Mambo Ya Msingi Unapotongoza Mwanamke Katika Kikundi cha wanawake wengi,kamwe hachomoki
Kutongoza ni sanaa ambayo inahitaji mmoja kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili aweze kuwa na ustadi ambao unaweza kumnufaisha au kumsaidia mhusika wakati ambapo anakabiliwa na tatizo la kumshawishi mwanamke. Ijapokuwa kuzijua sanaa hizi dhidi ya wanawake haitaonekana kuwa na ustaarabu katika jamii, kila mwanaume ana haki ya kuzijua na kutambua mbinu hizi.
Kitu cha kwanza ambacho unapaswa kujua ni kuwa kutongoza si matumizi ya mistari na miondoko ya mwili pekee bali pia ni subira. Kutongoza mwanamke kutachukua muda mwingi kutoka kwako hivyo unahitajika kuwa na imani. Kwa mfano kabla ya kuchukua hatua ya kuapproach mwanamke lazima upime manufaa na hasara ambazo zitakuja iwapo utaamua kutangamana na mwanamke ambae unakusudia kuwa naye.
Ikija swala la kumtongoza mwanamke katika kikundi cha watu, haya hapa ni baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuwa nayo wakati unapokabiliana na windo lako.
#1 Kumsifia
Kama umetoka out hadi kwa klabu na marafiki zako halafu ukamwona mwanamke unayemtamani akiwa katika kikundi, muapproach na umuagizie kinywaji na uwe mkweli na mhakika wakati unapomsifia kuhusu umbo lake na nguo alizovalia. Weka katika akili yako kuwa mwanamke anapenda kusifiwa kwa nguo alizovaa, hairstyle yake, macho yake, ucheshi wake na pia marashi aliyoyapaka. Pia, hakikisha kuwa unaspend muda mwingi zaidi hata kama klabu inaenda kufungwa. Kama umeongea na mwanamke huyu usiku huo, hakikisha kuwa unamwambia kuwa umependezwa na kuspend muda na yeye.
#2 Jiamini
Confidence ni nguzo ya kila mwanaume ambayo anapaswa kuwa nayo wakati wowote ule. Mwanaume anayejiamini anatambulika haraka na wanawake. Hivyo lazima uwe na confidence wakati unapotangamana na wanawake. Hii inamaanisha kuwa lazima uonyeshe confidence mbele ya umati na pia uonyeshe kuwa una interest na yeye hata kama umezungukwa na watu. Confidence ni lazima kama unataka kumtongoza mwanamke. Usifikirie sana kuhusu jinsi utakavyompendeza kwa sasa lakini. Kwa kujionyesha wewe mwenyewe bila kujifanya mtu mwingine kutakusaidia zaidi kuliko kuwa muigo wa mtu mwingine ili uonekane mzuri.
#3 Kujieleza
Wakati unapomtongoza mwanamke katika umati, ni bora zaidi kuweka toni ya sauti yako chini na ambayo itavutia kadri uwezavyo. Hii haimaanishi kuwa unapaswa kumnong’onezea, la. Kile unachopaswa ni kuweka wazi sauti yako aisikie vizuri na mara kwa mara umuonyeshe tabasamu ambalo utalichanganya na mvutio wa macho yako. Pia wakati unapoongea onyesha ujuba na maneno unayoyatamka. Hii itamfanya akuone kuwa wewe una interest kwake na unataka kuendeleza aproach yako zaidi.
Wakati utakapokuwa umeuchukua muda wako kuongea na mwanamke na kumuonyesha kuwa uko interested na yeye, jaribu kutafuta ishara ambazo zinaonyesha kuwa pia yeye amevutiwa ama anahisi kama vile unahisi wewe. Ishara hizi utaziangalia kupitia miondoko ya mwili wake. Je anapinda mwili wake upande wako? Je kifua chake amekienua ili uone ukubwa wa matiti yake? Je anacheka mizaha yako hata kama haichekeshi? Kama umeona kuwa amevutiwa na wewe kupitia ishara hizi, basi rudi nyuma na umngojee yeye aanze kuchukua hatua. Hii ni njia hakika ya kumfanya amaintain interest na wewe.
No comments