyomuhitaji na kujitengeneza vizuri ni moja ya njia ya kuonesha hayo.
Usitegemeee mwanaume atapata furaha chumbani kama mwanamke mwenyewe ndo huna mpango na uzuri wa mwili wako.
Je mwanaume kwa chakula unaweza kumpa furaha?
Ni kweli tupu, Unaweza kumfanya mwanaume ajisikie raha sana na furaha kubwa hadi chumbani hasa kama unajua jinsi ya kumpa mlo wa uhakika (chakula anachokipenda) na kama Mungu amekubariki kupika vizuri basi hiyo ni silaha muhimu sana.
Jaribu angalau kwa weekend mtengenezee chakula maalumu ili na yeye awe moja ya wanaume wenye furaha hiyo hapa duniani.
Hivi umewahi kupanga mkakati wa kuhakikisha kuna siku mume wako anakuwa ni mtu pekee mwenye furaha duniani?
Kama bado sasa ni wakati wake!
Hata kama unajua wewe kupika chakula kitamu ni kilaza, bado unaweza kusoma vitabu au kujifunza then ukampikia mumeo.
Wapo wanawake wanajua kabisa mume wake anapenda chakula aina fulani na anajua kabisa akimpikia hicho chakula mume huwa anafurahia lakini who cares, miezi inapita mume hajapata hicho chakula anachokipenda na wakati huohuo mwanamke ana lalamika eti mume siku hizi hanipendi na chumbani mambo si moto, anza kwaza kuwasha moto jikoni then usubiri na yeye awashe moto wa chumbani; thubutu utavuna ulichopanda!
Kama unataka chumbani kuwe na furaha lazima na wewe afanye sehemu yako kwa ajili yake.
Wapo wanawake miezi na miezi, mwaka hadi mwaka kila siku chakula anapika house girl, najua wanaume tunafahamu kabisa kwamba wake zetu mna majukumu makubwa, ila kitendo cha kupikiwa na msichana wa kazi mwezi mzima, mwaka mzima na wewe upo huwa wanaume hawafurahii.
mwanaume hujisikia furaha sana siku akila chakula alichopika na mke wake.
Utampaje furaha huko chumbani?
Ukisha kuwa umemtengenezea mazingira ya furaha nje ya chumbani, basi lazima hata chumbani atakuwa na furaha tu kwani kazi muhimu umeifanya, kilichobaki ni kuangusha mbuyu kwa shoka moja tu.
Wakati unaingia chumbani tu achana kabisa na mawazo yoyote hasi kuhusu yeye, achana kabisa na mambo usiyoyapenda kuhusu yeye na badala yake jiweke huru na wazi kabisa zaidi jimwage au jiachie kabisa.
Usimfiche kitu chochote unataka kutoka kwake, yaani uwe wazi na jisikie huru fanya kile yeye huwa anapenda hapo hakuna mipaka hakuna kuogopa kufanya kitu, hapo ni uhuru wa ajabu. Mpende kwa maneno,
kwa matendo,
kwa kunusa,
kwa kuonja kwa kugusu na
kwa hisia zote.
Usijilaze kama gogo mbele ya mume wako na kumsubiri yeye afanye kila kitu, participate fanya kile kimekuleta kutoka kwa wazazi wako, kwani kwa wazazi wako ulikuwa huvai, ulikuwa huli, si umemfuata kwa sababu yeye ndiye peke yake anaweza kukupa huduma ambayo wazazi wako hawawezi kukupa, yeye peke yake anaweza kuuhudumia mwili wako na feelings zake, ndiyo maana inabidi uchangamke, ujishughulishe na kuhakikisha unapata kile unahitaji kutoka kwake na kwa kuwa wote mna furaha na mnafanya kile mnapenda basi hapo kutakuwa na furaha kuu.
Mwanamke lazima uwe mtundu!
No comments