MAMBO 10 YA KIZINGATIA KUJIKINGA NA MAGONJWA.


Hivi ulisha wahi kukaa na kujiuliza ni kwa nini unaugua? Pia ulisha wahi kutamani ni kwa nini usiugue? Basi kama wewe hupendi kuugua ugonjwa wowote ule nia yako tumeigundua sisi Hapa AFYAKONA na yafuatayo ni mambo 10 ambayo kama ukiyazingatia utaweza kuepukana na maambukizi ya Magonjwa mbalimbali na pia Afya yako itaweza kuimarika nayo ni kama;-

Kwanza kabisa kuhakikisha Mazingira unayoishi (yanayokuzunguka) yako safi na salama mda wote.
Chakula chochote unachokula hakikisha kipo katika hali ya usafi kikiwa kimepikwa katika hali ya usafi pia na kimeiva vizuri.
Kuzingatia usafi wa Mwili, Mavavi, na Malazi.
Kuhakikisha Mikono yako inakuwa katika hali ya usafi mda wote (kunawa mikono na sabuni kila na baada ya kula, kutoka chooni, kabla ya kuandaa chakula, baada ya kushikana na watu mbalimbali kama vile kusalimiana, baada ya kufanya usafi wa ndani na chooni, baada ya kumtawaza na mtoto na pale mikono inapokuwa imechafuka   kutokana na shughuli yoyote ile.)
Kuwa na mpenzi mmoja na kutumia kinga katika kila tendo la Ngono.
Kuwa na utaratibu wa Kupima Afya yako mara kwa mara hata kama hauna dalili zozote za Magonjwa.
Kuhakikisha unapata mlo kamili (balanced diet) na kwa mda maalum.
Kupata Chanjo ya Magonjwa mbalimbali.
Kwa akina Mama Wajawazito kuhakikisha una hudhuria kliniki mapema na pia kujifungulia katika kituo cha Afya chini ya uangalizi wa wataalamu wa Afya, pia kuhakikisha mtoto anapata maziwa ya Mama kwa mda usiopungua mwaka mmoja na nusu huku akipokea chanjo zote anazostahili kuzipata kwa mda maalum.
Kuhakikisha unalala siku zote katika Chandarua safi chenye dawa na kisichokuwa na matundu hata kama hakuna dalili za kuwepo kwa Mbu katika mazingira hayo.
N.B;- Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ukiyazingatia unaweza kuishi ukiwa na Afya bora na maisha ya raha pia unaweza kuokoa gharama ambazo unaweza ukazitoa pindi unapokua umeugua badala yake hiyo pesa ukaitumia katika shughuli nyinginezo za kimaendeleo kingine kikubwa zaidi utaweza kuishi maisha marefu sana hapa Duniani. “Nani asiyependa kuishi kwa amani akiwa na afya njema? Jibu ni kwamba hakuna Basi ni vyema ukaanza kuzingatia hayo kuanzia sasa”.

No comments