USIFANYE MAKOSA HAYA....
Unapotafuta mwenzi wa maisha si suala la kubahatisha kama vile kuwa kwenye chumba chenye giza totoro na kuanza kutafuta sindano sakafuni bali ni suala la kuhakikisha kuna mwanga wa kutosha kupata kabla ya kuingia kutafuta.
Ukweli ni kwamba dalili za ndoa kushindwa huweza kujulikana mapema hata kabla ya ndoa kufungwa hasa kutokana na jinsi mwenzi alivyopatikana
1.USIKUBALI KUOANA HARAKA MNO.
Kuwa wachumba kwa muda mrefu huwezesha ndoa yenye afya.
Hapa unatafuta mtu wa kuishi nawe maisha yako yote ina maana utalala naye chumba kimoja maisha, utakula naye chakula maisha yote, utakuwa naye katika matatizo ya kifedha maisha yako yote, utauguzana naye miaka yako yote, mtakumbana na kukatishwa tamaa pamoja maisha yako yote.
Kuamua haraka haraka kuoana ni kujitengenezea risk kubwa.
2.USIKUBALI KUOANA WAKATI BADO UMRI MDOGO SANA.
Oa au olewa wakati kwanza wewe mwenyewe unajijua vizuri.
Pia hakikisha unamfahamu vizuri yule unaoana naye.
Kuanzia miaka 24 kwenda mbele ni umri mzuri kuoa au kuolewa.
Kuwa na umri mdogo maana yake bado hujatimiza mambo ya msingi kama pamoja na kukomaa kiakili kuishi kama mke na mume.
Tafiti zinaonesha ndoa stable ni zile ambazo wanandoa walioana wakiwa na miaka kuanzia 28.
3.USIKUBALI KITU CHOCHOTE, MAZINGIRA YOYOTE AU MTU YOYOTE KukuSUKUMA KUOLEWA.
Hakikisha umetuliza akili zako ndipo ingie katika biashara za kuoana.
Inawezekana unataka kuoana haraka kwa sababu uliachwa na mchumba mwingine, au unajisikia mpweke, au anahisi ukiolewa suala la uchumi litakuwa limepata jibu.
4.USIKUBALI KUMRIDHISHA MTU YEYOTE NA CHAGUO LAKO.
Ni wewe utakaye pata faida au hasara, raha au machungu, furaha au huzuni, utamu au kuumizwa na si muda mfupi bali hadi kifo kitakapowatenganisha.
Haina haja kuwafurahisha wazazi au marafiki, au mchungaji, au mchumba mwenyewe kwamba unaoa au unaolewa eti wawe very happy.
Hii haina maana kwamba hutakiwa kuwasikiliza katika ushauri wao kuhusu wewe kuoa/kuolewa bali hii ni ndoa ni yako a lifetime opportunity.
Wala usikubali mtu awaye yote akuchagulie au kukufanyia uamuzi hata kama anauzoefu namna gani.
Wewe ndiye unatakiwa kuwa na uamuzi wa busara hata baada ya kupokea ushauri wa kila aina kutoka kwa watu tofauti
5.USIKUBALI KUOANA NA MTU HADI UWEZE KUMFAHAMU KTK NJIA TOFAUTI.
Unatakiwa kumfahamu vizuri huyo mwenzi wako mtarajiwa, mfahamu tabia zake kwa kadri unavyoweza.
Kutembea mmeshikana mikono miaka 10 ijayo kunategemea sana jinsi unavyomfahamu vizuri kabla ya kuingia naye kwenye ndoa.
6.USIOLEWE AU KUOA HUKU UNA MATARAJIO MAKUBWA SANA.
Ndoa kimbilio la faraja; inahitahiji kazi ya maana ili ikupe faraja.
Usiingie kwenye ndoa umeweka matarajio ya juu sana as if ni solution kwa shida zako zote kifedha, kihisia na kimaisha.
Hata kama sasa kuna mapenzi ya juu sana na una matumaini makubwa uwe makini kwani kila kitu kinaweza kuyeyuka kama barafu kwenye jua.
Kama unataka kuwa an ndoa imara jiandae kwa kazi iliyombele, kujitoa kutakuwa na maumivu, kuvumiliana, utakutana na changamoto ambazo inabidi ushindi na kuthibitishwa ili kuwa na true love kwa mwenzi wako.
7.USIKUBALI KUOANA NA MTU AMBAYE TABIA YAKE UNAHISI HUTAWEZA KUIVUMILIA MAISHA YAKO YOTE.
Kama kuna tabia Fulani ambayo hupendezwi nayo kama wivu, uchoyo, uchafu, hasira, uvivu, kutowajibika, siyo mkweli au msumbufu; jiulize kama utaweza kutumia maisha yako yote na yeye huku ukipambana na hiyo tabia.
Hiyo tabia mbaya kwake haitaondoka, kama unaomba muujiza abadili tabia hakikisha unatokea kabla hujaoana naye lakini si kuoana naye huku unajua kuna tatizo kubwa eti ukioana naye muujiza utatokea.
No comments