Wakati Mzazi Apatapo Mwenza Mpya
Muda wowote familia inapokutana na mwingiliano fulani hubadilika.
kutoka katika hali ya kawaida kama kifo, talaka, au kuongezeka mtu, kwa mfano kama kuzaliwa mtoto ndani ya familia, au kuna familia zingine baba kuoa mwanamke wa pili, au mama kuolewa na mume mwingine , wakati huo huo ana watoto tayari .
Hali hii huwa ni ngumu kwa kila mtoto au ndugu wa familia hio kukubaliana nayo. Hasa pale anapokuja kutambulishwa kama girlfriend au boyfriend , ni ngumu kwa watoto kiuambiwa huyu ni mama mpya , baba mpya.
Hivi karibuni ndugu mmoja alinielezea jinsi binti yake alivyomwita girlfriend wake malaya, mwehu, mzinzi, maneno ya ajabu yalimtoka huyo binti tena mbele za watu, hakuweza kuthibiti hio hali, watu walikuwepo wengi wamewazunguka, kulikuwa na hisia nyingi kwa kuwa ni mambo ambayo yalikuwa yanaumiza.
Kwa hio Utafanyaje kama mwanao amemtamkiwa maneno kama hayo mwenza wako?
Kinapotokea kitu kama hiki kwa sababu ya kupanic unaweza ukamuadhibu vibaya mtoto wako, bila ya kuchukua jukumu la kuongea naye kwanza . Unaweza kuona umefanya vizuri wakati huo lakini je utakuwa umetengeneza au umeharibu zaidi.
Makwazo hayana budi kuja , lakini angalia usije ukatenda dhambi. usije ukaharibu kabisa. Jaribu kufungua akili yako ili uweze kuelewa vizuri kitu gani kimetokea , hata kama hujapenda kilichosemwa au kutendwa. Fikiri kwa kina sana utaona kitu gani kimeleta hasira kwa mtoto au watoto.
Vaa viatu vyao, vaa kiatu chake , ili uone kinaumiza namna gani au kinampa shida gani huyo mtoto. Hapo ndipo utakapoelewa jinsi gani alikuwa na hasira mpaka kutamka au kufanya jambo kama lililotokea hapo.
Ni ngumu sana kumkubali mtu mpya kwenye maisha yao kama walikuwa na mama yao au baba yao , lakini sasa wakiangalia hayupo tena kwa sababu moja au nyingine. watakuwa wanamwangalia mtu mpya kama ni mshindani wao , kama atapunguza mapenzi yako kwao, kama vile watakosa nafasi kwako. wanaweza kufikiri kwamba hutaweza kuwahudumia tena, au wataona kama vile ni badala ya baba yao au mama yao, ni ngumu kukubali kirahisi.
Kama ukjijikuta katika hali hio au mazingira kama hayo, njia pekee iliyo bora ni kukaa na kuongea nao ili uweze kujua tatizo. Anza kwa kutambua hasira iliyopo. waulize ni kitu gani kinawafanya wawe na hasira , utakapoelewa , waulize wanajisikiaje kuwepo na mwenza wako mpya.
Wape nafasi ya kuongea ili waondoe woga walionao , baada ya kumaliza kile ambacho kilikuwa kinafanyika kwao. Utaona unaanza kupata majibu ya matumaini. Au tafuta njia ya kuwafanya wote wakae katika hali ya kujisikie salama . wahakikishie kwamba hakuna kitakachobadilika, umuhimu wao kwako upo palepale haijalishi kuwa na mwenza mpya. utakuwa karibu yao kila mara na kuwasikiliza vizuri.
Unapotengeneza nafsi kubwa kwa ajili ya watoto wako, na kujua hisia zao, ni hatua moja kubwa sana ya kumtengenezea mwenza wako mpya nafasi yake ya kukubalika kwenye familia yako maisha yako yote. Mara tumaini hili likiwepo watoto wataanza kumkubali mwenza wako na kujiona kama hawakupotelewa na mtu bali wapo kawaida.
Natumaini kwa wale wenye mazingira haya magumu wameelewa vya kutosha. Nikupe tu angalizo . Bila Mungu Hutaweza kufanikisha haya yote . Kila jambo lako mshirikishe Mungu akufanyie wepesi .
No comments