Najua Unampenda, Lakini Yeye Anakupenda?
Kwa hio tambua hili
Haihusiani na upendo wako kwake
Ni kuhusu upendo wake kwako.
Wewe tayari unajua ni kiasi gani unavyompenda ndani ya moyo wako na jinsi gani unajisikia kuhusu yeye.
Jinsi gani anamiliki kila chembe ya moyo wako kidogo kidogo
Unafahamu hilo kupitia maumivu yako na machozi yako
Kila mara unapopigania uwe karibu yake na kuhitaji kusikia sauti yake nzuri, unahamu jinsi gani umependa kupitiliza.
Lakini hapana, Hii sio kuhusu upendo wa kumpenda yeye
Ni kuhusu upendo wake kwako.
Anakupenda na kutafuta muda wa kuwepo na wewe, anaumia anapokukosa kama wewe unavyoumia juu yake?
Je unamtazama kama yeye ndio Ulimwengu wako, Nyota ,Bahari na kila kitu katika sayari hii? Na yeye anakutazama kama wewe unavyomuona?
Unaona kitu chochote chenye matumaini ndani ya macho yake? Unaona Upendo ?
Sasa Kwa nini, Kwa nini bado upo hapo? Unajaribu kwa bidii kubwa
Unashikilia kwa nguvu sana?
Kwa nini usikubali hali halisi
Kwamba hakuna kinachoendelea .
Kwa nini usitambue
Kwamba kama ni kweli anakupenda wewe
Asingeweza kuacha kukufuatilia na kutaka uwepo wako kila mara.
Wakati unapokuwa una tatizo , Ulimwengu unapokupiga, usingeona madhara makubwa , angekuwepo karibu yako.
Na ungekuwa unasikia sauti yake nzuri ya dhahabu ikipita ndani ya moyo wako na kujibu simu zako alfu moja ulizopiga.
Tambua kuwa hastahili kupata upendo huo kutoka kwako.
Kwa hio usiingie kwenye sehemu ambayo hakuna chumba cha kukaa wewe. subiri utapata mahali pa kuweka upendo wako. yupo mtu anayestahili kupata huo upendo.
Usiogope . Unastahili kupata kilicho bora.
Toa maoni yako.
Kisha Subscribe kupata makala mpya kila mara.
Mungu akubariki.


No comments