CHOMEZO MALKIA WA JELA SEHEMU YA NANE
SEHEMU YA NANE
.............................. ......
Baada ya siku kadhaa kupita ndani ya gereza kuna mfungwa mpya aliletwa na askar na kuingizwa gerezan alikuwa ni mama wa makamo flan mwenye mwili mnene rangi ya kunde na mrefu kias akiwa ndan ya jezi ya rangi ya chungwa iliyofanania na za wenzie Baada ya LINDA kumwona yule mama ameingizwa mule ndan alinyanyuka mahala alipo kuwa amekaa na kumsogelea pale karbu na mlangon alipokuwa amesimama yule mama LINDA alifika na kuanza kumzunguka huku akimtizama juu na chini "Mamaa Kubwaaa Mmmmh! Nakuona karibu paradise Hahhahjahahaha " a lounge a LINDA huku akionekana kumdhihaki mama yule "Utazoea tu Aam labda kabla tu hatujakupatia siti ningependa upate utambulisho kidogo ambao utakusaidia hili mwisho wa siku usije sema hujalijulishwa " aliongea LINDA na kuwageukia wafungwa wenzie na kuwauliza yeye ni nan "Naomben mu mwambie mapema Kwa sauti Mimi ni nan ?"
Yule mama alikuwa akimtizama msichana LINDA Kwa hasira
"Mimi ni nan ?" Aliuliza Linda
"Malkia Wa Jela " ilisikika saut Kama ya watu wanne hivi huku wengine wakionekana kukaid amri ile
"Anhaaa! Sasa kwa kuwa hamtak kusema mtasema kwa lazima Alianza kumtembelea mmoja Baada ya mwingine huku wale wanne aliowaona wakisema akiwa amewasimamisha na kuwatenga pembeni walipokwisha kusema wote kuwa yeye ni Malkia Wa Jela Alimsogelea tena yule mama " Mama nadhan Kama tu hujaelewa naiman utakuwa umesikia .......Unaweza kunambia Mimi ni nani ? LINDA alimwambia mama yule huku akimtaka arudie kusema Kama walivyosema wenzie lakin mama hakuwa tayar LINDA alimkamata mama Taya kwa kutumia mkono wake wa kulia "Anhaaa ! Kumbe wewe jeur siyo !.. Inamaaana hujasikia walichokisema Mimi ni nani " aliongea a LINDA kwa hasira mama yule alimtoa mkono LINDA "We Binti kuwa na abadu mm n sawa na mama yako mzaz jaribu kuwa heshima na mim tena usinizoee " aliongea yule mama akionekana waz kuchukizwa na kitendo kile "Eeeeh ! Ushakuwa mwenyej siyo ila siyo mbaya kwa kuwa Leo ndo siku yako ya kwanza kuwa huru kuongea lolote ila kesho utajua vzur mm n nan karibu humu wote watu wazima lakin ningekuwa binti nisingekuwa humu karibu tena mama Kubwaa Malkia wa jela niko hapa " Baada ya LINDA Kumaliza kutamba alirud na kukaa chn Palipo pambazuka na wafungwa wote wakiwa wanafanya usafi wa kusafisha mazingira yule mama alikuwa bado amejikalia peke yake ndan ya gereza Huku LINDA akiwa kwa nje anasimamia arijaribu kuangaza huku na huku akimtafuta yule mama akatikisa kichwa na kuamua kuondoka kuelekea ndan ya chumba cha gereza na kuweza kumkuta yule mama amekaa peke yake "Mmh mama hukuja huku kukaa tu kuna kaz za kufanya huko nje " aliongea LINDA Yule mama alimtizama na kucheka kisha kuinamisha kichwa chini "Kondoo Eeh ! Husikii nachoongea au hapo unatakiwa unyanyuke ukafanye kaz "
"Binti hapa sinyanyuki kas sifanyi nimekuja kutumikia kifungo na siyo kuja kufanya kaz uraian nimefanya Sana tu nanilikuwa nalipwa " aliongea yule mama akionekana kujiamini "Kumbe wewe jeuriii Ngoja nikakuletee Dawa " LINDA alimtizama kwa hasira na kuondoka kuelekea moja kwa moja katika ofisi ya Afande MUGA "Vipi kunatatzo lolote " aliuliza afande baada y a LINDA kuingia ghafla pasipo kubisha hodi "Baby kuna mtu hatak kabisa kufanya kaz na ananijibu vile atakavyo " kwa sauti ya madeko aliongea LINDA "Anajipenda kweli huyo tangulia nakuja "
"Nataka twende wote Baby "
Afande aliamua kutoka na kuongozana na LINDA mpk ndan ya gereza Yule mama alipomwona afande alinyanyuka upesi "We mmama kwanini unakuwa mkaid Umeambiwa humu umekuja kustarehe...Unaleta kibur ?
Yule mama alijibu kwa kutikisa kichwa huku akitetemeka "Haya haraka ukwende Nje kufanya usafi Unamdharau kiongoz "
Yule mama alitoka mbio kuelekea nje "Hahahahaahaahhahhahha " LINDA aliangua kicheko
"Hawa watu wadogo Sana siyo wa kubishana nao akijaribu kubisha tena we niite "Aliongea afande MUGA
"Mmmh ! Sawa halafu kuna kitu nataka nikwambie "
"LINDA we nambie tu "
"Aaaam ! baby ni Muda sasa sizion siku zangu na kwa hali ambayo naiona ninayo nahisi nimeharibu mambo"
"Sielew unataka kuongea nn naona unazunguka we nambie moja kwa moja Wewe ndo MALKIA WA JELA nan mwingine Kama siyo wewe uhitaj shida kabisaa "
"Baby mm nahisi Nina mimba "
"Eti ! Hahaha LINDA Hapana Ivi unawezaje kujiachia namna hii utadhan upo uraian Unataka kuniharibia kazi cyo "
"Sikia wewe tena usitake kunipanda kichwan MUGA nan siku ile alimbaka mwenzie nilihitaj mm unifanyie kitendo hiki "
"Niite afande usiniite MUGA naona sasa mazoea Kama yamezid we mwanamke "
"Mmh! Sasa kwa taarifa yako siri hii nitamwambia kila mtu nitaomba nionane na mkuu wa magereza nimweleze kuwa ulinibaka afu tuone utaishia wapi Kama siyo segerea "
"Basi usifike huko naomba ufanye kitu kimoja tu nakuomba hiyo mimba tuitoe "
"Hahahaahhha unawazimu nin sitoi mimba wala mama ake mimba "
"Utaniingiza kwenye matatizo ujue "
"Wakat unafanya hukujua kuna matatzo "
Afande MUGA aliamua kuondoka na kuelekea ofisini kwake huku tayar kichwan kwake akiwa na maswal mengi juu ya jambo lile
Baada ya siku kadhaa kupita afande MUGA aliamua kumwita LINDA ofisin kwake na kuongea nae juu ya suala la ujauzito
"Sikia LINDA utakapo kataa kuitoa hyo mimba na bado inaendelea kukua wakija kujua utaniharibia kaz "
"Leo ndo unaliona hilo ukumbuki Mimi na we we ni nan aliyemlazimisha mwenzie Mimi sipo tayar kufa kifungo nilichopewa kinanitosha kabisa kwa hilo sipo tayar "
"Mmmh! Haya ukijulikana utasema nini ?
"Mimi n mtu mzima najua n namna Gan ntasema "
"Ila bado unajidanganya kwann usifanye nnalokwambia Kakae ufikirie ukiwa tayar kuna dokta ntaongea nae tutakwenda "
"MUGA usinitafutie matatzo "
"LINDA au umechoka uongozi ?"
"Bado nataka "
"Basi nenda kafikirie vizur halafu ntakutafuta tuongee "
LINDA aliondoka na kurud ndan ya chumba cha gereza kisha kwenda kukaa pemben ya rafiki yake PENDO
"PENDO kuna jambo nataka unishaur?
"Jambo Gan tena ? (Kwa mshangao)". "Afande MUGA anataka niitoe hii mimba "
"Eeeh ! (PENDO alishangaa kwa sauti akaangaza huku na huku Wafungwa wenzao wakawa wakiwatizama ) PENDO aliamua kumnong'oneza na kumtaka asifanye kitendo hicho
Katika Maeneo ya nyumban kwao LINDA mama yake akiwa na mdogo wake AMANDA "Dada muda Una kwenda lini tunaenda kumwona LINDA ?
"mmmh! Hali yangu nadhan unaijua AMANDA nusu nife siku ya kesi yake sasa nikienda kule nikirud tu hospitalin moja kwa moja "
"Lakin atajisikia vibaya Dada "
"Mim yule n mwanangu ananijua vizur Jambo dogo tu hali yangu haichelew kubadilika miaka mitatu siyo mingi ngoja tusubir akimaliza tutamfuata nikijua anarud nyumban lakin naenda kumwona halafu narud mwenyewe uzaz unauma we zaa uone "
"Basi yaishe Kesho nataka nirud kwangu "
"Nimekuudh lolote mbona haraka ivo unajua kabisa Niko mwenyewe "
"Hapana Dada wala hujaniudh ila ninatakiwa niende kuangalia panaendeleaje kumbuka hakuna mtu kule "
"Sawa lakin unaniachaje peke yangu "
"Dada sasa wewe unaogopa je mm wakirud walioniteka "
"Hebu usiongelee hayo mambo "
Wiki moja baadae LINDA akiwa anasimamia wenzie wakiwa wanafanya usafi Alikuja Afande na kuondoka nae Kisha kwenda kumkabidhisha kwa Afande MUGA "LINDA umefikia wapi ?"
"Siko tayar kuitoa hii mimba nasihitaj unilazimishe ukifanya ivo nitamwambia kila mtu ajue hili halafu tuone utaoshia wapi " LINDA aliongea kwa ukali "Sasa kwanini unakuwa mkali unataka watu wajue unataka kuni haibisha siyo nisikilize wewe si mjanja ila Mimi mjanja zaid yako nakupa siku ya Leo Kama hutokubali nitaitoa kwa mikono yangu ikitokea ukapoteza uhai kwa kitendo nitakachokufanyia nitakuzika Mimi mwenyewe hakuna hata mmoja atakae jua "
"Hizo kelele za chura tu najua huwez kufanya ivo Kama kweli unajiamini Fanya " LINDA alipomaliza kuongea aliamua kuondoka Afande MUGA alijaribu kumwita lakin LINDA hakuwa Tayar kabisa kurud Moja kwa moja LINDA alielekea katika chumba cha gereza huku akiwa amejawa na hasira baada ya kuingia alishangaa kumkuta yule mama mule ndan ikiwa alikuwa nje akifanya kaz na wenzie "We mama siyo bure kuna ambacho unakitafuta kaz ulizoacha huko nje nan akufanyie "
Yule mama alinyanyuka kwa Shari "Tena koma binti usinione navyo kaa kimya nakuogopa huo Unyampala wako usitupande kichwan nimepinda ile ile shika kabisa adabu yako sikaja huku kwa bahat mbaya kuwa na heshima "
"Usinitishie Mimi n kiongoz wako utafuata chochote nitakacho utaenda au hutoenda "
"Siend wala sitokwenda "
"Mmmh sawa " LINDA aliondoka na kwenda kumwambia Afande MUGA lakin Afande MUGA alikataa kwa kuwa LINDA hakuwa tayar kufuata anachotaka LINDA alirud tena kumtaka yule mama atoke nje akafanye kaz wakiwa wanaendelea kuzozana kuna mfungwa mmoja alikuja na kuwashuhudia alitoka anakimbia na kwenda Kumwita PENDO walikuja na kujaribu kuwaamua lakin haikuwa rahis kila mmoja alikuwa juu wafungwa wenzao walipomwona PENDO ameijiwa haraka moja kwa moja walijua kuta kuwa na kitu waliamua kuacha kufanya kaz na kuondoka wakielekea Ndan ya gereza kujua nn kinaendelea LINDA walishikana Name yule mama wakitaka kuanza kurushiana ngumi PENDO alijitahd kadir ya uwezo wake kumwomba rafik yake LINDA asiweze kugombana lakin yalikuwa yanapita wafungwa wenzao walipofika walianza kushabikia ugomvi ule PENDO baada ya kuona ivo aliamua kutoka kwenda kumwita afande Mmoja wa Mfungwa aliyejulikana kwa jina la FIONA alisogea na kumshika mkono LINDA na kumtaka asigombane LINDA alimsukuma kwa nguvu na kumtoa mkono Kwa bahat mbaya FIONA alifikia ukutan na kujikuta kichwa chake kikifikia ukutan Ulisikika mshindo ghafla Kelele zote zilizokuwa zikisikika ndan ya gereza zilipotea ghafla Kila mmoja akashika kichwa na kinywa waz PENDO alipofika na afande muda huo LINDA akitetemeka na kutokwa na machoz huku akiwa karbu na mwili wa FIONA,Mahakama iliamua kumfungulia upya kesi ya mauaji LINDA Na kuomba siku itakayosomewa ndugu zake wawepo Mama yake pamoja na Amanda waliweza kufika Maeneo ya Mahakama kusikiliza Mahakama Itaamua kitu gani Mahakama Iliamua kumhukum LINDA kifungo cha Maisha ambacho atatumikia akiwa ndan ya gereza atakalo hamishiwa huku na adhabu kali zitafuata dhidi yake Mama yake alikuwa akilia ovyo kwa saut na kushindwa kujizuia AMANDA alikuwa akijitahid kumnyamazisha Baada ya hukumu ile kutolewa LINDA aliomba aongee jambo na mahakama Ikamkubakia kutaka kusikia anachokwenda kuongea ni kitu gani "Najua imeshatokea Sina Budi Kukubaliana na kosa ila hii yote ni tamaa tu ndo ilofanya niwe hapa tena " wakat huo akiongea Afande MUGA kwa pemben alikuwa akijaribu kumpa ishara LINDA asiweze Kusema kuhusiana na Mahusiano yao "Mimi Naenda gerezan kutumikia kifungo cha maisha nikiwa na mwanangu Tumboni " Watu waliokuemo mule ndan ya mahakama wote walishangaa "Najua itawashangaza Sana ila huo ndo ukweli mm n mjamzito Nilidanganyika Mimi kwa tamaa ya kuwa huru na uongoz " Afande MUGA alikuwa akijirabu kumwomba LINDA kwa ishara asiseme "Afande MUGA usinizuie acha niseme " Baada ya LINDA kuongea vile macho yote ya watu yalimtazama afande MUGA huku wakijiukiza katenda kitu gani "Mahakama afande MUGA si mtu mzur kabisa katika jeshi lenu la polisi yupo kwajili ya kuwashushia heshima na yeye ndo mhusika wa ujauzito huu aliniongopea meng tu na alishawah kunitoa nje ya gereza na kwenda kula raha na huko ndipo aliponiingilia kimwili kilazima bila ridhaa yangu Namchukia sana Afande MUGA Polisi walisogea na kumkamata afande MUGA na kumfunga pingu LINDA alitolewa kizimban na kuambatana na Afande MUGA kuelekea katika gari la magereza Mama yake LINDA aliomba aweze kuongea na mwanae alipewa Dakika tano lakin hakuweza kuzitumia Alipojaribu kutaka kuongea aliishiwa na nguvu na kuanguka chini LINDA alipojaribu kutaka kurud alizuiwa na kuweza kupandishwa kwenye gar AMANDA alibakia akilia na kujaribu kutafuta msaada wa kumpeleka Dada yake hospitali Afande MUGA jeshi la polisi lilimfukuza kaz kwa kulitia aibu na kupelekwa gerezan kwa kutumikia kifungo cha miaka kumi Mama yake LINDA alipatwa na kiharusi na kushindwa kufanya shughul yoyote ile ikambdi AMANDA kuhamia nyumban kwa Dada yake kwaajil ya kumsaidia
------------------- MWISHO ----------------------------
.
Toa maoni yako kupitia
Instagram : @abbykamchoro
Facebook : abbykamchoro
WhatsApp : +255766025554
Mh : Simuliz hii ni yakufikirika ili kuwapa burudan haihusian na maisha ya mtu yeyote yule
No comments