UKWELI;Date Na Mtu Ambaye Unamwamini Asilimia Mia

alikiba-smanager-4-1024x682-1024x682 Date Na Mtu Ambaye Unamwamini Asilimia Mia
Date na mtu ambaye anaweza kuacha simu yake mezani na kwenda zake chumbani, na wewe huna muda wa kuigusa simu yake kwa ajili ya kuangalia meseji.
Akilini mwako unajua kabisa hakuna kibaya  kilichopo ndani ya simu yake, unafahamu kwamba hana tabia ya kumtumia mtu mwingine meseji, Unafahamu kuwa kipo chumba ndani ya moyo wake kwa ajili yako tu.
Date na mtu amabye hata akichelewa kutoka kazini , au kutoka kwa marafiki zake  usiku, na unakuwa huna wasiwasi naye.  Mtu unayejua kwamba hawezi kukusaliti, hata kama tumbo lake limejaa vinywaji, mtu ambaye anaweza kusema ukweli alikokuwa, kwa sababu hataweza kukudanganya kitu.
Date na mtu ambaye hata kama akiwatumia marafiki zake wa kike meseji hutaweza kuwa na wivu, hata kama atakuwa ni mzuri sana kuliko wewe. huna wasiwasi kwa sababu hawezi kukuibia  kutokana na uaminifu wa huyo mtu uliyenaye.  Kwa sababu utakuwa unajua kuwa alikuchagua wewe kwa sababu. utakuwa unatambua kama akikuambia hakuna kinachoendelea na mtu huyo.Unaelewa kuwa ni kweli.
Date na mtu ambaye hutaweza kuwa na ndoto ya kuwa atakusaliti. kwa sababu  unafahamu kuwa hataweza kukuumiza , kwa sababu ni wako na wewe wa kwake.
Mtu ambaye hutaweza kumuwazia mabaya anapokuambia kuwa ana safari kikazi, hutawaza itakuwaje huko aendako,  hutafikiria kuwa anaweza kutafuta mtu wa kuwa naye chumbani.
Date na mtu ambaye utamwamini kiasi cha kutosha  . Mtu mkweli. mtu muwazi, mtu muadilifu na  madhubuti.
Mtu ambaye hawezi kuona aibu kukupatia password ya emails zake, simu zake , account zake. mtu ambaye anaweza kukuachia computer yake utumie. mtu ambaye yuko tayari kushare kila kipande cha maisha yake na wewe  kama vile na wewe  ulivyokubali kufanya hivyo hivyo.
Date mtu ambaye hawezi kukufanya ujisikie kuwa hufai hata sekunde moja. mtu ambaye  hawezi kujilaumu kwa kuwa na wewe, mtu ambaye haoni ubaya kwako.mtu ambaye hatakuacha ufanye kitu ambacho utajisikia vibaya.  mtu ambaye atajiona kukamilika  akiwa na wewe na ukalifahamu hilo.
Mtu mwenye kufurahia kuvaa pete hata akiwa kazini au katika mazingira yote. Ambaye ataweka picha yako mezani kwake akiwa na wewe, kila wakati anatazama .mtu ambaye anajisikia furaha kukuita rafiki yake, mke wake  au mchumba wake.
Date mtu ambaye anakupenda. Mtu utakayemwamini. Mtu ambaye una uhakika hataweza kukuumiza.

No comments